Inakuwaje Mwanaume Una Miaka 20 Mjini, Hata Kiwanja cha Miguu 5 Huna? Rudi Kijijini Ukalime

Mimi naona hoja hii ina tatizo moja kubwa: inapima mafanikio kwa kipimo kimoja tu, yaani umiliki wa kiwanja.


Kitaalamu, maendeleo ya mtu hayawezi kupimwa kwa kumiliki kiwanja pekee. Wapo waliotumia miaka 20 kujenga taaluma, biashara, ujuzi, mitandao ya kikazi, elimu au uwekezaji ambao hauonekani kwa macho kama kiwanja.


Pili, kuna makosa ya kudhani kwamba kila aliyekaa mjini kwa muda mrefu na hana kiwanja ameshindwa maisha. Ukweli ni kwamba mazingira ya kiuchumi, majukumu ya kifamilia, magonjwa, ajira zisizo na uhakika, na changamoto nyingine huathiri uwezo wa mtu kujikusanyia mali.


Tatu, kurudi kijijini si suluhisho la kila mtu, kama ambavyo kubaki mjini si suluhisho la kila mtu. Wapo waliofanikiwa vijijini na wapo waliofanikiwa mijini. Kilicho muhimu ni tija ya kile unachokifanya, si eneo ulipo.


Zaidi ya yote, kuna tofauti kati ya mtu ambaye hajafanya jitihada zozote na mtu ambaye amekuwa akijitahidi lakini matokeo hayajafika kwa kiwango kinachotarajiwa. Kuwachanganya watu hao kwenye kundi moja si haki wala si uchambuzi wa kitaalamu.


Kwa mtazamo wangu, mwanaume hapimwi kwa kiwanja pekee, bali kwa uwezo wake wa kuwajibika, kuzalisha thamani, kuendelea kujifunza, na kuboresha maisha yake na ya wanaomtegemea. Kiwanja ni matokeo yanayowezekana, si kipimo pekee cha mafanikio.
 
Hizi fikra ndio zinazalisha mafisadi.

Kkila mtu akitaka kuwa na kiwanja NHC na TBA watampangisha nani?
Mnawapa watoto presha ooh umeanza kazi sasa jenga alafu ununue gari na kuoa, WTF!
Masiha si lazma kujenga, unaweza kukopa Nyumba iliyojengwa ukalipa kidogo kidogo, si laz,ma ujenge DAr , mikoa ipo mingi au hata kwenu USHETU.
 
Kujenga ni woga wa maisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…