Inakuwaje mtu anagoma kufa mpaka amuone mtu anayemhitaji kumuona?

Inakuwaje mtu anagoma kufa mpaka amuone mtu anayemhitaji kumuona?

Mwabhleja

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2016
Posts
1,351
Reaction score
2,061
Asalaam!
Rejea mada tajwa hapo juu. Kuna suala moja nimejihoji kwa muda mrefu lakini sijapata jawabu kutokana na visa vikuu viwili nilivyovishuhudia mwenyewe.

Mwaka 2013 mkoani Mbeya, Baba yetu mkubwa aliugua sana. Alizungushwa hospital nyingi sana pasipo mafanikio.
Mara ya mwisho ilikuwa MNH ambapo alishauriwa kurudi nyumbani ili walau ndugu wahangaike na tiba ya upande wa pili.
Mzee yule alikuwa akisema natamani kufa lakini kabla sijafa nataka kumuona mwanangu wa mwisho Asubhisye ambaye alikuwa Tanga. Ilibidi aitwe na aliporudi nyumbani Asubhisye aliongea nae na Mzee akachangamka kweli. Cha ajabu kesho yake alifariki.

Kisa cha pili nilikishuhudia kwa baba mwenye nyumba enzi nafanya kazi Geita mwishoni Mwa mwaka 2013. Mzee yule aliitwa Kachila alikuwa Muha wa Kasulu huko. Aliugua sana na matibabu yalishindikana.

Alikuwa kila Mara akisema naombeni muende Ukerewe mkaongee na Mke wangu amlete mtoto nimuone. Miaka mitatu nyuma alitengana na mkewe ambaye alikuwa mjamzito na tangu aondoke hakuwahi kurudi hata baada ya kujifungua.

Baada ya matakwa yake kutekelezwa naye alifariki baada ya siku moja.
Sasa najiuliza...je kuna mahusiano gani kati ya kukata roho na kumuona MTU unayemhitaji?

Kwa visa tajwa hapo juu, je nawe umewahi shuhudia au ni coincidence tu niliyokutana nayo?

Karibuni tueleweshane na kubadilishana uzoefu katika hili!



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi mwenyew nimeshudia sana hilo jambo likitokea mahala fulan.......nadhan kuna mihadi inayowekwa baina ya kiumbe mtoa roho na binadam husika kiroho.........!!! Kitu anachohtaji kutimiza mtu ambaye tayar anaiona roho yake ipo ktk njia ya umauti....pindi tu atamkapo kwamba nataka kitu fln bs hutamka kwa nia kubwa sana yenye nguvu za kiroho ndani yake ambazo hakiwahi kuwa nazo kabla......ndipo hilo jambo hugeuka AHADI NZITO ambayo inanguvu za kiroho ndani na mara nyingi huwa hawafi mpka zitimie........akifa kabla zijatimia...bs ni shiddah kwa wew ulieharibu mipango yake
 
Mkuu unataka kutuaminisha kuwa kama hao walioaga wasingetimiziwa matakwa yao wasingefariki hadi leo????
Hii huwa inatokea katika jamii zetu.
Ni kwamba anayetarajia kufa huwa anamwomba mtu ili amwone na azungumze naye ndipo afe.
Kwahiyo anawaagiza watu wakamlete.

Wale watu wakirudi na kusema huyo mtu hawezi kuja katika kipindi husika basi huyo mzee anakufa na wala hasubiri hadi leo kama unavyosema.

Mgonjwa anapoomba kukutana na mtu ili ampe urithi au baraka au neno la mwisho anaangalia hali yake kiroho na anajua kuwa hana mda mrefu atafariki.

Ndipo sasa hutumia huo mda uliobaki kuomba kuonana na mtu wake anayetaka amuage na akikosekana katika kipindi alichokitaja basi huridhika na hufa.

Ukisoma hata vitabu vya dini utaona akina Isaka, Yakobo, Nuhu, Rutu, Eliya nk. Walikuwa wanawaita watoto wao, wanawabariki wanawarithisha ndipo wanafariki.

Mara nyingi hasa ukiwa mtu mwema unajua mda wa kifo chako hivyo unajiandaa vizuri kutubu na kuaga wapendwa wako.

Unajua kabisa unapo karibia kufa mwili hawa katika hali ambayo haijawahi kukutokea na unapiga kengele ya kifo kama unavyoisikia kengele ya njaa, kiu, haja, homa nk.

Haya mambo yapo.
 
Ni kweli swala hili huwa linatokea na mara nyingine watu hawa huwa wanakufa kabla ya walioagiza waitwe hawajafika!
Binafsi nadhani huwa wanataka kuagana nao tu na ndio maana ikitokea mtu huyo hajafika mapema basi huwa wanakufa bila kuonana na waliohitaji kuwaona
 
mungu haicheleweshi nafsi muda wa kufa unapofika
 
Mkuu unataka kutuaminisha kuwa kama hao walioaga wasingetimiziwa matakwa yao wasingefariki hadi leo????
Hapana Mkuu, sikuwa na maana hiyo. Kwa misingi ya African Tradition Religion inasadikika kuwa asipokuja MTU anayehitajika mhusika hufariki lakini atakuwa akimtokea MTU aliyekuwa akimhitaji endapo hakwenda kwa makusudi.
Hali hiyo itaisha baada ya tambiko katika kaburi LA marehemu. Jambo hili si LA dhahiri sana lakini lipo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulimwengu wa kiroho umefichika sana ni vigumu wanadamu wenye macho ya nyama kufahamu kitu.
Ila inawezekana malaika huongea na mhusika kabla ya kukata roho katika ulimwengu wa roho achague mtu ambaye angependa kuagana naye.
Ni mtazamo tu ila hakuna mwenye kujua sana
 
Kuna stage of death,binadam hana tofaut na myama ie kujitenga,,kutoona vizur,,kukosa ham ya kula,,but during the last stage of death controlled by emotion,,, yaan in that stage mtu anaweza kuamua kufa au asife,,kwa mfano mtu mwingine akihudumiwa vizur na akaridhika during this stage she,he may survive for several hour or day,kumbuka stage hii inatokea kama kuna natural death but not accident or attack

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna stage of death,binadam hana tofaut na myama ie kujitenga,,kutoona vizur,,kukosa ham ya kula,,but during the last stage of death controlled by emotion,,, yaan in that stage mtu anaweza kuamua kufa au asife,,kwa mfano mtu mwingine akihudumiwa vizur na akaridhika during this stage she,he may survive for several hour or day,kumbuka stage hii inatokea kama kuna natural death but not accident or attack

Sent using Jamii Forums mobile app
Exactly, vifo vinavyotokea kwa ajali havihusiani na hili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi kweli muda wa sir GOD kukuchukua ukifika kuna kugoma acha hizo
 
Back
Top Bottom