#COVID19 Inasemekana kirusi cha COVID-19 aina ya Delta kimeingia Mwanza

#COVID19 Inasemekana kirusi cha COVID-19 aina ya Delta kimeingia Mwanza

Ila Tanzania masihara ni kubwa mno kuhusu Corona. Omba Tu Mungu isikupitie au kupitia wa karibu yako au ndugu ndiyo utajua machungu yake. Sitaki kukumbuka madhara ya hii Corona kwenye ukoo wetu na majirani kadhaa. Rest in Peace my people.
Umegonga penyewe. Mtanzania hatajua madhara ya kitu mpanga aone kimemtokea yeye, mtu wa familia au jirani. Hii ni aina ya ubongo wa panya hii.
 
Hakuna cha DELTA VARIANT wala .DELTA FORCE 3

Mtuache jamani nyie kama mnanufaika na corona hamieni huko ilipo mkapige pesa...
Inavyosemekana hili ni toleo la nne kati ya matoleo 24 yaani tunaenda na herufi za kigiriki sasa tulianza na Alpha tutamaliza na Omega.....ukinusurika hayo yote bila kuchanjwa basi wewe ni mwamba🤣👇🐒

images (83).jpeg
 
Aliyekwambia covid imetua mwanza leo nani? tangu wiki tatu zilizopita kuna cases za watu wanaopata mafua na kupoteza uwezo wa kuhisi harufu, labda kama wewe ndo umeona jambo geni...
Hata mii sikumbuki kama kuna kipindi dunia ilikuwa free from Covid tangu itue kwenye sayari hii 2019.

Ni kama ukimwi tu, tangu tuupokee miaka ya 80 mambo yanaenda tu. Ikikuotea ni shidaa. Ikikukosa mwendo mdundo.
 
Binafsi nimeshaliandaa BEGA LANGU.

Ninaisubiri chanjo kwa hamu kubwa mno. IJE TU TUDUNGWE then TUPAMBANE NA YATAKAYOJIRI.

#KaziIendelee
 
Kwamba kipo Mwanza hiyo ni assumption. Fact ni kwamba kipo Tanzania, Dar es Salaam, Tanga
 
Back
Top Bottom