Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 376,316
- 871,876
Huu ni ushauri murua wa kiroho utakaokuzindua hisia
1. Kuwa mbinafsi na nguvu/nishati yako. Mimi
Ilinichukua miaka mingi kujifunza hili:
Acha kuwa entatain watu wanaokupa makombo tu.
Kilichokusudiwa kwa ajili yako hakitahitaji kutumia ili kije kwako, kwa hiyo ikiwa hakiendi vyema, usikilazimishe.
Na mipaka (boundaries) si kitu unachokiomba kwa upole. Ni kitu unachokisimamia na kukilazimisha kiheshimiwe.
2. Kamwe usibishane au kufanya majadiliano na hisia zako za ndani (intuition).
Ule msisimko wa kwanza, au lile bando/fundo linalojitengeneza tumboni mwako wakati mtu anaposogea karibu, ni roho yako inayokuonya kabla ya akili yako kuanza kutafuta visingizio.
Unajisihi kutokuwa na amani? Ondoka. Bila kutoa maelezo yoyote na bila kufikiria mara mbili.
3. Jifunze kujichagua mwenyewe kwanza.
Kung'ang'ania mtu hadi unajisahau wewe ni nani ndio uchawi kiini macho kibaya zaidi ambacho mtu anaweza kujifanyia kwenye maisha yake mwenyewe.
Hukuzaliwa ili ujifanye mdogo au ujishushe thamani mbele ya mtu mwingine.
4. Funga mlango kwa mahusiano yasiyoeleweka..
Usiku mmoja ukiwa peke yako na nafsi yako unapaswa kuwa na thamani kubwa zaidi kuliko saa moja ukiwa pembeni ya mtu asiyejali hisia zako au asiye na nia ya dhati nawe.
Mtu yeyote anayebaki juu mchangani (asiyetaka kuingia ndani zaidi kwenye mahusiano) hapati fursa ya kukufikia wewe, wala kupata nguvu/nishati yako.
5. Jua thamani ya amani yako.
Katika umri wangu, mimi hufanya hesabu hii haraka sana! ikiwa kitu kinakuondolea utulivu wako, tayari kimekugharimu kiasi kikubwa sana.
Kata kamba (vunja uhusiano huo) na ushike njia yako kabla hakijanyonya nguvu zako zote kabisa.