Inakuwaje CCM ndiyo wanauchoka uenyekiti wa Mbowe?

Inakuwaje CCM ndiyo wanauchoka uenyekiti wa Mbowe?

1. Mbowe amekaa mda mrefu sana madarakani, anaiua chadema.
2. Mbowe haambiliki!!!
3.Hawana ofisi za chama.
4. Mbowe mpigaji.
Na bhlaaaa blaaaa ...... nyingi ......
Hivi Mbowe na Lipumba, Cheyo na Mrema nani kakaa kwenye uwenyekiti kwa mda mrefu?
Mbowe na jiwe nani haambiliki?

Hivi hii ni huruma ya CCM kwa CHADEMA au ni mbinu tu ya kumtoa Mbowe kwa sababu wameshindwa kumfanya kama Lipumba, Mrema au Cheyo?
 
Mbowe ataondoka itakapothibitika pasi na shaka kuwa yupo wa kumrithi na sababu ya kumrithi.

Kama na Uenyekiti, hata TLP, UDP, CUF(propesa) etc, Wenyeviti ni walewale! iweje CDM ndio nongwa.

CHADEMA fanyeni mabadiliko kwa kujitathmini na kwa umakini kama ipo haja!
Huyu fisi anayewafuatilia hatawaacha salama!
 
Mcha Mungu ukiona siku moja shetani anakusifia kwamba wewe ni mcha Mungu then jiulize mara mbili mbili, hali kadhalika kwenye hili la Chadema na ccm kwenye uenyekiti
 
Lengo la CCM na serikali ni kuona Chadema ikipata mwenyekiti dhaifu dizaini ya kina Lipumba, Cheyo, Mrema na mama Mgwhira ili wapate chance ya kukisambaratisha.

Mbowe ana msimamo, ni mpinzani halisi, kimsimamo hana tofauti na Seif. Ana hekima, ana busara hakurupuki anajua nini chama chake na wafuasi wake wanataka, hana jaziba wala visasi kama mwenyekiti wa upande wa pili. Kuongezea hapo Mbowe hana njaa za kijinga ana biashara zake, hanunuliki. Wamejaribu kuharibu mali zake wakafikiri atalegeza msimamo, TRA wamembambikia kodi kalipa, NHC wamebomoa Bilicanas wakafikiri ndiyo biashara yake pekee.

Mbowe sio Mrema wa kudanganywa kwa cheo mbuzi, kwa Mbowe CCM watakesha sana na naomba wajumbe wa mkutano mkuu wa Chadema uchaguzi utakapofika wamchague tena kwa kura zaidi ya alizopata tuwashangaze mahasimu wake.
That is why i love JF, yule msukuma Ngabu alidhani kaanzisha idea mpya humu.Jinga kabisa.
 
Hii ni mbinu ya kutaka mbowe asiwepo kwenye siasa, wanaamini akiachia uwenyekiti basi atapotea kisiasa, nia yao ni kuiuwa chadema kwa hio asikuambie mtu wanaosema aondoke sio watu wema, iweje mtu anaekutakia mabaya akushauri jema?
 
Hii ni mbinu ya kutaka mbowe asiwepo kwenye siasa, wanaamini akiachia uwenyekiti basi atapotea kisiasa, nia yao ni kuiuwa chadema kwa hio asikuambie mtu wanaosema aondoke sio watu wema, iweje mtu anaekutakia mabaya akushauri jema?
Ni wajinga sana halafu wanasahau mapema mno! Yani mijitu inatokwa mipovu kabisa humu ya ccm eti inalilia mabadiliko chadema!Mijinga sana hii mijitu!
 
Kafanya mengi mazuri sana tu na amekitoa chama mbali, lakini kwa ustawi wa chama, anaweza kubaki kuwa mshauri wakajaribu mtu mwenye mbinu mpya.
Na mimi nakuuliza swali, kwa kufuata mazingira ya siasa yalivyo hapa nchini ni nani anafaa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa badala ya Mbowe?
 
Anazungumziwa Mbowe kwa sababu ni kiongozi wa chama ambacho muda wowote kinaweza kuwa mbadala wa CCM.
Ndiyo maana Mbowe huwa anasema kwamba CHADEMA ni mpango wa Mungu. Hivi wewe uliwahi kudhani iko siku utaandika maneno kama haya JF?
 
MBOWE kisiki kile. Kuongoza chama cha upinzani hasa Tanzania ni kujitoa; lolote na liwe!! High risk lakini kamanda kakubali yote.
 
Na mimi nakuuliza swali, kwa kufuata mazingira ya siasa yalivyo hapa nchini ni nani anafaa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa badala ya Mbowe?

Unapoanza kunipa majukumu ambayo kuna watu wanalipwa na kuendesha maisha kwa hizo kazi sio sawa. Kama chama kina mtu mmoja tu anaeweza kuwa mwenyekiti sio tatizo langu. Kumbuka hata mimi napigania upinzani imara.
 
Ndiyo maana Mbowe huwa anasema kwamba CHADEMA ni mpango wa Mungu. Hivi wewe uliwahi kudhani iko siku utaandika maneno kama haya JF?
Ndio maana msisitizo wangu wa maadili mema ndani ya CDM unapokuwa muhimu zaidi.

Haiwezekani CDM ikapewa nchi halafu mwenyekiti wake kila anapotakiwa kuachia ngazi anatengeneza mazingira ya yeye kuendelea kuongoza chama.

Uongozi wa nchi unahitaji nidhamu kubwa. CDM ikiwa kama mfaidikaji wa kodi ya wananchi ni lazima kiwe chama ambacho utendaji wake unaakisi maadili ya taifa zima.
 
Unapoanza kunipa majukumu ambayo kuna watu wanalipwa na kuendesha maisha kwa hizo kazi sio sawa.
Basi tusubiri wanaolipwa kwa kufanya kazi ya kutafuta mbadala wa Mbowe wafanye kazi yao. Kila mtu anataka na kupenda kuwe na upinzani Imara!!
 
.Haiwezekani CDM ikapewa nchi halafu mwenyekiti wake kila anapotakiwa kuachia ngazi anatengeneza mazingira ya yeye kuendelea kuongoza chama.
Na ndiyo maana kila wakati nashangaa ni kwa nini kila wakati CCM inapoelekea kushindwa huwa inatengeneza mazingira ya kuendelea kuongoza (kutawala).
 
Back
Top Bottom