Niliandika kama mara 4 hivi kuhusu COVID-19 sasa wanaiita Delta Variant. Nikaandika kiufupi tu kuwa hatuishi kwenye dunia ya peke yetu, nikaendelea kuhusu ugonjwa huu kuingia nchini kutoka Uganda, hakuna aliyejali.
Sasa leo ITV wametangaza upungufu wa oxygen Bugando. Niliomba Serikali yetu tukufu ipige marufuku mikusanyiko yote mipirani, mikutanoni na hata kwenye mazishi, misiba, harusini, mikutano ya hadhara ya kisiasa na kidini n.k. Nikaandika hilo gonjwa la COVID-19 au Delta Variant linateketeza wenzetu Uganda, bado watu hawaamini.
Sasa hayawi hayawi yamekuwa. Nilishangaa sana na hata kupigiwa simu na marafiki zangu waliopo nje ya nchi wakishangaa sana kuona mechi ya Simba na Yanga kujaza watu wote wale elfu 55 sio maskhara. Narudia tena kutoa wito kwa wahusika kupiga marufuku mikusanyiko ya watu. Jamani jamani tunaishi dunia hiyo hiyo ya wenzetu tena waafrika wanaoathirika na kuteketea.
Tulete chanjo ya Pfizer kupitia mahospitali binafsi na ya serikali. Anayetaka achanje asiyetaka shauri lake ila tutashindwa hata kwenda sokoni na hizo jezi za Yanga na Simba zitageuka sanda.
EEH ALLAH TUNUSURU NA WANUSURU WAJA WAKO WOTE AFRIKA NA DUNIANI.SISI TUNAKIRI MBELE YAKO KUWA TUNAISHI KATIKA DUNIA HIYO HIYO WANAOISHI WENZETU ULIYOIUMBA WEWE MTUKUFU PEKEE. AMEEN.