Inakuwaje CCM ndiyo wanauchoka uenyekiti wa Mbowe?

Inakuwaje CCM ndiyo wanauchoka uenyekiti wa Mbowe?

Najiuliza tu maana kuutamani uenyekiti pale chadema imekuwa kama jinai na anayetamani lazima akimbie chama. Ni vema chadema wakaiga utaratibu mzuri kutoka CCM was kubadilishana vijiti vya uongozi kwa amani na upendo. Ni hayo tu, ahsante!
 
Najiuliza tu maana kuutamani uenyekiti pale chadema imekuwa kama jinai na anayetamani lazima akimbie chama. No FEMA chadema wakaiga utaratibu mzuri kutoka CCM was kubadilishana vijiti vya uongozi kwa amani na upendo. Ni hayo tu, ahsante!
Ile cdm ni kampuni ya mtu binafsi kwahiyo kama sio sehemu ya familia au mkwe huwezi kupata uenyekiti. Na ukilazimisha sasa ndio wanakuvalia uninja
 
Kuna siku moja nimemtumia bandiko moja kuelezea kuhusu Chadema.

"KWA WANAOAMINI KUWA CHADEMA NI CHAMA CHA UPINZANI NCHINI BASI WANAWAZA OVYO SANA. MBOWE SIKU AKIONDOKA ATAACHA MTU AMBAE ANAJUA NINI LENGO NA UWEPO WA CHADEMA NCHINI"

KAMWE HAITATOKEA CHAMA CHOCHOTE KILE HAPA NCHINI KITAPEWA NAFASI YA URAIS ISIPOKUWA CCM, LABDA YAYOKEE MAPINDUZI YA KEJESHI.

"CHADEMA SIO CHAMA CHA UPINZANI JAMANI"
 
Naomba kufahamishwa ni lini ma ccm yaliwahi kufanya uchaguzi wa mwenyèkiti wao kitaifa ?

Na wagombea walikuwa nan na nani ?
 
Haaaaaahaa ukijibiwa unitag mkuu.
Hawajawahi kujibu. Na wale waliojitwisha zigo la kukitetea chama hicho kwa mwavuli wa kujifanya hawana upande, nao pia utasikia CHADEMA isijifananishe na CCM kwa kuwa chenyewe kinapaswa kuwa tofauti. Kikiwa tofauti kinalaumiwa kwa kuwa tofauti.
 
Na ndiyo maana kila wakati nashangaa ni kwa nini kila wakati CCM inapoelekea kushindwa huwa inatengeneza mazingira ya kuendelea kuongoza (kutawala).
CCM ina utaratibu wa miaka kumi kwa mwenyekiti kuongoza, kwa kufanya hivyo inakuwa inaliishi neno mapinduzi. Kwa kufanya hivyo chama kinakuwa kinaiishi demokrasia.

CDM inalo neno demokrasia lakini tangu kaka Aikaeli aingie madarakani mwaka 2004 ni kama hilo neno lipo lakini kivitendo halipo.

Kibaya zaidi kwa CDM ni kwamba kadri siku zinavyokwenda kinakuwa ni chama kisicho na substance, kinakosa uhalali kwa sababu uongozi wa juu hauna ubunifu unaoendana na mabadiliko mazima ya kimaisha.

Hiyo gia ya CCM kuonekana ni chama kinachobeba uonevu na dhuluma inakuwa ni gia isiyo na mashiko kwa jinsi ambavyo demokrasia ndani ya CCM inavyoleta watu wenye msaada wa moja kwa moja kwenye maisha ya mtanzania wa kawaida.
 
#MAKAVU Live
Uzwazwa wa Chama cha Kijani ni Kuendelea Kumshambulia MBOWE Kuwa ni Mwenyekiti DHAIFU; Eboo! ADUI akiwa DHAIFU sio ndiyo unaweza ku-capitalize katika udhaifu huo?
Amini nawaambieni ukiona maneno na mashambulizi ya namna hiyo yanatoka kwa mpinzani wako na hasa wa kisiasa, ujue hana jipya zaidi ya HOFU ya "Potentials" zako.
Raha ya CCM ni kuona upinzani dhaifu na legelege; Sasa kama Mbowe anabeba sifa hizo si muacheni kwenye chama chake? Aue chama hicho ili muendelee kutamba na "tambo mfu za kutawala milele"
Mnazuiaje mikutano kama MBOWE akiwa ndio Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani ni dhaifu? Mnajitekenyaaa, kisha mnachekaaaa! Halafu mnachekwaaaa, mnachekwaaa, mnachekwaaaa!!
Jambo la kuona WanaKijani hawa ni mazwazwa ni pale unapoona LIPUMBA, MREMA, DOVUTWA, CHEYO nk. wote wamekaa kwenye nafasi ya Uenyekiti kwenye vyama vyao zaidi ya miaka 20, hii ni zaidi ya ile ya Mbowe ambaye amekaa chini ya miaka 14! Na kwa vipimo halisi waliotajwa hao (MREMA, LIPUMBA, CHEYO na DOVUTWA) huenda wakawa Wenyeviti wa vyama ambao ni dhaifu katika ukanda mzima wa Jangwa la Sahara Kusini na Kaskazini, Lakini kwa KIJANI, hao ambao ni dhaifu wanaendelea kuwapendaaaaaaaaaaaaa!!!!
 
Habari zenu wana jamvi. Mara nyingi nimefuatilia threads zinazomshinikiza Mbowe aachie ngazi. Tena hoja zinazotolewa ni za kitoto tu. Halafu nikifuatilia watoa threads naona ni wa mlengo wa kulia. Swali langu ni je, kama kweli kuachia ngazi kwa Mbowe kutakuwa na faida kwa CDM ni kwanini shinikizo litoke without na sio within? Tangu lini CCM ikaitakia mema CDM? najiuliza tu.
 
Bavicha mko kwa ajili ya Mbowe na siyo kwa ajili ya chama cha chadema.


Mko tayari chadema ife kabisa ila mbowe abaki salama.!!
Hapao ndipo usomi wenu unakuwa wa hovyo na wa kutia mashaka.

Pauline Gekul, Mwita waitara , Katambi, Zito Kabwe , Kitila Mkumbo ,Chacha Wangwe wote wamefukuzwa Chadema na kupata matatizo kwa kutaka Mbowe aondoke madarakani walikuwa ni ccm?
Ni ccm yupi anayetaka mbowe aondoke madarakani?

Bavichaa mmebuni mbinu ya kumlinda Mbowe kwa kujificha kwenye kivuli cha ccm??
 
Ujinga ni kumtetea Mbowe, wakati mnajua kabisa kavunja katiba ya Chama kwa kupitiliza ukomo wa Uongozi.

Chadema sio Saccos kwamba mtu anaweza kuendesha maisha yake yote, Chadema ni Chama cha wananchi kinachoendeshwa na kodi za wananchi....hivyo sheria lazima zifuatwe kwenye uendeshaji wake.

Naona wafuasi wa Mbowe mnavyohangaika kumpa uhalali boss wenu kuendelea kutafuna ruzuku.

Mara Kubenea,Kom ama CCM hamjui mchawi wa Mbowe ni Mbowe mwenyewe.... Demokrasia tunayoililia kila siku lazima tuwe tayari kuiishi hata kama Chungu.
 
Bavicha mko kwa ajili ya Mbowe na siyo kwa ajili ya chama cha chadema.


Mko tayari chadema ife kabisa ila mbowe abaki salama.!!
Hapao ndipo usomi wenu unakuwa wa hovyo na wa kutia mashaka.

Pauline Gekul, Mwita waitara , Katambi, Zito Kabwe , Kitila Mkumbo ,Chacha Wangwe wote wamefukuzwa Chadema na kupata matatizo kwa kutaka Mbowe aondoke madarakani walikuwa ni ccm?
Ni ccm yupi anayetaka mbowe aondoke madarakani?

Bavichaa mmebuni mbinu ya kumlinda Mbowe kwa kujificha kwenye kivuli cha ccm??
Swadaktaaa!!!!! umeongea ukweli mnoo. Hiki ndicho kinachofanyika ili kuficha mgogoro unaondelea ndani ya Chadema. wanaotaka mbowe aondoke wapo ndani ya Chadema tena wengine wapo kwenye Kamati kuu.
 
Back
Top Bottom