Inakuwaje Mwanafunzi wa Form Six kusoma Diploma sawa na Form Four failure?

Tcha anakwambia diploma ni form four failure...nimesoma diploma nina division 1 ya 15 form 4 tena one ya mwaka 2012 shule ya kata sio hizi one za mchongo za miaka hii.
Sasa kumbe unajua kwamba diploma is much better kwann unasema advance ni shortcut? Kama ulisoma pale DIT miaka mitatu je degree ulisoma miaka mingapi?
 
Wacha wapambane wakati kwenye vijiwe sasa hivi mishahara midogo sana, na hiyo MD
Waache watakuwa disappointed baada ya kumaliza, Vijiweni huku MD wanalilia shift na CO na

ujira wenyewe mdogo sasa mtu unatoka familia masikini unataka wazazi wauze
rasilimali zao ili usome private baada ya miaka 6 unakaa bench kwa miaka
5 ukisubiri ajira ya serikali kituo cha afya huko Nanjilinjili, Tandahimba, Namtumbo
au Kazuramimba ina make sense na tena ni mpaka ufaulu interview.

Huyo akasome Program za miaka 3 au 4 ambazo anaweza kujiajiri kama sio za Health Science
asome computer science, IT, Software Engineering nakadhalika.
 
elimu ya F5/6 ni takataka, ingefutwa
imeleta dumb graduates waliojazana mtaani

mwambie dogo aachane na F4 failure wa dip, aende Hubert Kairuki
Una ada ya kumpa Kariuki MD milioni 7 bado mambo mengine
unapotoa ushauri zingatia mambo mengi. Asome Program nyingine
 
Kakosa MD, lakini hawezi kupata kwa vyuo vya serikali, labda huko hubert kairuki, st joseph ambayo ada ni million 7 kwa Mwaka.
Ada kwa mwaka milioni 7 plus, kila siku akitumia 10k, kwa mwakani milioni 3 laki 6 na nusu, hapo mengi hujaweza, matumizi mengine inazidi milioni 10 kwa mwaka

Miaka mi5, imetumika milioni 50+
 
Ada kwa mwaka milioni 7 plus, kila siku akitumia 1k, kwa mwakani milioni 3 laki 6 na nusu, hapo mengi hujaweza, matumizi mengine inazidi milioni 10 kwa mwaka

Miaka mi5, imetumika milioni 50+
Unasubiri uje uajiriwe baada ya miaka 5 tangu ugraduate like serious
 
kaangalia kigezo kisa D 4 wakati hata hiyo MD ni D3 tu, shida inakuja kwenye upinzani
True , kuna vyuo vinawafadhili wanafunzi waliochagua diploma moja kwa moja na unakuta wana ufaulu mkubwa kabisa kwa mfano chuo cha ufundi arusha ni moja ya chuo kizuri na kina wa sponsor wanafunzi wote waliochagua kujiunga nacho badala ya kwenda advance nadhani kigezo ni division 1 na 2 kama sikosei ATASOMA , ATAKULA , MALAZI, NA PESA YA IPT BURE KABISA
 
mfumo wetu wa elimu ni mbovu sana mno na kuufanya tuzeekee shuleni. mkuu kwa huo ufaulu wake kama pesa ipo akasome nje
 
Competition iliyopo ni kubwa sasa unakuta watu wana division 1 kali wote wameomba Bugando, Muhimbili, udsm n.k sasa atafanyeje maana mwenye ufaulu ndio anachukuliwa


Hapo kama mnaweza mlipieni vyuo binafsi ambako ada imechangamka, kusema amekosa chuo hapana sio kweli


Sema amekosa chuo cha serikali chenye bei nafuu, huko binafsi nafasi zipo tele zinawasubiri nyinyi tu


Sasa hapo amueni kusuka au kunyoa


Mjichange asome kwenye milioni 6+ atimize ndoto zake kama huko Kairuki ama Kampala etc.


Au aende education na fani zinginezo ale mkopo wake wa 3m per year ale nyama na anyamaze
 
Kwa kozi za engineering ukienda advance ni upuuzi maana mwenye diploma anasoma degree miaka mitatu na sio minne. Na atakuzidi pakubwa sana inapokuja ishu ya ajira.
Hata kwa baadhi ya course za afya. Mfano Physiotherapy na Nursing, ukiwa na diploma utasoma tu kwa miaka 3 tofauti na aliyetoka advance atasoma kwa miaka 4
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…