Salama JF?
Kutokana na jinsi Mambo yanavyoenda nchini siku hizi siangalii wala kusikiliza taarifa za habari za ndani.
Nimewapa jukumu watoto wangu kuangalia taarifa ya habari ili baadaye waniambie wamepata habari gani. Mimi nimebaki kuingia JF, Instagram,Twitter na kwingine ambako napata habari za ukweli, umbeya, majungu, tetesi na uchambuzi. Jukumu langu ni kutumia akili yangu na kaelimu kangu kadogo kuzichuja!
Jana watoto walipoona habari ya Wachina kukamatwa na magunia ya Sarafu za Tanzania walilazimika kuniita nishuhudie mubashara!
Kwa wale ambao hawakubahatika kuona ni kuwa Wachina wachezesha kamari walikamatwa na sarafu za Tsh.200 na 500 zenye thamani ya Sh.Milioni 200.
Nimejiuliza lengo la hao ndugu wa Nyerere nini au ni kukwepa kodi? Swali gumu zaidi, inakuwaje kwa Mji mdogo kama Morogoro sarafu za Milioni 200 zitolewe kwenye mzunguko mamlaka husika zisigundue hadi wakusanye viroba vya fedha kiasi kile!?
Kwa akili yangu, inakataa na kuuita huu ni uzembe uliovuka mipaka! Hata Kama sio Mtaalamu wa fedha au mchumi lakini mhhhh!