Inakuwaje Rais wa Zanzibar kumuapisha kadhi? Kwani serikali inasimamia ibada?

Inakuwaje Rais wa Zanzibar kumuapisha kadhi? Kwani serikali inasimamia ibada?

Swali zuri. Mimi mwenyewe nasubiri jibu. Nimeshawahi kusikia tu “mahakama ya Kadhi”, ambapo masuala yanaamumuliwa kwa kutumia taratibu na sheria za kiislam.
Uko kama mimi mkuu ndomaana nilipoona hapo kadhi nimeogopa
Maana sheria zao si maskhara kwenye izo mahakama.
 
Nimeona kwenye taarifa ya habari Rais wa Zanzibar anamuapisha kadhi mkuu wa Zanzibar kwani serikali inasimamia ibada za watu!?
Zanzibar ni sehemu ya Tanzania yenye utawala wake wa ndani, asilimia 98 ya Wazanzibari ni Waislamu hivyo wanatumia sharia law, Kadhi Mkuu analipwa na serikali. Hata wakati wa ukoloni mpaka tunapata uhuru, makadhi walikuwepo na wanalipwa na serikali, hata mimi nimeshauri turuhusu mahakama za kadhi huku bara, ila tusiwalipe ma kadhi.

- Mwarobaini wa Kweli wa Mahakama ya Kadhi ni Huu, Wakristo, Waislamu, Kuukubali Bila Matatizo!.

- BAKWATA Ina matatizo ya Uendeshaji. Je, itaziweza Mahakama za Kadhi?!

P
 
Mimi kero yangu ni kwa nini kodi wazolipa watu wa imani zote zitumike kumlipa kadhi ili akawaamue watu wa dini Moja!?
 
Zanzibar ni sehemu ya Tanzania yenye utawala wake wa ndani, asilimia 98 ya Wazanzibari ni Waislamu hivyo wanatumia sharia law, Kadhi Mkuu analipwa na serikali. Hata wakati wa ukoloni mpaka tunapata uhuru, makadhi walikuwepo na wanalipwa na serikali, hata mimi nimeshauri turuhusu mahakama za kadhi huku bara, ila tusiwalipe ma kadhi.

- Mwarobaini wa Kweli wa Mahakama ya Kadhi ni Huu, Wakristo, Waislamu, Kuukubali Bila Matatizo!.

- BAKWATA Ina matatizo ya Uendeshaji. Je, itaziweza Mahakama za Kadhi?!

P
Ni kwa nini asilipwe kwa sadaka na michango mbalimbali ya waumini wenyewe
 
Sio kuapishwa tu na ulinzi anapewa na serikali.na analipwa na serikali haya unasemaje?
 
Nimeona kwenye taarifa ya habari Rais wa Zanzibar anamuapisha kadhi mkuu wa Zanzibar kwani serikali inasimamia ibada za watu!?
Zanzibar wana Kadhi Court katika mfumo wao wa Mahalama. Haileti shida kwa sababu asilimia 99 ni waislamu. Islam pia ni a way of life, na ina sheria zake. Na lengo la sheria ni ku-regulate maisha ya binadamu
 
Ni kwa nini kodi za serikali zitumike kuendesha dini!?
 
Kama sio la kidini kwa nini ndoa nyingi hufungiwa/hufungishwa nyumba za ibada?
kwani shule ni za kidini au za serikali? mbona kuna seminari na zile za Muslim, ndoa ni wewe unaamua nani akuapishe, mchungaji, Shekhe au uende bomani
 
Zanzibar ni nchi tuachene Wazanzibar tunaanza kurejesha mamlaka zetu kidogo kidogo Hadi Wadanganyika wakistuka....Done Deal.
 
Watanganyika( sorry ) watanzania bara,,,,, fanyeni yenu,,,🤐
 
Siasa katika mfumo wa Uislamu ni sehemu muhimu ya maisha ya kijamii na kidini. Uislamu hauitazami siasa kama taasisi tofauti na dini, bali ni sehemu ya mfumo mpana wa maisha unaoongozwa na sheria za Mwenyezi Mungu (Sharia). Katika mfumo wa Uislamu, siasa inalenga ustawi wa jamii kwa kuimarisha haki, usawa, na uadilifu, sambamba na kuwahimiza watu kumtii Mwenyezi Mungu.

Hapa kuna vipengele muhimu vya siasa katika mfumo wa Uislamu:

1. Uongozi na Khilafa

Uongozi katika Uislamu unachukuliwa kuwa amana (jukumu la dhamana) kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Kiongozi wa Kiislamu (Khalifa au Imam) anawajibika kutekeleza sheria za Mwenyezi Mungu na kuhakikisha ustawi wa jamii.

Khilafa ni mfumo wa uongozi wa Kiislamu uliolenga kuendeleza mafundisho ya Qur'an na Sunnah. Khalifa wa kwanza alikuwa Abu Bakr (R.A), aliyechaguliwa baada ya kifo cha Mtume Muhammad (S.A.W).

2. Sheria (Sharia) kama Msingi wa Siasa

Sheria za Kiislamu (Sharia) ndizo zinazotumika kama mwongozo wa kuendesha masuala ya kisiasa na kijamii. Sharia inahusisha haki za watu, uwajibikaji wa viongozi, na mipaka ya mamlaka.

Sheria hizi zinajumuisha mambo ya kijamii, kiuchumi, na kisiasa, na zinalenga kuleta haki na usawa katika jamii.

3. Mashauriano (Shura)

Shura ni kanuni ya Kiislamu inayohimiza maamuzi kufanywa kupitia mashauriano ya pamoja. Kanuni hii inasisitizwa katika Qur'an:

"...Na amri zao ni za kushauriana baina yao..."
— (Surat Ash-Shura, 42:38)

Hii inamaanisha kwamba viongozi wanapaswa kuwasiliana na watu wao kabla ya kufanya maamuzi makubwa.

4. Haki na Usawa

Mfumo wa Kiislamu wa kisiasa unalenga kuhakikisha haki na usawa kwa watu wote bila kujali dini, kabila, au hadhi ya kijamii. Qur'an inasema:

"Hakika Mwenyezi Mungu anakuamrisheni mrejeshe amana kwa wenyewe; na mnapohukumu baina ya watu mhukumu kwa uadilifu..."
— (Surat An-Nisa, 4:58)

5. Uhuru wa Kuabudu

Mfumo wa Kiislamu wa siasa unaheshimu uhuru wa dini kwa watu wa imani tofauti. Watu wa Ahlul Kitab (Wakristo na Wayahudi) walihifadhiwa haki zao chini ya uongozi wa Kiislamu, kulingana na dhana ya Dhima (uhakikisho wa ulinzi).

6. Kuzingatia Maadili

Viongozi wa Kiislamu wanapaswa kuwa watu waadilifu, wacha Mungu, na wa kuaminika. Mtume Muhammad (S.A.W) alisema:

"Kiongozi ni mchungaji, na atawajibika kwa wale anaowasimamia."
— (Bukhari na Muslim)

7. Kupinga Ufisadi na Udhalimu

Mfumo wa Uislamu unasisitiza kupinga ufisadi, ukandamizaji, na dhuluma katika jamii. Viongozi wanawajibika kusimamia mali za umma kwa uaminifu na kuhakikisha usambazaji sawa wa rasilimali.

8. Misingi ya Amani

Siasa za Kiislamu zinahimiza amani na kuzuia vita, isipokuwa pale ambapo haki inatakiwa kulindwa. Qur'an inasema:

"...Lakini mkikubali amani, basi ipokeeni..."
— (Surat Al-Anfal, 8:61)

Kwa ujumla, siasa katika mfumo wa Uislamu inalenga kuleta haki, maendeleo, na amani kwa watu wote kwa kufuata mwongozo wa Qur'an na Sunnah. Mfumo huu unatazama siasa si kama njia ya kutafuta mamlaka pekee, bali kama jukumu la kuwahudumia watu kwa uadilifu na kumtii Mwenyezi Mungu.
 
Zanzibar ni sehemu ya Tanzania yenye utawala wake wa ndani, asilimia 98 ya Wazanzibari ni Waislamu hivyo wanatumia sharia law, Kadhi Mkuu analipwa na serikali. Hata wakati wa ukoloni mpaka tunapata uhuru, makadhi walikuwepo na wanalipwa na serikali, hata mimi nimeshauri turuhusu mahakama za kadhi huku bara, ila tusiwalipe ma kadhi.

- Mwarobaini wa Kweli wa Mahakama ya Kadhi ni Huu, Wakristo, Waislamu, Kuukubali Bila Matatizo!.

- BAKWATA Ina matatizo ya Uendeshaji. Je, itaziweza Mahakama za Kadhi?!

P
Uwingi wa watu fulani nchini hauwanyimi walio wachache kulindwa na kupata haki zao zote kama wananchi wote wanavyozipata.
Kulipwa mshahara hakuna uhusiano na kutambulika kisheria, unaweza ukalipwa kama posho kwa kuisaidia serikali kwenye jambo fulani, inawezekana wale maliwali walikuwa wanalipwa posho kwa kuisaidia serikali kwenye ulinzi wa nchi.
 
Hapo kongolo linahusikaje
Unakurupuka tuu kama umeoga upako sasa kadhi na kusimamia ibada wapi na wapi?
Kadhi anafanya kazi chini ya SMZ,usije kuuliza Sheha ni nani pia?
Mana'ke mnashindwa kumuhoji Papa huko kufungusha ndoa za mashoga unakuja kuhoji mambo uliyoyakuta
 
Kwani kadhi jukumu lake nini kama si kuhukumu kwa mujibu wa sheria za kiisilamu alafu ajenda ya shoga unaileta hapa inahusikaje
 
Back
Top Bottom