Mwabhleja
JF-Expert Member
- Jan 27, 2016
- 1,351
- 2,061
Asalaam!
Rejea mada tajwa hapo juu. Kuna suala moja nimejihoji kwa muda mrefu lakini sijapata jawabu kutokana na visa vikuu viwili nilivyovishuhudia mwenyewe.
Mwaka 2013 mkoani Mbeya, Baba yetu mkubwa aliugua sana. Alizungushwa hospital nyingi sana pasipo mafanikio.
Mara ya mwisho ilikuwa MNH ambapo alishauriwa kurudi nyumbani ili walau ndugu wahangaike na tiba ya upande wa pili.
Mzee yule alikuwa akisema natamani kufa lakini kabla sijafa nataka kumuona mwanangu wa mwisho Asubhisye ambaye alikuwa Tanga. Ilibidi aitwe na aliporudi nyumbani Asubhisye aliongea nae na Mzee akachangamka kweli. Cha ajabu kesho yake alifariki.
Kisa cha pili nilikishuhudia kwa baba mwenye nyumba enzi nafanya kazi Geita mwishoni Mwa mwaka 2013. Mzee yule aliitwa Kachila alikuwa Muha wa Kasulu huko. Aliugua sana na matibabu yalishindikana.
Alikuwa kila Mara akisema naombeni muende Ukerewe mkaongee na Mke wangu amlete mtoto nimuone. Miaka mitatu nyuma alitengana na mkewe ambaye alikuwa mjamzito na tangu aondoke hakuwahi kurudi hata baada ya kujifungua.
Baada ya matakwa yake kutekelezwa naye alifariki baada ya siku moja.
Sasa najiuliza...je kuna mahusiano gani kati ya kukata roho na kumuona MTU unayemhitaji?
Kwa visa tajwa hapo juu, je nawe umewahi shuhudia au ni coincidence tu niliyokutana nayo?
Karibuni tueleweshane na kubadilishana uzoefu katika hili!
Sent using Jamii Forums mobile app