Inakuwaje sarafu za milioni 200 zinafichwa mamlaka zisishtuke mapema?

Inakuwaje sarafu za milioni 200 zinafichwa mamlaka zisishtuke mapema?

Mkuu tatizo hapo sio kukusanya izo coins. Tatizo ni kuwa wanakwepa kodi hawa jamaa. Unakuta mtu amechukua kibali cha kuchezesha kmali cha mashine 100 tu. Kumbe amesambaza mashine 200. Na ukiwa na mashine nyingi ni lazima uwe na coins nying za kusambaza.

Kitu kingine kunakiwango maalumu cha pesa mtu anatakiwa awe nacho kama cash. Kikizidi ni makosa.

Sasa uyo mchina kosa linaweza kuwa ni kuwa na kiwango kikubwa cha pesa in cash.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe una endeshwa na hisia tu na sio uhalisia!!!! Mtu anapoenda kukata leseni pale bodi ya michezo ya kubahatisha lazima atabainisha ni mashine ngapi atakazo miliki, ili wajue, na kuweza kumtoza tozo la leseni, vile vile kule TRA, kwenye kukadiria kodi lazima ijulikane ana mashine ngapi,.

Kama akizidisha ni uzembe wa wafuatiliaji. Kuhusu kiwango cha pesa kuwanacho mkononi kuwa kosa, hizo pesa ni mtaji wa hizo mashine, sasa kama mashine moja tu mtaji wake ni laki 2,sasa mkoa mzima labda wana mashine 500,unategemea nini?

Na hapo hapo kuna siku ya makusanyo ya pesa walizopata kutoka kwenye mashine hizo, na kulingana na nature ya biashara hiyo ni lazima tu wawe na coins muda wowote kwani wakati wowote mashine inaliwa pesa wanapigiwa simu waende wakaongeze mtaji, HAPO, cha msingi ni serikali kupiga marufuku hizo mashine kutumia coins za nchi, badala yake watumie TOKEN., ndio suruhisho lake!!
 
Kuna mbwiga hata humu wamo wanaamini hiyo ndo "risk taking" ambayo ni muhimu kwenye biashara yaani kuweka pesa ambayo ni mtaji wako ndani.

Hata kwao binafsi ni hatari mno kukaa na hiyo pesa ndani sababu ya uporaji na majanga kama ilivyomtokea Marehemu Mzee Shinyanga huko Mwanza.
 
Sasa umesha sema wamekamatwa na mpaka waneoneshwa kwenye vyombo vya habari Ila unaamua uanzishe Uzi na kusema ni uzembe why watanzania?
 
Hayo ma mashine yanapiga hela jaman Kuna siku nilisikia mchina anatoa hela Yan dude lilipiga kelele Ela zinatoka Kama dakika 15nikasena dah [emoji1787][emoji1787][emoji1787] wachina wanapiga Ela yote hayo sababu ya technology Yao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wachina naona wanataka kugeuza hapa ni kwao mana wanafanya vitu vingi kinyume na sheria na taratibu.
 
Mkuu, una elimu gani, tuanzie hapa kwanza..

1. Unafaham madhara ya kiuchumi kwa baadhi ya watu ku hold pesa bila kuziingiza kwenye mzunguko!??

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu elimu yangu mie ni chekechea.

Ofcoz madhara yapo wazi. Lkn kuna kitu haujanielewa. Em nikuulize swali, HIO BIASHARA YA WACHINA NA MASHINE ZAO ZA BONANZA WATAIENDESHA VIPI BILA KUWA NA COINS???

Ndio maana nasema wanachofanya ni sawa kutokana na nature ya biashara yao lkn si sawa kisheria. Na kama si sawa kisheria basi walowapa leseni ya hio biashara hawakufatilia kiundani kujua hio biashara inaendeshwaje.

Wangefatilia wakajua inahusisha kuhold kiasi hicho cha sarafu basi aidha wangewaambia warekebishe au wasingepewa kabisa leseni. So kosa limeanzia kwenye mamlaka zinazotoa leseni.
 
Kuna sehemu tumekosea. TISS wanatakiwa kuongeza nguvu kwenye maeneo kama haya. Wachina ni tatizo sana.
Waongeze nguvu huko alafu waache chadema ijitawale..
Kuna haja ya kuifumua taasisi yote pia polisi
 
Hao wachina hawana kosa, tena hiyo kesi watashinda mapema sana,

Kama kosa ni kuwa na fedha ndani millioni 200+,kuna watu wanahifadhi billions, baada ya mauzo au huduma then wanapereka benki!

basi inabidi kila mtu anayeenda kudepost pesa benki akamatwe na ashitakiwe kwamba kwanini amehifsdhi pesa zote hizo!

Hivi kweli ukienda casino kama palm beach au legrande casino, watu wanaocheza kamari, zile hela huwa zinakimbilia benki instantly! Au huwa zinakusanywa ndio zinaperekwa?
Mwmposa alikuwa anasafirisha sadaka,sarafu kibao, je akikamatwa muda huo utasema amehifadhi pesa ndani?

Kwanza hatujaambiwa hizo sarafu wanazo kwa muda gani,
Hao jamaa wanachezesha kamari, wanalipa kodi, wanakusanya hizo pesa then zinaenda benki, sasa hatujaambiwa hizo pesa wamekaa nazo kwa siku ngapi, huwa wanapereka benki baada ya muda gani!

Kama wachina walioiba samaki wetu, tukataifisha samaki na boti, lakini mwisho wakashinda kesi na tukawalipa fidia, hata hili litakwisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hayo ma mashine yanapiga hela jaman Kuna siku nilisikia mchina anatoa hela Yan dude lilipiga kelele Ela zinatoka Kama dakika 15nikasena dah [emoji1787][emoji1787][emoji1787] wachina wanapiga Ela yote hayo sababu ya technology Yao

Sent using Jamii Forums mobile app
Wao kazi yao ni kuzunguka na Kluger kukusanya pesa vijiweni
 
tapatalk_1588448421047.jpeg
hii ni kama sh ngapi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mm sio mtaalam wa maswala ya sheria, ila ningeomba kujua kama kuna sheria inayombana mtu kuwa na kiwango fulani cha pesa ndani ya nyumba zaidi ya hapo anapaswa kupeleka bank

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mm sio mtaalam wa maswala ya sheria, ila ningeomba kujua kama kuna sheria inayombana mtu kuwa na kiwango fulani cha pesa ndani ya nyumba zaidi ya hapo anapaswa kupeleka bank

Sent using Jamii Forums mobile app
Faru John weka avatar ya Faru bana huyo Nyau niachie mimi.....ni kosa kuweka fedha nyumbani fedha zimetengenezwa zizunguke wewe uan miliki thamni ya fedha kulingana na ujira wako!
 
Kwa wale ambao hawakubahatika kuona ni kuwa Wachina wachezesha kamari walikamatwa na sarafu za Tsh.200 na 500 zenye thamani ya Sh.Milioni 200.

Nimejiuliza lengo la hao ndugu wa Nyerere nini au ni kukwepa kodi?
Ndio. ni rahisi sana kukwepa kodi kama tu una untraceable transactions
 
wali gumu zaidi, inakuwaje kwa Mji mdogo kama Morogoro sarafu za Milioni 200 zitolewe kwenye mzunguko mamlaka husika zisigundue hadi wakusanye viroba vya fedha kiasi kile!?
Sishangai sana kuhusu kushindwa ku-detect hiyo financial crime. We still have a long way to go katika financial crime anticipation na mitigation. Ni lazima tuiimarishe FIU na hata idara ya upelelezi ya jeshi la polisi
 
Biashara hii inawalipa haswa na hizo 200 naona ni kama chenji tu za kurudisha kwenye mashine na kufanya zizungushe na kazi ziende
Hapo kuna hela nyingi sana na ukwepaji wa kodi ni kama kumsukuma mlevi

Wachina wamekuwa sumu kwa kwa mataifa mengi na wanahonga haswa
Angalia tena taarifa hii
Adjustments.jpg



Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Salama JF?

Kutokana na jinsi Mambo yanavyoenda nchini siku hizi siangalii wala kusikiliza taarifa za habari za ndani.

Nimewapa jukumu watoto wangu kuangalia taarifa ya habari ili baadaye waniambie wamepata habari gani. Mimi nimebaki kuingia JF, Instagram,Twitter na kwingine ambako napata habari za ukweli, umbeya, majungu, tetesi na uchambuzi. Jukumu langu ni kutumia akili yangu na kaelimu kangu kadogo kuzichuja!

Jana watoto walipoona habari ya Wachina kukamatwa na magunia ya Sarafu za Tanzania walilazimika kuniita nishuhudie mubashara!

Kwa wale ambao hawakubahatika kuona ni kuwa Wachina wachezesha kamari walikamatwa na sarafu za Tsh.200 na 500 zenye thamani ya Sh.Milioni 200.

Nimejiuliza lengo la hao ndugu wa Nyerere nini au ni kukwepa kodi? Swali gumu zaidi, inakuwaje kwa Mji mdogo kama Morogoro sarafu za Milioni 200 zitolewe kwenye mzunguko mamlaka husika zisigundue hadi wakusanye viroba vya fedha kiasi kile!?

Kwa akili yangu, inakataa na kuuita huu ni uzembe uliovuka mipaka! Hata Kama sio Mtaalamu wa fedha au mchumi lakini mhhhh!
Wale ndio wenye mashine ya kucheza kamari kuna mashine ya 500 naya 200 hivo zile flooti zao ndio hizo wanahifadhi endapo mashine mtu akala nyingi wana wanachukua sarafu kwa ajili ya kuzihifadhi ili chenji isiwasumbue
 
Back
Top Bottom