Mama nahisi ana ishu personal na Mbowe, kila akitajiwa kuhusu Mbowe huwa anapaniki sana na anajikuta anaropoka mambo yasiyo ya msingi.
Nadhani ni zaidi ya tunayoyajua kuhusu mama na uhusika wake kwa hii kesi ya Mbowe.
Kuhusu msamaha mwenyewe kwanza nimemshangaa yeye kusema anaweza kusamehe, sasa Mbowe bado hajahukumiwa yeye mam anawezaje kusamehe kama sio yeye ndio ameishikilia hii kesi??
Rais anaweza kusamehe mtu endapo atakutwa na hatia mahakamani, lakini mtu ambaye bado ni mtuhumiwa nadhani mtu mwenye mamlaka ya kuondoa kesi ni DPP, naelewa anapisema "anaweza kumsamehe" alimaanisha anaweza kumpa maelekezo DPP asiendelee na kesi waifunge Mahakamani which means Mbowe atakuwa Freeman kama jina lake Ila mama hakupaswa kutumia lugha za namna hiyo Kama kweli yeye Hana personal interest na hiyo kesi.
There is more into it tutakuja kujua ukweli tu.