#COVID19 Inasemekana kirusi cha COVID-19 aina ya Delta kimeingia Mwanza

#COVID19 Inasemekana kirusi cha COVID-19 aina ya Delta kimeingia Mwanza

Watu wangehamasishwa kutumia zile Tiba zetu za Asili, Allah alizipa barka zake zikasaidia sana mara zote

Safari hii naona kina Doroth Gwajima hawaja kampeni kabisa
Dorothy yupo Mubashara TBC anatuhimiza tuvae barakoa, kuosha mikono na kuepuka misongamano kama vile ndio kaigundua korona wiki iliyopita 🤣👇
20210706_215631.jpg
 
Vitoto vya chuo hivi, baba zao ndo wameanza kugonga 40 ndo maana vinawaona wazee.....
🤣🤣🤣

Labda hawatofika 40 ndio maana wanaona mbali....

Binafsi hata 60 naona karibu mno....nakimbizana niishi vyema miaka hiyo panapo uhai kwani it's so soon......

Time is not our best Ally!
 
"Kama kufa tutakufa tu " jpm
Kuna vifo vya:

1. Uzee (80 - )
2. Kusababishiwa (kuuwawa, magari nk)
3. Kijinga (kuzembea tahadhari za wazi)
4. Mapenzi ya Mungu (kina Nyerere wamo humu)

Hakuna anayepinga kufa. Lakini unakuta vipi?
 
Niliandika kama mara 4 hivi kuhusu COVID-19 sasa wanaiita Delta Variant. Nikaandika kiufupi tu kuwa hatuishi kwenye dunia ya peke yetu, nikaendelea kuhusu ugonjwa huu kuingia nchini kutoka Uganda, hakuna aliyejali.

Sasa leo ITV wametangaza upungufu wa oxygen Bugando. Niliomba Serikali yetu tukufu ipige marufuku mikusanyiko yote mipirani, mikutanoni na hata kwenye mazishi, misiba, harusini, mikutano ya hadhara ya kisiasa na kidini n.k. Nikaandika hilo gonjwa la COVID-19 au Delta Variant linateketeza wenzetu Uganda, bado watu hawaamini.

Sasa hayawi hayawi yamekuwa. Nilishangaa sana na hata kupigiwa simu na marafiki zangu waliopo nje ya nchi wakishangaa sana kuona mechi ya Simba na Yanga kujaza watu wote wale elfu 55 sio maskhara. Narudia tena kutoa wito kwa wahusika kupiga marufuku mikusanyiko ya watu. Jamani jamani tunaishi dunia hiyo hiyo ya wenzetu tena waafrika wanaoathirika na kuteketea.

Tulete chanjo ya Pfizer kupitia mahospitali binafsi na ya serikali. Anayetaka achanje asiyetaka shauri lake ila tutashindwa hata kwenda sokoni na hizo jezi za Yanga na Simba zitageuka sanda.

EEH ALLAH TUNUSURU NA WANUSURU WAJA WAKO WOTE AFRIKA NA DUNIANI.SISI TUNAKIRI MBELE YAKO KUWA TUNAISHI KATIKA DUNIA HIYO HIYO WANAOISHI WENZETU ULIYOIUMBA WEWE MTUKUFU PEKEE. AMEEN.
Wananchi wanatishwaaaa ila wamega kutishika...
Acha vije, tena vija na rafiki zao hivyo virusi
 
Tz siyo ug. Usitishe watu, hakuna huo ugonjwa hapa. Kachome kinga wewe akili ni nywele watu wanatofautiana kwa ujinga sorry kwa ufahamu!
 
Watanzania kuna wakati tuna hamasishwa tunawe kwa vitakasa mikono na tuepuke mikusanyiko,lakini linapo kuja suala la mbio za mwenge haohao tena wanatutangazia tujitokeze kwa wingi kwa mapokezi hivi wanatuonaje?

Sent from my SM-A307FN using JamiiForums mobile app
 
Wimbi la 1,2,3 yote yamepita nashukuru hatukuokota maiti barabarani au hospitali kuzidiwa wagonjwa, taharuki za corona huwa zina athari zake.
 
Oya mniamini

Hapa napofanyia kazi

Watu wanaondoka.


Jichunge, chunga familia yako.


Nyie wazee wazee wamiaka kuanzia 40+,na wenye UKIMWI, kisukari, magonjwa ya Moyo, Shinikizo la Damu,Magonjwa sugu ya mfumo wa upumuaji ... Mnaondoka chap chap.
Jinga kweli hili.

Kwanza huna maadili yoyote ya kuwa japo nesi wa zahanati.

Unaonekana muhuni muhuni tu wewe, na hao waliokuajiri watakuwa fyatu kama wewe.
 
Back
Top Bottom