Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Tumemsikia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akitoa taarifa bungeni Leo, kuwa mafuriko hapa nchini kote, tokea mvua za masika za mwaka huu zianze, yamesababisha vifo vya jumla ya watu 155!
Hizi habari tulipaswa sisi wananchi tupewe taarifa na vyombo vya habari nchini, kuanzia kifo Cha kwanza hadi vinafikia vifo, tulivyotajiwa Leo, kuwa ni vifo 155
Tunajiuliza pia, hivi vyombo vya habari hapa nchini, pamoja na kuelezwa viko huru, je huwa vinawekewa na watawala "speed governor" ya nini Cha kuripoti??
Kwa kuwa hao waliofariki ni watanzania wenzetu, Kwa hiyo ni muhimu taarifa hizo zikawa za wazi Kwa wananchi wote, badala ya kuwa "Siri" Kwa watawala wetu pekee!
Tunapaswa tujirekebishe, iwapo kama Taifa, tunataka kweli kuhesabika kama Taifa lenye utawala Bora lenye uhuru kamili wa vyombo vya habari.
PIA SOMA
- Kassim Majaliwa: Watu 155 wamepoteza maisha na wengine 236 wamejeruhiwa kutokana na Mvua za El nino