Inakuwaje mtu anagoma kufa mpaka amuone mtu anayemhitaji kumuona?

In short hao wote walikua wame sell their souls to the devil.
Wanachofanya ni kuacha maagizo na Mikoba iendelee kwa kizazi kijacho walichokikabidhi kama kanuni inavyowataka kwenye ukoo na mila za matambiko.
Na Roho zao wanazikabidhi baada muda mfupi waliokaa hapa duniani wakitumikia.
Na kinachowatokea sio natural death/God's plan.

Reason:- Hakuna mwanadamu mwenye uwezo WA kuamua afaje.
Cc mshana jr

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kisa hiki changu nadhani utashi tu wa mtu ndio humfanya awe na hofu kubwa ya maisha hata kuhisi kifo kinamkabili.

Baba yangu mdogo baada ya kuugua sana kwa kipindi cha muda mfupi, alipoteza kabisa hata nguvu ya kugeuka kitandani. Siku moja akiwa na mdogo wake pale hospital, alimuagiza aje aniite kwani Ana maongezi na mimi.

Nilifika pembeni ta kitanda chake kisha akanishika mkono na kuniachia maneno ya wosia. Alipomaliza, alinitajia namba yake ya siri ya ATM ya NMB akaniomba nikamtajie mama mdogo ila kadi ya CRDB nibaki nayo. Aliongea kwa sauti ya upole na msisitizo hata kidume nikadondosha machozi.

Baada ya mimi kuondoka eneo la hospitali, hali ya mzee ikabadilika na kuwa mbaya, akapewa referral kwenda MNH, baada ya mwezi mmoja, alipona kabisa na yupo hai mpaka leo.
Ilikuwa 2012 lakini siku ile naikumbuka mpaka leo kama vile ni tukio la jana.
So sio kila mtu akihitaji kuonana na mtu basi HUFA baada ya kumuona.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwa hawagomi kufa... maana ukijua mtu kagoma kufa mpaka amwone flan nanyi hamtaki huyo mtu afe basi mna mwambia tu jamaa alisafiri kwenda uk ndo anadunduliza nauli aweze kurudi uje umwage so vuta vuta subira msubiri aje... au unamwambia naye jamaa hali yake ni mbaya hatukukwambia subiria apone then aje akuone.
 
Kumbuka hata yule nabii Mzee wa kwenye biblia aliyeambiwa na Roho mt. Kwamba hatakufa mpaka atakapomwona masihi ( yesu) na baada ya yesu kuzaliwa yule Mzee alipomwona, alisema hivi " sasa Bwana waweza kumchukuwa mtumishi wako apumzike kwa amani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio hvyo tu mkuu, wengne kabla ya umauti huwa wanaomba wapikiwe aina flan ya chakula, au hata huomba maji ya kunywa....haya mambo kina mshana jr wanaeza kufafanua zaid, wamebobea ktk hz fani ngoja tumuite aje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…