#COVID19 Inasemekana kirusi cha COVID-19 aina ya Delta kimeingia Mwanza

#COVID19 Inasemekana kirusi cha COVID-19 aina ya Delta kimeingia Mwanza

Mkuu hi serekali haiko serious kabisa,nashangaa Jana mwenge mwanza umelala buhongwa watu nyomi na serekali inahamashishaa watu wajeee kwa wingi!
 
Kama yeye anadhan chanjo ndiyo itamlinda yuko sahihi,kama naww unadhan Maombi ndo yatakulinda upo sahihi,usibeze mawazo ya mwenzako,kila mtu ana maisha yake,

Na unataka watu wajikinge vip na hiyo Covid 19??
Ni hizo hizo zilizokwishatolewa za kunawa na maji tiririka, vitakasa mikono, kuvaa barakoa hasa kwenye mikusanyiko, kuzingatia lishe bora na mazoezi, kutengeneza nyungu na juisi za matunda ambavyo utakuwa unatumia mara kwa mara ku-boost kinga ya mwili.
 
Tumwombe sana Mungu atutangulie, hili tatizo halihitaji kubeza wala utani. Hali ni mbaya nikama hiI delta 3 imelenga Afrika zaidi.

Nianze kivi kwa dhati kabisa MUNGU BABA MUWEZA WA YOTE NAKUOMBA UTUNUSURU WATANZANIA, UTUNUSURU WAAFRIKA NA DUNIA KWA UJUMLA NA GONJWA HILI.
 
Aliyekwambia chanjo ya mabeberu ya Pfizer ndo itakulinda na kifo ni nani
Israel walipochanja zaidi ya 70%..... Delta variant imepata watu 500 hivi.... But 93% hawajapata serious infection sababu chanjo imesaidia. Bila chanjo ina maana wangekufa au kuwa mahututi.

Ni fact hii sio speculation kama zako
 
waisraeli ndo wapinzani namba moja wa hizo chanjo huwa nafuatilia habari zao, sema na wenyewe wanapelekwapelekwa na wanasiasa.....hiyo chanjo hakuna inachosaidia zaidi ya kuharibu mfumo asili wa kinga ya mapafu na kuingiza sumu mwilini.
 
Unafikiri serikali ikipiga marufuku mikusanyiko ndio mikusnyiko haita kuweko,kiufupi hapa mwanza ndio kwanza mikusanyiko imeanza
 
Chanjo situmii kwa kweli ntapambana na machungwa maana ndio yaliniokoa nilikuwa nakula machungwa kama chizi na unga wa ubuyu
Hukutengeneza nyungu yenye mchanganyiko wa tangawizi, vitunguu swaumu, kitunguu maji, pilipili na limau.......ungepiga hii cocktail unge revive mapema sana.
 
Ila Tanzania masihara ni kubwa mno kuhusu Corona. Omba Tu Mungu isikupitie au kupitia wa karibu yako au ndugu ndiyo utajua machungu yake. Sitaki kukumbuka madhara ya hii Corona kwenye ukoo wetu na majirani kadhaa. Rest in Peace my people.
Chukua tahadhari zote zinazoshauriwa na wataalam wa afya

Sent from my TECNO KE5 using JamiiForums mobile app
 
Niliandika kama mara 4 hivi kuhusu COVID-19 sasa wanaiita Delta Variant. Nikaandika kiufupi tu kuwa hatuishi kwenye dunia ya peke yetu, nikaendelea kuhusu ugonjwa huu kuingia nchini kutoka Uganda, hakuna aliyejali.

Sasa leo ITV wametangaza upungufu wa oxygen Bugando. Niliomba Serikali yetu tukufu ipige marufuku mikusanyiko yote mipirani, mikutanoni na hata kwenye mazishi, misiba, harusini, mikutano ya hadhara ya kisiasa na kidini n.k. Nikaandika hilo gonjwa la COVID-19 au Delta Variant linateketeza wenzetu Uganda, bado watu hawaamini.

Sasa hayawi hayawi yamekuwa. Nilishangaa sana na hata kupigiwa simu na marafiki zangu waliopo nje ya nchi wakishangaa sana kuona mechi ya Simba na Yanga kujaza watu wote wale elfu 55 sio maskhara. Narudia tena kutoa wito kwa wahusika kupiga marufuku mikusanyiko ya watu. Jamani jamani tunaishi dunia hiyo hiyo ya wenzetu tena waafrika wanaoathirika na kuteketea.

Tulete chanjo ya Pfizer kupitia mahospitali binafsi na ya serikali. Anayetaka achanje asiyetaka shauri lake ila tutashindwa hata kwenda sokoni na hizo jezi za Yanga na Simba zitageuka sanda.

EEH ALLAH TUNUSURU NA WANUSURU WAJA WAKO WOTE AFRIKA NA DUNIANI.SISI TUNAKIRI MBELE YAKO KUWA TUNAISHI KATIKA DUNIA HIYO HIYO WANAOISHI WENZETU ULIYOIUMBA WEWE MTUKUFU PEKEE. AMEEN.
Watakusikia? Sijui wa TZ tumelogwa na mlozi kafa? Watu na viongozi wetu hawajali. Kumkimbilia Mungu kwa uzembe wetu ni kumkufuru. Hatatusaidia.
 
Hukutengeneza nyungu yenye mchanganyiko wa tangawizi, vitunguu swaumu, kitunguu maji, pilipili na limau.......ungepiga hii cocktail unge revive mapema sana.
Hapana mkuu sjapiga nyungu
 
Kipi ni ushahidi wa kwamba huo upungufu wa mitungi ulikuwepo toka zamani?
Upungufu wa mitungi ni tatizo moja lakini mikusanyiko ya watu kwenye mipira, makongamano na kukimbiza mwenge ni tatizo jingine. Daktari mmoja wa Bugando ameugua baada ya kumtibu mkimbiza mwenge Mwanza.
 
Niliandika kama mara 4 hivi kuhusu COVID-19 sasa wanaiita Delta Variant. Nikaandika kiufupi tu kuwa hatuishi kwenye dunia ya peke yetu, nikaendelea kuhusu ugonjwa huu kuingia nchini kutoka Uganda, hakuna aliyejali.

Sasa leo ITV wametangaza upungufu wa oxygen Bugando. Niliomba Serikali yetu tukufu ipige marufuku mikusanyiko yote mipirani, mikutanoni na hata kwenye mazishi, misiba, harusini, mikutano ya hadhara ya kisiasa na kidini n.k. Nikaandika hilo gonjwa la COVID-19 au Delta Variant linateketeza wenzetu Uganda, bado watu hawaamini.

Sasa hayawi hayawi yamekuwa. Nilishangaa sana na hata kupigiwa simu na marafiki zangu waliopo nje ya nchi wakishangaa sana kuona mechi ya Simba na Yanga kujaza watu wote wale elfu 55 sio maskhara. Narudia tena kutoa wito kwa wahusika kupiga marufuku mikusanyiko ya watu. Jamani jamani tunaishi dunia hiyo hiyo ya wenzetu tena waafrika wanaoathirika na kuteketea.

Tulete chanjo ya Pfizer kupitia mahospitali binafsi na ya serikali. Anayetaka achanje asiyetaka shauri lake ila tutashindwa hata kwenda sokoni na hizo jezi za Yanga na Simba zitageuka sanda.

EEH ALLAH TUNUSURU NA WANUSURU WAJA WAKO WOTE AFRIKA NA DUNIANI.SISI TUNAKIRI MBELE YAKO KUWA TUNAISHI KATIKA DUNIA HIYO HIYO WANAOISHI WENZETU ULIYOIUMBA WEWE MTUKUFU PEKEE. AMEEN.
corona haipo
 
Kuleni vitunguu swaumu vinaboost immunity 🙏
 
Upungufu wa mitungi ni tatizo moja lakini mikusanyiko ya watu kwenye mipira, makongamano na kukimbiza mwenge ni tatizo jingine. Daktari mmoja wa Bugando ameugua baada ya kumtibu mkimbiza mwenge Mwanza.
Hivi huu mwenge bado upo!?
 
Ndugu zangu hivi 'kwa mfano wewe mwenye hospitali ungeanzia wapi kusema tuna upungufu wa mitungi wakati ule, maana ingemaanisha kuna wagonjwa wa corona, na hapo ndo shida ingekuangukia, manake serikali haikutaka kusikia story hizo za corona maana hata Rais alishatangaza ugonjwa huo haupo/ umetokomezwa ..... yaani ilikuwa kazi kweli ,na ndipo kwa kuficha wakaja na jina la ' tatizo la ugonjwa wa upumuaji' .......... hahahahaaaa
Tatizo la ugonjwa upumuaji lipo hadi sasa na ndio maana hata huko walikotangaza huo upungufu wa mitungi wamesema hiyo mitungi kwa ajili ya wenye matatizo ya kupumua na wagonjwa wa corona, tatizo sasa imekuwa kwamba tukisikia matatizo ya kupumua tunahitimisha kuwa ni corona tu ndio maana hata Rais Samia siku ile anaambiwa huku kwa wenye matatizo ya kupumua yeye anauliza kama ni covid.

Sasa hizi hoja za kwamba serikali haikutaka kusikia story corona ndio zimefanya kila tatizo la kupumua tuite ni corona kwamba waliamua kuita hivyo ili isijulikane kama ni corona, na sasa hili la upungufu wa mitungi pia tunasema lilikuwepo toka zamani ila walikuwa wanaogopa kutangaza, watu humu walikuwa wanaeleza kwamba Madaktari huko ndio wanajua uhalisia wa corona kwamba wameambiwa hivi mara vile na hao madaktari ila hatukusikia hilo la upungufu wa mitungi ya oksijeni.
 
Eti " Hayawi hayawi sasa yamekuwa" bob nini cha kufurahia hapo kwa kauli yako hii?
Hayawi hayawi, siyo neno la furaha!!! ndo mwalimu wako wa UPE alivo kufundisha??? mrudie tena umwambie arudishe mshahara alio kula
 
Upungufu wa mitungi ni tatizo moja lakini mikusanyiko ya watu kwenye mipira, makongamano na kukimbiza mwenge ni tatizo jingine. Daktari mmoja wa Bugando ameugua baada ya kumtibu mkimbiza mwenge Mwanza.
Ameugua nini?
 
Back
Top Bottom