Inakuwaje parachichi tunauziwa bei kubwa hivi?

Inakuwaje parachichi tunauziwa bei kubwa hivi?

kwanini iwe bei kubwa hivyo

Kanuni ni ile ile tuu, demand and supply.
Parachichi inatoka mbali, ina soko. Wakulima wena option nyingi, wengine wanawauzia wanouza nje kwenye maeneo kama Moshi, Njombe na Mbeya.
Kabla ya Parachichi za kisasa na kutanuka kwa soko la nje. Parachichi ilikuwa bei chee tuu.
 
Kabisa mkuu hili swala liundiwe agenda ya dharula pale Dom.

Wauza magenge wanatuibia sana hawa watu, bila kuwa na umoja kwenye hili tutaendelea kuumia tu.

Halafu ile hali ya kufokewa na muuzaji baada ya mnunuzi kulibinya binya ku test kama limeiva nayo imekuwa ni kero sana.

Treatment ya mteja wa parachichi imekuwa ni tofauti na wateja wa bidhaa zingine kabisa. Mambo haya huyakuti Mbeya.
 
Kuna haya maparachichi makubwa kama papai sijui yanalimwa wapi, wanauza 4,000. Sehemu nyingine wanajiongeza wanauza kwa vipande
 
Back
Top Bottom