Kwasababu una uwezo wa kuongea haijalishi inabidi uongee, punguza maneno na ishi kivyakoWakuu, naomba nizungumze na wale wazee wa jiji ambao kazi yao kubwa mjini ni kubadilisha namba za umri kwenye vitambulisho, lakini maisha yao yamesimama kama sanamu ya Posta.
Hivi inakuwaje mwanaume mzima, una akili zako timamu, upo mjini miaka 15 hadi 20—eti unatafuta maisha.
Swali langu ni dogo sana, Hayo maisha mnayoyatafuta kwani yalijificha wapi kiasi kwamba miaka yote hiyo hamjayapata tu?
Mtu upo Dar au miji mikubwa hapa nchini tangu enzi za mtandao wa Celtel, lakini mpaka leo hii tunavyoongea, hata kiwanja cha miguu mitano kwa mitano huna! Kila mwaka unachofanya ni kuongeza namba ya umri tu kwenye cheti chako cha kuzaliwa, Kazi yako kubwa mjini ikifika mwezi wa kumi na mbili ni kulalamika mwaka umeenda kasi sana, Kasi gani wakati we umeganda.
Ukiangalia akaunti yako ya benki ni sifuri, ukiangalia mali uliyomiliki ni sifuri, zaidi ya maboksi ya feni na TV uliochukua kwa mkopo.
Ukweli mchungu, Mjini siyo mama yako mzazi kwamba atakuhurumia kwa sababu umekaa sana kwenye benchi lake. Kama miaka 20 imepita na bado unalipa kodi ya chumba kimoja ambacho mwenye nyumba akikohoa tu presha inapanda, jua umefeli, Ulichonacho siyo subira ya mafanikio, huo ni ulemavu wa fikra.
Ushauri wa Bure, Funganya Virago, Rudi Kijijini
Acheni kungangania dharau za kuitwa wa mjini wakati mifuko yenu imetoboka, Kuliko uendelee kuwa mzigo kwa ndugu na kujaza idadi ya watu kwenye daladala bila mpango
Funganya virago vyako.
Rudi kijijini kwenu.
Shika jembe, ukalime.
Kule kijijini ukisafisha heka mbili za mahindi au alizeti, unapata uhakika wa maisha na unaokoa heshima yako, Mjini pamekuwa shamba la bibi kwa sababu ya watu kama ninyi mnaoogopa jua la shambani lakini mnaweza kushinda vijiweni mkitathmini mechi za Ulaya kuanzia asubuhi hadi jioni.
Mwanaume ni vitendo na matokeo, siyo idadi ya miaka uliyofika mjini. Kama huna kiwanja, huna mbele wala nyuma, rudi kijijini ukajikwamue kiuchumi kabla uzee haujakukuta.
Nawasilisha kishujaa. Kama imekugusa, kachukue fomu ya kurudi kwenu.
Masikini wengi wanawaza Kama wewe, wenzio wanasoma wewe unawaza kuuza karanga ukanunue kiwanja mbande
Siku hizi kuna wahindi wananunua viwanja.Kuna Mhindi Ana kiwanja kivule au Chamazi?
Kama hana kivule wala chamazi anacho kwako indiaKuna Mhindi Ana kiwanja kivule au Chamazi?
umepiga kwenye mshono kabisa gentleman, halafu kisayansi zaidi.Wakuu, naomba nizungumze na wale wazee wa jiji ambao kazi yao kubwa mjini ni kubadilisha namba za umri kwenye vitambulisho, lakini maisha yao yamesimama kama sanamu ya Posta.
Hivi inakuwaje mwanaume mzima, una akili zako timamu, upo mjini miaka 15 hadi 20—eti unatafuta maisha.
Swali langu ni dogo sana, Hayo maisha mnayoyatafuta kwani yalijificha wapi kiasi kwamba miaka yote hiyo hamjayapata tu?
Mtu upo Dar au miji mikubwa hapa nchini tangu enzi za mtandao wa Celtel, lakini mpaka leo hii tunavyoongea, hata kiwanja cha miguu mitano kwa mitano huna! Kila mwaka unachofanya ni kuongeza namba ya umri tu kwenye cheti chako cha kuzaliwa, Kazi yako kubwa mjini ikifika mwezi wa kumi na mbili ni kulalamika mwaka umeenda kasi sana, Kasi gani wakati we umeganda.
Ukiangalia akaunti yako ya benki ni sifuri, ukiangalia mali uliyomiliki ni sifuri, zaidi ya maboksi ya feni na TV uliochukua kwa mkopo.
Ukweli mchungu, Mjini siyo mama yako mzazi kwamba atakuhurumia kwa sababu umekaa sana kwenye benchi lake. Kama miaka 20 imepita na bado unalipa kodi ya chumba kimoja ambacho mwenye nyumba akikohoa tu presha inapanda, jua umefeli, Ulichonacho siyo subira ya mafanikio, huo ni ulemavu wa fikra.
Ushauri wa Bure, Funganya Virago, Rudi Kijijini
Acheni kungangania dharau za kuitwa wa mjini wakati mifuko yenu imetoboka, Kuliko uendelee kuwa mzigo kwa ndugu na kujaza idadi ya watu kwenye daladala bila mpango
Funganya virago vyako.
Rudi kijijini kwenu.
Shika jembe, ukalime.
Kule kijijini ukisafisha heka mbili za mahindi au alizeti, unapata uhakika wa maisha na unaokoa heshima yako, Mjini pamekuwa shamba la bibi kwa sababu ya watu kama ninyi mnaoogopa jua la shambani lakini mnaweza kushinda vijiweni mkitathmini mechi za Ulaya kuanzia asubuhi hadi jioni.
Mwanaume ni vitendo na matokeo, siyo idadi ya miaka uliyofika mjini. Kama huna kiwanja, huna mbele wala nyuma, rudi kijijini ukajikwamue kiuchumi kabla uzee haujakukuta.
Nawasilisha kishujaa. Kama imekugusa, kachukue fomu ya kurudi kwenu.
Unanikataa au sio [emoji23]