Inakuwaje sarafu za milioni 200 zinafichwa mamlaka zisishtuke mapema?

Na ukiwa China mtu mgeni (Foreigners) hata raia si ruhusa kuchezesha kamari ni serikali tu.

huku Kwetu lazima kuna viongozi wana neemeka. Hizi kamali zipo sana vijijini watu walikolala.

shamba la bibi
Wewe kinakushangaza nini upo Tanzania na kuna baadhi ya vitu vinalipiwa kwa dollar mfano majumba ya kupanga haya mahekalu hawalipishi shilingi kitu ambacho huwezi kutana nacho Ulaya ,Asia nk ndio maajabu yanayopatikana Tz

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa unauliza kwa nn mamlaka husika zisigundue na wakati tayari wameshakamatwa[emoji854]
 
Milioni 200 kwa ile biashara Ni hell ndogo mno, hakunaga mtu anaweza kuficha sarafu za milioni 200, kwanza hata ubebaji wake ni shida

Itakuwa hizo sarafu zilikuwa katika process ya kutawanywa kwenye zile mashine, ile biashara inafanyika kwa sarafu, sio noti kwa hiyo mtaji lazima uwe katika sarafu
 
Ndio maana Bora Kama vipi, hizo mashine zizuiwe tu, lakini justification ya kukamata zile sarafu kwangu bado inazua maswali tu
 
Mkuu tatizo hapo sio kukusanya izo coins. Tatizo ni kuwa wanakwepa kodi hawa jamaa. Unakuta mtu amechukua kibali cha kuchezesha kmali cha mashine 100 tu. Kumbe amesambaza mashine 200. Na ukiwa na mashine nyingi ni lazima uwe na coins nying za kusambaza.

Kitu kingine kunakiwango maalumu cha pesa mtu anatakiwa awe nacho kama cash. Kikizidi ni makosa.

Sasa uyo mchina kosa linaweza kuwa ni kuwa na kiwango kikubwa cha pesa in cash.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Masikini ndio wanazidi kunyonywa yani,kwa kupenda pesa za kitonga.
 
Inatia huruma sana. Yaan waTZ ndo tumefanywa shamba. Siku nikipata hilo limashine lazima nilifanyie reverse engineering aisee. Washatuona wadhaifu sana
Mkuu jaribu kusaidia katika hilo la kulichanganya mashine lile.Nipo kijijini lakini ukiona jinsi watu wanavyoliwa pesa unaweza kushangaa. Naomba tuwasiliane ikiwezekana tumfilisi huyu mchina maana hujichumia pesa bila hata kutia jasho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo siouhakali,kwa Nini wazifungie ndani ...Sarafu M200!
Sarafu 200 zenye thamani ya milioni 200, kwa maana idadi ya sarafu ilikuwa milioni moja. Wamepata wapi chenji zote hizo
 
Ukicheza kamari unaruhusiwa kuweka ndani Sarafu zote hizo!Nielimishe!?
Hata kama sio mchezesha kamari,
Kwani hapa Tanzania kuna sheria inaweka ukomo wa kiasi cha fedha mtu anachotakiwa kuwa nacho nyumbani au ofisini?
 
Kwa hiyo kuwa na chenji Ni kosa kisheria? Mie ninazo huwa asubuhi nabeba shs Mia nane za kupandia daladala nisizinguane na konda, asubuhi shs mia nne jioni shs mia nne
 
Tatizo siouhakali,kwa Nini wazifungie ndani ...Sarafu M200!
What if waliokuwa na mpango wa kupeleka bank kubadirisha baada ya kufikia kiwango flani ambacho kampuni kimekipanga? Naongea hivi huku nikiangalia uhuru wa mfanyabiashara na mahusiano ya ulipaji kodi.
 
sarafu 200 zenye thamani ya milioni 200,kwa maana idadi ya sarafu ilikuwa milioni moja.wamepata wapi chenji zote hizo
Walikuwa wachezesha kamali zinazotumia coin za 200 na 500
 
Nadhani huo ni uonevu tu wa mamlaka.

Hao wachina wana mashone zao za kuchezesha kamari na wameruhusiwa na mamlaka.
Na wanalipa kodi.

Sasa Mamlaka ilipowaruhusu waweke makorokoro mitaani walijua kuwa yanaweka ili yagawe maziwa?
 
Well said.
Hio ni mitaji ya watu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…