Samcezar
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 13,095
- 22,731
Ndio maana ya neno BAHATI NASIBU. NASIBU ni neno linalomaanisha kitu cha kinachofanania na ukweli ila si cha kweli.Hayo mamichezo yafutwe yanaharibu sana watoto, na hii bodi ya michezo ya kubahatisha imelala inatoa tu leseni kiholela.
Jamani zile mashine ni programmed, programmer anaweza weka conditions katika watu kumi wanaocheza washinde wanne kwa interval fulani sasa hiyo utaita ni bahati nasibu.
Bodi kabla haijatoa leseni ya hayo madude ilitakiwa ichukue hata madude 10 wakae nayo wiki nzima waone ila hata isingesaidia sana maana mwiaho wa siku yanabadilishwa setting kirahisi, wito wangu hayo mamashine yafutwe kabisa hawa wachina wanatuchuna ngozi bila ganzi.
Wanaingiza pesa nyingi kwa kazi zisizoeleweka.
Hayo madude wameyasambaza hadi maeneo ya vijijini kukamua maskini, ni kama kuku wao wa mayai wamewasambaza mwisho wa siku wanaend kuokota mayai.
Bodi ya michezo ya kubahatisha haya madude tuondoleeni tafadhali watoto wanaiba pesa wanapeleka huko.
Mwisho.
Mfano unaposema bahati nasibu unamaanisha kuwa ni bahati ambayo si ya ukweli kiuhalisia......
Sent using Jamii Forums mobile app