Inakuwaje hadi watu 155 wanafariki Kwa mafuriko, wananchi hatupewi taarifa, hadi Waziri Mkuu atuhabarishe?

Inakuwaje hadi watu 155 wanafariki Kwa mafuriko, wananchi hatupewi taarifa, hadi Waziri Mkuu atuhabarishe?

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
15,843
Reaction score
31,057
Tumemsikia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akitoa taarifa bungeni Leo, kuwa mafuriko hapa nchini kote, tokea mvua za masika za mwaka huu zianze, yamesababisha vifo vya jumla ya watu 155!

Hizi habari tulipaswa sisi wananchi tupewe taarifa na vyombo vya habari nchini, kuanzia kifo Cha kwanza hadi vinafikia vifo, tulivyotajiwa Leo, kuwa ni vifo 155

Tunajiuliza pia, hivi vyombo vya habari hapa nchini, pamoja na kuelezwa viko huru, je huwa vinawekewa na watawala "speed governor" ya nini Cha kuripoti??

Kwa kuwa hao waliofariki ni watanzania wenzetu, Kwa hiyo ni muhimu taarifa hizo zikawa za wazi Kwa wananchi wote, badala ya kuwa "Siri" Kwa watawala wetu pekee!

Tunapaswa tujirekebishe, iwapo kama Taifa, tunataka kweli kuhesabika kama Taifa lenye utawala Bora lenye uhuru kamili wa vyombo vya habari.

PIA SOMA
- Kassim Majaliwa: Watu 155 wamepoteza maisha na wengine 236 wamejeruhiwa kutokana na Mvua za El nino
 
Sometimes usikute wewe ndo hujafuatilia, hivo vifo from Hanang
 
Labda kuwepo na thread ya kutoa hizi taarifa.

Yule wa kutoa taarifa za ziara za Mhe. Rais nje ya nchi kaishia wapi?
 
Tumemsikia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akitoa taarifa bungeni Leo, kuwa mafuriko hapa nchini kote, tokea mvua za masika zianze, yamesababisha vifo vya jumla ya watu 155...
Yaani kwa akili zako zilivyo ‘ndogo’ unataka vyombo vya habari na social media viache ku report habari za Makonda eti zika report habari hizo!? Upo serious kweli au unatania tu?
 
Ukitaka kuficha jambo Mtanzania asilijue, basi liweke kwenye maandishi
"Ukitaka kumficha mwafrika weka ujumbe kwenye vitabu ,mimi natumia mziki kufikisha ujumbe kwa watu ,usitembee peku peku bila kuvaa viatu,kitaa wananiamini kama kiongozi wa dini,nawakilisha kitaa yaani kuliko hata wabunge,mimi ghetto super star ukombozi wa nini,Mie mtoto wa kichaga desturi yangu ku-hustle usinletee upimbi kwenye maswala ya shilingi,sibishani na promoter usipofika dau siimbi?" -Langa
 
Mafuriko yote hayo yasiwe na maafa?

Waandishi wanapiga picha maji tu ila huoni wakienda sehemu zenye maafa wala kuhoji, hovyo kabisa
 
Maisha ya Waafrika thamani yako ndogo sana, ingekuwa ulimwengu wa kwanza hadi CNN wangekuwa wanarusha
Hakika.

Maisha ya Mwananchi ni ya thamani sana, Kwa hiyo sisi watanzania tunapaswa kujulishwa
 
Yaani kwa akili zako zilivyo ‘ndogo’ unataka vyombo vya habari na social media viache ku report habari za Makonda eti zika report habari hizo!? Upo serious kweli au unatania tu?
Duh.......🙆

Hivi upo serious kweli?

Hivi unaweza linganisha habari za huyo "aliyefoji" vyeti Bashite na uhai wa watanzania??
 
Duh.......🙆

Hivi upo serious kweli?

Hivi unaweza linganisha habari za huyo "aliyefoji" vyeti Bashite na uhai wa watanzania??
Acha tu mkuu. Makonda ana team yake na ndiyo wanao control social media za bongo. Wanachofanya hivi sasa ni kama vile wana test mitambo tu.
Nape ni kama wameshakzidi nguvu, ingawa bado ana play smart.
 
Back
Top Bottom