Inasemekana Cloud media inataka kumshuka Diamond kimziki kwasababu alikataa ofa ya kuwa chini yao

Inasemekana Cloud media inataka kumshuka Diamond kimziki kwasababu alikataa ofa ya kuwa chini yao

bwana ugali

Member
Joined
Jan 13, 2015
Posts
25
Reaction score
7
Jamanii hii ni tetesi lakini nimeamua kuifanya utafiti na nimegundua nyimbo za Diamond zimepungua kupigwa kwenye kituo cha Television na radio cha Clouds baada ya msanii huyu kukataa mchongo wa Clouds kutaka ku manage msanii huyu wao.

Na mbadala wake wakaamua kumpandisha chati Ali Kiba ili Watanzania wapate mbadala. Fanya research na wewe uchangie.

Karibuni.
 
Nakataa maana babutale mkubwa fela ruge na kusaga ni mtu mmoja sio kweli kabisa kama dadamond anashuka ni muda tu umefika msitafute kisingizio mpanda ngazi hushuka eboo
 
Sidhani, Fela na Tale ni vivuli vya Ruge. Ingekuwa hivyo basi Cloudz wangekuwa na bifu na hao mameneja wake pia maana wao ndo wanahusika sana kufanya bargaining za show za msanii, na kama hawa mameneja wangekuwa na bifu na Cloudz tusingisikia wakizipromoti kwa sana nyimbo za wasanii wao kama Madee,Chege,Temba na Yamoto Band. So research yako sidhani kama ina ukweli, mi nachoona ni kwamba nyimbo mpya za Diamond kama Mdogomdogo,Bum bum na huu wa sasa Nitampata wapi ni za kawaida sana, kitu kinachozibeba ni Video na sio Audio. Hazijafikia level za Ukimwona, Mawazo, Moyo wangu, Number1,etc
 
Kajishusha mwenyewe maana wadau wa mziki wake wamechoka skendo zake...
 
Kila chenye mwanzo hakikosi mwisho. Walikuwepo akina Mr. Nice leo hii wako wapi? Hivyo sishangai Diamond kushuka, ni ishara ya wasanii wengine kurise
 
Naona nguvu zimeelekezwa kwenye yamoto
 
Nyimbo mpya ya ali.kiba ni kali hatari. Yani ukichukua yale mapambio yote ya diamond kuanzia mbagala, nataka kulewa, my number one na taka taka zake zoote haifikii hii ngoma, Ally kiba ni mkali
 
Alie pewa kapewa,wamshushe wampandishe ila binadamu lazima tukubali kua wambili havai moja,awe Dai au Kiba....
 
Back
Top Bottom