Inamaanisha nini kufuatilia bunge la Kenya zaidi kuliko bunge letu tukufu?

Inamaanisha nini kufuatilia bunge la Kenya zaidi kuliko bunge letu tukufu?

Kuna Watanzania wengi sana wanafuatilia kwa makini bunge la Kenya huku wakipuuza kufuatilia hata kidogo mambo yanayoendelea kwenye bunge lao, huko sio kukosa uzalendo?

Pia Wakenya wenyewe hawafuatilii kabisa bunge letu, sijawahi kuona Mkenya ameposti mtandaoni kuhusu jambo lolote linaloendelea kwenye bunge letu. Sio kwamba tunajichoresha kufuatilia, kuzipa umuhimu na kufuatilia sana siasa za Kenya kama hii impeachment ya Gachagua?
Unataka kusemaje, malizia sentensi, haijafika mwisho. Eleweka mkuu.
 
Tz hakuna bunge bhana, lingekuwepo hata ile mada ya sukari tulitegemea nae Bashe aje ajibu, sio anatetewa na anakuwa huru.
Hoja ijibiwe kwa hoja ila badala yake akaenda watusha wananchi kuwa wakiendelea msikiliza mbunge wao hata serikari itasitisha huduma.
Hebu fikiria hili lingetokea kenya au nchi yoyote yenye watu wakijielewa wakiwa na bunge kweli kama muhimili wa serikali unazan nin kingetokea??
 
Bunge la Kenya lipo wazi (open) kwa umma na ni la kidemokrasia lenye pia kuleta bashasha na mvuto kwa wapiga kura na lenye wabunge mchanganyiko kutoka vyama tofauti vya siasa.

Bunge la Tanzania ni pale Spika atakaporuhusu "flow" na kila mtu amwage ugali na mboga hapohapo kwa kutoa mchango wake.

Pia wapiga kura wa Tanzania ndo wenye uwezo wa kulibadili bunge letu ikiwa wataruhusiwa kupiga kura kwa kutumia uwezo wa kufikiri kwamba mbunge wanomhitaji atakidhi matarajio yao na sio matarajio yake yeye.
Kwa hali ilivyo sasa ni ngumu mno wananchi kufukia maamuzi kama hayo hatuna tofauti sana na nchi za Korea, ukiambiwa hakuna kusherekea siku flani unatakiwa kutii amri tuu na hakuna kuhoji, ukiambiwa mtoto wa rais au wa mjomba ndiye atachukua wadhifa flan mwananchi hautakiwi kuuliza wewe nikutulia tu na kufanya kazi zako.
 
Kweli kabisa,nchi ya matamko,amri na walinda dola kutembeza vichapo kwa wasio na hatia.
 
Back
Top Bottom