Kuna Watanzania wengi sana wanafuatilia kwa makini bunge la Kenya huku wakipuuza kufuatilia hata kidogo mambo yanayoendelea kwenye bunge lao, huko sio kukosa uzalendo?
Pia Wakenya wenyewe hawafuatilii kabisa bunge letu, sijawahi kuona Mkenya ameposti mtandaoni kuhusu jambo lolote linaloendelea kwenye bunge letu. Sio kwamba tunajichoresha kufuatilia, kuzipa umuhimu na kufuatilia sana siasa za Kenya kama hii impeachment ya Gachagua?
WEWE ni umeleta HOJA YA KIJINGA kuja kupima upepo, wakati unajua ukweli.
Bunge la k
Kenya linajadili mambo mtambuka kwa maslahi mapana ya wakenya.
Bunge ma wabunge wake wamevuka level ya kutanguliza maslahi ya vyama vyao vya siasa, wanatanguliza maslahi ya Mama yao Kenya.
Wanapiga kura na kusign kumuondoa VICE PRESIDENT,bila kujali chama,wanatanguliza maslahi ya Kenya.
Huku TZ wabunge wa CCM watishiwa na kupewa maelekezo kwenye caucas party kutanguliza chama katika mambo ya KISHENZI.
Ccm inatoa rushwa kwa ajili ya kupitisha bajeti ya wizara flani yenye utata.
Wabunge wa Tanzania na akili zao wanakaa kitako kupitisha hoja ya kuuza Bandari benchmark ya nchi yetu.
Wanakwenda tour ya kuwa brain 🧠 wash uarabuni ili wapitishe hoja ya kuuza Bandari za BARA.
Kwahiyo mtu mwenye akili hawezi kukaa kuangalia Bunge la Tz,ni Bora kukaa kuangalia vibonzo, program za vichekesho kwenye TV kuliko kuangalia Bunge la Tanzania
Kulikuwa na wakati Bunge la Tz lilikuwa Bunge, wakati wa speaker Anne Makonda, Speaker Samwel sitta.
Bunge la Mwisho ni lile alilomaliza nalo kikwete na kuanza nalo Magufuli na kuzuiwa kuoneshwa laivu na TUMBOTUMBO Nape Mnauye.
Kukaa kuangalia bunge la Tz ni kujitoa ufahamu kwa mazingira ya sasa.
Bunge linaoogopa kujadili kwa uwazi wizi,WEZI wa Fedha za Serikali kupitia ripoti ya CAG.
Bunge linalzuia kujadili hoja za watu kutekwa na kuuwawa?? Nani awaangalie.
Kwa sasa bunge ni kama mkusanyiko wa WAHUNI,WAPIGA UPATU,WAAUZA NGADA,MADALALI WA KUUZA NCHI.
Yaani kwa sasa mijadala ya vijiwe vya kahawa unaweza kuambulia mambo ya maana kuliko Bungeni.
So acha Watu waangalie na kujifunza namna bora ya Bunge kufanya Kazi kwa weledi nchini Kenya.
Muwe na siku njema.