Kwa lugha nyepesi kabisa Kadhi ni hakimu kwa mujibu wa sheria za kiislamu,yeye anajua hukumu stahiki kwa makosa mbali mbali kwa mujibu wa muongozo wa dini ya kiislamu
Watu wanahoji je itakuwaje alipwe na serikali? Kwani mahakimu wengine hawalipwi na serikali?
Litakuja swali sasa yeye si anahukumu waislamu? Kwani hao waislamu sio wananchi wa nchi hii,inamaana wangehukumukiwa na hakimu wa kawaida wasingekuwa waislamu?
Haki ambayo ingetolewa na hakimu wa kawaida na hata kwa kadhi ingetolewa haki hiyo ila kwa mujibu wa kiislamu,kwahiyo ishu ni kutafuta ufumbuzi wa shida za watu period
Kuhusu kwanini anaajiriwa na serikali ili kumpa kadhi nguvu kimamlaka,kwa maana hata mtu akiitwa mahakamani basi anatii sheria kana kwamba ameitwa na hizi mahakama za kawaida
Kikubwa mjue pale kazi haswalishi wala kutoa mawaidha wala hafundishi uislamu kwamba mumtolee macho,yupo pale kufanya kazi za hukumu kama mahakimu wengine period,je kuna mwenye shida na hilo?