Inakuwaje mashujaa hawa walioinusuru TANU hawajaadhimishwa hadi leo?

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
PATWA%2B-%2BCopy.jpg

Mwalimu JK Nyerere na Bw. Patwas kualia kwake unapoitazama picha. Kulia mwenye koti na kofia Mzee Rashid Makoko Babu na wa pili yake ni mwanae Mamboleo Makoko na kushoto mwenye koti na kofia mzee Makata Mwinyimtwana.
Tarehe 23 Oktoba,1955 wanachama wa mwanzo wa TANU huko Tanga walikutana kuchagua uongozi wao chama. Hamisi Heri alichaguliwa kuwa mwenyekiti na Peter Mhando katibu. Jumla ya watu arobaini na tano walihudhuria mkutano huo na wakapewa kadi za TANU. Mwalimu Kihere alihudhuria mkutano ule lakini hakuchaguliwa katika nafasi yoyote ya uongozi. Kamati ya wanachama iliundwa kutokana na wale wanachama kumi na moja waasisi waliokutana katika ule mkutano wa kwanza mwezi uliopita. Kamati hiyo ilikuwa na wajumbe wafuatao: Abdallah Rashid Sembe, Mohamed Kajembe, Victor Mkello, Dhili Mgunya, Ali Mohamed, Abdallah Mohamed na Mohamed Sadik. Peter Mhando alijitolea nyumba yake kuwa ofisi ya kwanza ya tawi la TANU mjini Tanga. Mara tu baada ya mkutano huu wazee wa Tanga wakiongozwa na Makoko Rashid, mwanachama wa zamani wa TAA walianza kufanya kampeni kwa ajili ya TANU. Chama kilipata msukumo mwingine na kuongezeka nguvu wakati Sadik Ali Patwa Muasia tajiri alipoingia TANU.

20431205_2305043049522045_5715176440330895933_n.jpg

Patwa alikuwa Muislam wa madhehebu ya Shia. Patwa alikuwa amehamia Tanganyika kutoka Zanzibar mwaka 1918 baada ya kumalizika kwa Vita Kuu ya Kwanza. Pale Tanga Patwa alianzisha kiwanda cha soda na akatajirika. Wakati huo wa zama za ukoloni wakati Waasia wenzake walikuwa wakiwabagua Waafrika, Patwa alikuwa akikaa na Waafrika wa rika lake akinywa nao kahawa. Halikadhalika watoto wake wakawa wanacheza kandanda na vijana wenzao wa Kiafrika katika vilabu vya Tanga. Hili lilikuwa jambo geni na lisilokuwa la kawaida kutoka kwa familia ya Kiasia wakati wa ukoloni. Patwa alisaidia harakati za kudai uhuru kwa hali na mali, na akaifanyia kampeni TANU miongoni mwa jamii yake mwenyewe ya Kiasia. Wakati wa harakati Nyerere alikuwa akifanyiana maskhara na Patwa akimwambia, ‘’Mzee Patwa baada ya kupata uhuru nadhani tukuteuwe uwe balozi wetu India.’’ Lakini Patwa hakuiona Tanganyika huru, alifariki kabla ya uhuru kupatikana.

Baada ya kufungua tawi la TANU mjini Tanga, uongozi wa chama ulimwalika Julius Nyerere, Bibi Titi Mohamed, John Rupia na Mbutta Milando kufanya ziara Tanga. Nyerere alifikia nyumbani kwa Hamisi Heri. Ujumbe huu kutoka makao makuu ya TANU ulipata makaribisho makubwa yaliyoandaliwa na vyama vya lelemama ambavyo kwa kawaida vilikuwa vingi sana katika pwani ya Afrika ya Mashariki kutoka Mombasa nchini Kenya hadi Mikindani, Tanganyika. Kiongozi wa akina mama hawa mjini Tanga aliyesaidia kuieneza TANU alikuwa Bibi Mwanamwema bint Sultan, ndugu wa mbali wa mwenyekiti wa TANU Tanga, Hamisi Heri.

Matokeo ya ziara ya Nyerere Tanga ilikuwa ni kumrudisha Mwalimu Kihere katika siasa. Baada ya kushindwa kupata nafasi yoyote katika chama, Mwalimu Kihere alipoteza shauku ya siasa. Nyerere alipokuja Tanga kuifanyia kampeni TANU ndipo Mwalimu Kihere alikaribishwa kujiunga na chama. Mwalimu Kihere alifahamiana na Nyerere mwaka 1946 walipokutana Dar es Salaam katika mkutano wa mwaka wa African Association. Nyerere alipozuru Tanga Mwalimu Kihere alitaka kufanya dhifa nyumbani kwake kwa heshima yake. Uongozi wa TANU, hususan Hamisi Heri na Mzee Makoko walikataa kumruhusu Nyerere kuhudhuria dhifa hiyo kwa sababu Mwalimu Kihere alikuwa hajaonesha kuiunga mkono TANU. Nyerere akitambua utu uzima wa Mwalimu Kihere, uzoefu na sifa yake ya uongozi katika African Association, alishauri uongozi wa TANU Tanga usiache fursa ile ipite bure. Nyerere alitoa hoja kuwa, ilikuwa muhimu kukubali mwaliko wa Mwalimu Kihere na kutumia fursa hiyo kumuomba arudi kwenye harakati kwa kuwa TANU ingefaidika kutokana na uzoefu wake alioupata katika African Association. Kwa ajili ya nasaa hiyo TANU ilikubali mwaliko wa Mwalimu Kihere na Nyerere alihudhuria dhifa ile nyumbani kwa Mwalimu Kihere pamoja na wanachama wengine.

20479660_2305040996188917_2590609322615442244_n.jpg

Mwalimu Kihere

Mwalimu Kihere alikuwa mwanasiasa wa msimamo wa wastani, alikuwa mbali na msimamo mkali dhidi ya serikali. Kwa ajili hii Mwalimu Kihere alielewana vizuri na utawala wa kikoloni. Hii ilikuwa kinyume kabisa na wazalendo wengine kama Mzee Makoko Rashid ambaye kwa miaka mingi alijulikana kwa chuki yake dhidi ya Waingereza. Inasadikiwa kwamba watu wawili wataingia katika historia kwa chuki zao mahsusi dhidi ya Waingereza, mtu wa kwanza ni Abdillah Schneider Plantan na wa pili ni Mzee Makoko Rashid. Wote wawili walifungwa gerezani kwa sababu ya msimamo wao dhidi ya serikali ya kikoloni. PC na DC wake wote wawili walikukubali mwaliko wa Mwalimu Kihere. Mwalimu Kihere alimtambulisha Nyerere kwa wageni mashuhuri na alimuomba azungumze maneno machache. Nyerere kwa kipaji chake cha ufasaha wa kuzungumza alitoa hotuba kuhusu lengo la TANU na kanuni za kidemokrasia kama zilivyoelezwa na Umoja wa Mataifa. P.C. alisimama baada ya Nyerere kuzungumza na akatoa hotuba kwa niaba ya serikali. P.C. alimsifu Nyerere kuwa ni mwanasiasa mzuri kinyume na vile alivyosikia kabla ya kukutana naye. Hapo hapo alitoa ruhusa kwa Nyerere na TANU kufanya mikutano ya hadhara katika wilaya zote za jimbo hilo. Lakini uhusiano huu haukudumu, serkali iliyapiga marufuku matawi kadhaa ya TANU Tanga mara tu baada ya kuundwa kwa UTP.

Siku iliyofuata mabingwa wa hotuba wa TANU, Julius Nyerere na Bibi Titi Mohamed walihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Tangamano. Hii ilikuwa hatua kubwa sana kwa TANU, na kwa harakati dhidi ya ukoloni pale Tanga. Ilikuwa muda mrefu umepita tangu zile siku za zile siasa za wasomi katika Discussion Group, kikundi cha majadiliano; na ile mizozo baina yao na ule uongozi Waarabu katika TAA. Baada ya hapo, Mwalimu Kihere alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa TANU Tanga badala ya Hamisi Heri na Amos Kissenge alichaguliwa katibu. Abdallah Rashid Sembe mmoja wa wanachama waasisi wa mwanzo kabisa wa TANU alichaguliwa kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya TANU akiwakilisha Jimbo la Tanga.

Ilikuwa chini ya hali ya hewa ya kisiasa kama hii ndipo TANU iliingia kwenye uchaguzi wake wa kwanza katika Tanganyika, chaguzi wa Kura tatu wa mwaka wa 1958 Tanga ambako United Tanganyika Party (UTP) ilikuwa imara, TANU iliwachagua John Keto, B. Krishna na R. N. Donaldson kama wagombea wake. John Keto akiwa miongoni mwa walimu wa St. Mary’s School, Minaki na alikuwa amefanya kazi kubwa katika siku za mwanzo kufungua matawi ya TANU huko Kisarawe. TANU iliamua kumteua Keto kusimama Tanga ambako ndiyo kulikuwa kwao. Katika uchaguzi huu serikali iliacha uandikishaji wa wapiga kura kwa vyama vyenyewe. Mzee Makoko Rashid, mwanasiasa wa makamo mwenye msimamo thabiti wa chama na kijana Mmaka Omari walikuwa maofisa waandikishaji wa wapiga kura katika wa TANU mjini Tanga. Makoko na Mmaka walikamatwa na kushitakiwa kwa kosa la kuwaandikisha watu ambao hawakutimiza masharti yaliyoelezwa na ilani ya uchaguzi. Katika ghera yao kwa TANU kushinda ule uchaguzi muhimu, Mzee Makoko alimsajili Mwafrika yoyote aliyetaka kuipigia kura TANU bila kujali sifa zake. Bhoke Munanka alikamatwa vilevile kule Mwanza kwa kosa hilo hilo. Hakukuwa na ushahidi wa kutosha dhidi ya Mmaka Omari kwa hiyo aliachiwa huru mara tu baada ya kukamatwa kwake. Mzee Makoko Rashid alipatikana na hatia na alihukumiwa kufungwa jela. Adhabu ya kifungo ilidhoofisha sana afya yake na mara baada ya kufunguliwa kutoka gereza baya sana la Maweni Mzee Makoko alifariki.

Iweje leo hawa mashujaa hakuna kumbukumbu zao Tanga ukitoa Makoko Road. Hivi ule Mtaa wa Maua pale katika ya mji una akisi kitu gani? Dessa una sauti CCM wakumbushe na wazindue kuhusu historia hii kama hawaijui mimi nitakuja kwa nauli yangu kuja kutoa mhadhara In Shaa Allah.

Mkutano wa Tabora ulitishia kuigawa TANU katika makundi hasimu yaliyokuwa yakivutana, kama isingekuwa kwa ule mkakati uliopangwa kule Mnyanjani, kijiji kidogo nje ya mji wa Tanga. Waliopanga mkakati huo - Nyerere mwenyewe, Amos Kisenge, Hamisi Heri, mwenyekiti wa TANU Tanga, Mwalim Kihere mwanasiasa mkongwe wa African Association, Sheikh Abdallah Rashid Sembe, Ng’anzi Mohamed, Mustafa Shauri na Abdallah Makata - Hawa ndiyo waliinusuru TANU isinase katika mtego uliotegwa na wakoloni ambao ungeifanya TANU igawike katika mapande mawili na kila moja dhaifu kuweza peke yake kuikabili serikali ya kikoloni.

hongera kaka, mungu akujalie afya njema, wenyewe hawataki tujue wanahofu tutawadharau kwani wapiganaji ni wengine.Elimu yako ni faida kwa nchi hii, usikate tamaa.
 
Tatizo lenu mlikuwa mnapambana na Mkoloni "kidini" zaidi na hata unapoibua hoja hii ni kwa mtizamo ule ule! Mada kama hizi za kibaguzi huwa hazifiki mbali! Ni vizuri ukazipeleka Msikitini zaidi utaeleweka!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Buchanan,
Nimeandika kitabu kizima kinaitwa: ''The Life and Times of Abdulwahid
Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against
British Colonialism in Tanganyika,''
Minerva Press, London 1998.

Kitabu hiki kimefika mbali na mimi kimenifikisha kwenye ngazi sikutegemea kufika
hata katika njozi zangu.

Kitabu kimefanyiwa tafasiri ya Kiswahili 2002 na kipo katika toleo la tatu na cha
Kiingereza kipo toleo la pili.

Kitabu kimefanyiwa ''review'' na mabingwa wa African History, Ulaya na Marekani
kama John Iliffe, James Brennan na Jonathon Glassman ''review'' zimechapwa
katika Cambridge Journal of African History.

Kitabu kimesababisha mimi kuingizwa katika miradi miwili ya Oxford University Press
na Harvard na nimeshiriki katika uandishi wa Dictionary of African Biography (DAB).

Kitabu kimesababisha mimi kualikwa kuzungumza Chuo Kikuu Cha Iowa na Northwestern
University, Evanston Chicago.

Yako mengi.
Si kweli kama kitabu hakijafika mbali.
 
hongera kaka, mungu akujalie afya njema, wenyewe hawataki tujue wanahofu tutawadharau kwani wapiganaji ni wengine.Elimu yako ni faida kwa nchi hii, usikate tamaa.
Nnangale,
Ahsante ndugu yangu.
 
Ok

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sidhani historia hii ilifichwa. Enzi hizo hatukuwa na waandishi na wanahistoria mahiri kama Sheikh Mohamed
Jasusi,
Historia hii haikuwapendeza baadhi ya watu ndani ya uongozi wa juu wa TANU kwa sababu ilipoanza kutafitiwa ili iandikwe wao wenyewe wakaihujumu.

Hili nimelieleza katika kurasa za mwanzo kabisa katika kitabu cha Abdul Sykes.

Isitoshe nilipoanza kuandika historia hii kwa njia za makala katika gazeti la Africa Events (London) mwaka wa 1998 kuna toleo zima lilikusanywa lisisomwe na pakatokea pia ubishani baina yangu na Dr. Mayanja Kiwanuka kuhusu historia hii ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Dr. Kiwanuka alikuwa Mkurugenzi wa Uhamasishaji Umma Makao Makuu ya CCM Dodoma.

Upo ushahidi mwingi tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee Mohamed kulikuwa na umuhimu wa kusema Patwa ni muislam na dhehebu gani? Maana hapo kwenye uasia umeiweka kuonyesha kuwa alikuwa muasia tofauti na wengine kitabia Je kuutaja uislam ulitaka kutuonyesha nn?

Even as a politician, Nyerere practiced his Christian faith openly in concrete ways. First, he was a very devoted member of the Roman Catholic Church. When at home he went to early Morning Prayer everyday from 6.00 to 7.00 a.m. at St. Joseph's congregation, Dar es Salaam.

Nimekitowa kipande hicho katika maandishi ya mwandishi Angolwisye Isakwisa Malambugi, unaweza kutuaminisha wasifu huo wa Nyerere ambae anasifika kuwa alikuwa "si mdini", ulikuwa na maana gani?
 
ingependeza sana watoto wetu wafundishwe haya mambo shuleni wakue wakiifahamu historia ya nchi yao.
 
Even as a politician, Nyerere practiced his Christian faith openly in concrete ways. First, he was a very devoted member of the Roman Catholic Church. When at home he went to early Morning Prayer everyday from 6.00 to 7.00 a.m. at St. Joseph's congregation, Dar es Salaam.

Nimekitowa kipande hicho katika maandishi ya mwandishi Angolwisye Isakwisa Malambugi, unaweza kutuaminisha wasifu huo wa Nyerere ambae anasifika kuwa alikuwa "si mdini", ulikuwa na maana gani?
Ungemuuliza alieandika angekujibu Mimi nimemuuliza aliendika hapa ktk jukwaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Buchanan,
Nimeandika kitabu kizima kinaitwa: ''The Life and Times of Abdulwahid
Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against
British Colonialism in Tanganyika,''
Minerva Press, London 1998.

Kitabu hiki kimefika mbali na mimi kimenifikisha kwenye ngazi sikutegemea kufika
hata katika njozi zangu.

Kitabu kimefanyiwa tafasiri ya Kiswahili 2002 na kipo katika toleo la tatu na cha
Kiingereza kipo toleo la pili.

Kitabu kimefanyiwa ''review'' na mabingwa wa African History, Ulaya na Marekani
kama John Iliffe, James Brennan na Jonathon Glassman ''review'' zimechapwa
katika Cambridge Journal of African History.

Kitabu kimesababisha mimi kuingizwa katika miradi miwili ya Oxford University Press
na Harvard na nimeshiriki katika uandishi wa Dictionary of African Biography (DAB).

Kitabu kimesababisha mimi kualikwa kuzungumza Chuo Kikuu Cha Iowa na Northwestern
University, Evanston Chicago.

Yako mengi.
Si kweli kama kitabu hakijafika mbali.

Watu wengine wanasoma au wanasikiliza bila kujua kuna kitu kinaitwa critical thinking

Kuna hoja mbili kuhusu hili

1.Mohamed ameondoa ushiriki wa watu makusuadi katika historia anayosema ni ya Tanganyika, ingawa mambo yakibana husema ya wazee wake na ikiwa ngumu zaidi husema ya Waislam

Kosa ambalo Kivukoni walifanya kwa kutotambua michango mingine, kwake lina uhalali

2. Historia ina formula, kuieleza au kuiandika kwa mujibu wa matukio na wakati kama ilivyo
Jaribio la ku ''interject'' personal feelings or ideas, historia husota madole ya machoni dhahir shahir

Kwa waliosikiliza video, Mohamed anasema Kleist Sykes aliunda AA na kisha Jamii fil Islamiya 1933. Mohamed hakueleza chochote kuhusu Cecil Matola.

Kumtaja Cecil ni kumtaja Rais wa kwanza na hivyo hoja ya Kleist kuunda AA inakufa.
Katika maandishia anasema, Kleist aliunda kwasababu alikuwa na pesa na mashuhuri.

Mohamed haelezi Cecil Matola alikuwa msomi na 'immunity' dhidi ya Wakoloni kuliko Kleist
Tendo la kutomtaja Matola, historia haikukaa kimya imemnyooshea kidole

3. Mohamed anasema Abdul Aliunda TANU, Nyerere akiwa Rais wa TAA kabla ya 1954.

Kitendo cha kumuondoa Nyerere, historia inamzaba kibao Mohamed.
Huwezi kuwa Rais wa chama asiyejua transformation. Abdul hakuunda TANU, alishiriki

1929 cecil akiunda AA hadi uchaguzi katika miaka ya 1950 Abdul ni takribani miaka 23.
Kleist na Mwanawe Abdul walibaki na uana harakati kwa miaka 23.

Nyerere aliandika katiba ya TANU katika transformation ya chama kuwa ya kisiasa
Akafungua milango UN kwa kutumia usomi, na kupata Uhuru katika miaka 10

Mohamed hasemi hilo, lakini historia inamsuata bila mtu kuandika kitabu kingine

Miaka 23 Kleist na mwanae Abdul Sykes hawakuwa na wazo la kuandika katiba
Wazo amekuja nalo Nyerere. Ndio maana Mohamed hajibu hoja za nani aliandika katiba
Hataki kumsikia Nyerere mtu anayemchukia sana katika dunia hii

Mohamed anasema hotuba ya Nyerere UN iliandikwa na kamati ya watu watano.
Katika hao Mohamed hamtaji Nyerere aki back date kuandikwa kwake.

Historia inamshataki Mohamed, kama hotuba iliandikwa kabla ya Nyerere ni nani aliyetarajiwa kwenda UN?

Historia inasema kama kamati iliandika hotuba, kulikuwa na tatizo gani ikiwa lilikuwa suala la chama?
Kuna shida gani chama kuandika hotuba kubwa kama ya UN na kumkabidhi mhusika!

Mohamed anaingiza hoja kuonyesha Nyerere alisoma tu bila kujua maudhui ili kumdhalilisha.

Historia inamtetea Nyerere. Wakati hotuba inaandikwa yeye ni mmoja wa watu wachache sana waliokuwa na degree katika kiwango cha Master. Alishakuwa exposed katik siasa za dunia

Mohamed anaweza kumdhalilisha Nyerere atakavyo, wanaosoma kwa critical thinking watakuwa na rafiki yao mmoja anayeitwa Historia atakayewasaidia kuchambua chuki na ukweli
 
Jasusi,
Historia hii haikuwapendeza baadhi ya watu ndani ya uongozi wa juu wa TANU kwa sababu ilipoanza kutafitiwa ili iandikwe wao wenyewe wakaihujumu.

Hili nimelieleza katika kurasa za mwanzo kabisa katika kitabu cha Abdul Sykes.

Isitoshe nilipoanza kuandika historia hii kwa njia za makala katika gazeti la Africa Events (London) mwaka wa 1998 kuna toleo zima lilikusanywa lisisomwe na pakatokea pia ubishani baina yangu na Dr. Mayanja Kiwanuka kuhusu historia hii ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Dr. Kiwanuka alikuwa Mkurugenzi wa Uhamasishaji Umma Makao Makuu ya CCM Dodoma.

Upo ushahidi mwingi tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huu msiba huko ulikoenda hawakuona au umejitia upofu wewe mfia dini.

Watu wengine wanasoma au wanasikiliza bila kujua kuna kitu kinaitwa critical thinking

Kuna hoja mbili kuhusu hili

1.Mohamed ameondoa ushiriki wa watu makusuadi katika historia anayosema ni ya Tanganyika, ingawa mambo yakibana husema ya wazee wake na ikiwa ngumu zaidi husema ya Waislam

Kosa ambalo Kivukoni walifanya kwa kutotambua michango mingine, kwake lina uhalali

2. Historia ina formula, kuieleza au kuiandika kwa mujibu wa matukio na wakati kama ilivyo
Jaribio la ku ''interject'' personal feelings or ideas, historia husota madole ya machoni dhahir shahir

Kwa waliosikiliza video, Mohamed anasema Kleist Sykes aliunda AA na kisha Jamii fil Islamiya 1933. Mohamed hakueleza chochote kuhusu Cecil Matola.

Kumtaja Cecil ni kumtaja Rais wa kwanza na hivyo hoja ya Kleist kuunda AA inakufa.
Katika maandishia anasema, Kleist aliunda kwasababu alikuwa na pesa na mashuhuri.

Mohamed haelezi Cecil Matola alikuwa msomi na 'immunity' dhidi ya Wakoloni kuliko Kleist
Tendo la kutomtaja Matola, historia haikukaa kimya imemnyooshea kidole

3. Mohamed anasema Abdul Aliunda TANU, Nyerere akiwa Rais wa TAA kabla ya 1954.

Kitendo cha kumuondoa Nyerere, historia inamzaba kibao Mohamed.
Huwezi kuwa Rais wa chama asiyejua transformation. Abdul hakuunda TANU, alishiriki

1929 cecil akiunda AA hadi uchaguzi katika miaka ya 1950 Abdul ni takribani miaka 23.
Kleist na Mwanawe Abdul walibaki na uana harakati kwa miaka 23.

Nyerere aliandika katiba ya TANU katika transformation ya chama kuwa ya kisiasa
Akafungua milango UN kwa kutumia usomi, na kupata Uhuru katika miaka 10

Mohamed hasemi hilo, lakini historia inamsuata bila mtu kuandika kitabu kingine

Miaka 23 Kleist na mwanae Abdul Sykes hawakuwa na wazo la kuandika katiba
Wazo amekuja nalo Nyerere. Ndio maana Mohamed hajibu hoja za nani aliandika katiba
Hataki kumsikia Nyerere mtu anayemchukia sana katika dunia hii

Mohamed anasema hotuba ya Nyerere UN iliandikwa na kamati ya watu watano.
Katika hao Mohamed hamtaji Nyerere aki back date kuandikwa kwake.

Historia inamshataki Mohamed, kama hotuba iliandikwa kabla ya Nyerere ni nani aliyetarajiwa kwenda UN?

Historia inasema kama kamati iliandika hotuba, kulikuwa na tatizo gani ikiwa lilikuwa suala la chama?
Kuna shida gani chama kuandika hotuba kubwa kama ya UN na kumkabidhi mhusika!

Mohamed anaingiza hoja kuonyesha Nyerere alisoma tu bila kujua maudhui ili kumdhalilisha.

Historia inamtetea Nyerere. Wakati hotuba inaandikwa yeye ni mmoja wa watu wachache sana waliokuwa na degree katika kiwango cha Master. Alishakuwa exposed katik siasa za dunia

Mohamed anaweza kumdhalilisha Nyerere atakavyo, wanaosoma kwa critical thinking watakuwa na rafiki yao mmoja anayeitwa Historia atakayewasaidia kuchambua chuki na ukweli
 
Samahani ndugu, mbona vitabu vya hivi hatuwezagi kuvikuta bookshops zaidi ya kukuta vya nyambari?? Nielekeze pa kukipata ikibidi niambiwe na gharama za kukifikisha Bukoba make ndo nyumbani
 
Buchanan,
Nimeandika kitabu kizima kinaitwa: ''The Life and Times of Abdulwahid
Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against
British Colonialism in Tanganyika,''
Minerva Press, London 1998.

Kitabu hiki kimefika mbali na mimi kimenifikisha kwenye ngazi sikutegemea kufika
hata katika njozi zangu.

Kitabu kimefanyiwa tafasiri ya Kiswahili 2002 na kipo katika toleo la tatu na cha
Kiingereza kipo toleo la pili.

Kitabu kimefanyiwa ''review'' na mabingwa wa African History, Ulaya na Marekani
kama John Iliffe, James Brennan na Jonathon Glassman ''review'' zimechapwa
katika Cambridge Journal of African History.

Kitabu kimesababisha mimi kuingizwa katika miradi miwili ya Oxford University Press
na Harvard na nimeshiriki katika uandishi wa Dictionary of African Biography (DAB).

Kitabu kimesababisha mimi kualikwa kuzungumza Chuo Kikuu Cha Iowa na Northwestern
University, Evanston Chicago.

Yako mengi.
Si kweli kama kitabu hakijafika mbali.
Kitabu hiki nakipataje make ukienda bookshops vitabu vya hivi havipatikani!! Naomba kujua nakipataje hadi kunifikia nilipo bukoba, means naomba kujua gharama zote
 
Back
Top Bottom