#COVID19 Inasemekana kirusi cha COVID-19 aina ya Delta kimeingia Mwanza

#COVID19 Inasemekana kirusi cha COVID-19 aina ya Delta kimeingia Mwanza

Mnawatengenezea watu hofu,

Mtawapa pesa wakae ndani??

Au kwakua nyie mnampango wa kutumia Kodi zao Ili kununulia chanjo basi hamjali.
Ilanilazimu kupiga simu Kwa dactari hapo, Hii kitu ni upuuzi tu unsotengenezwa, na sasa tutahamushia mashambulizi kwa hao wanaotangaza hali zenye kuleta taharuki, Ili Mungu awalaani
 
Hatuwezi kumsujudu shetani haijalishi majina aliyokuja nayo. Mara COVID 19 mara DELTA VARIANT, n.k

Endeleen na ukaid wenu,jamaa yenu alisema hivyo hivyo kuwa tegemeo ni mungu,yuko wapi leo??

Kwani huko Vatican wanakodanja kila leo hawana Mungu??

Anyway,kufa wote tutakufa,mwenye masikio haambiwi sikia
 
Aliyekwambia covid imetua mwanza leo nani? tangu wiki tatu zilizopita kuna cases za watu wanaopata mafua na kupoteza uwezo wa kuhisi harufu, labda kama wewe ndo umeona jambo geni. Karibu mwezi mzima wizara imeshatoa tahadhari za watu kujikinga na covid, au unataka waje wakufunge pingu za miguu. Aliyekwambia chanjo ya mabeberu ya Pfizer ndo itakulinda na kifo ni nani........yaani ulivyokurupuka kuleta hii taarifa ni kana kwamba kuna jambo geni...

Kama yeye anadhan chanjo ndiyo itamlinda yuko sahihi,kama naww unadhan Maombi ndo yatakulinda upo sahihi,usibeze mawazo ya mwenzako,kila mtu ana maisha yake,

Na unataka watu wajikinge vip na hiyo Covid 19??
 
Almost 2 weeks ndio nikakaa poa
Vipi baada ya kurecover kichwa kilikaa sawa
Maana baadhi ya walioupata nilikuwa nikiwasikia wanalalamika kichwa hakija kaa sawa kuna muda wanahisi kama kizunguzungu na kuona maruweruwe lakin baada ya kupita miezi 3 ile hali ikaisha
 
Oya mniamini

Hapa napofanyia kazi

Watu wanaondoka.

Jichunge, chunga familia yako.

Wazee wa miaka kuanzia 40+ na wenye UKIMWI, kisukari, magonjwa ya Moyo, Shinikizo la Damu, Magonjwa sugu ya mfumo wa upumuaji mnaondoka chap chap.
Miaka 40 nimzee kumbe!
 
Hakuna cha DELTA VARIANT wala .DELTA FORCE 3

Mtuache jamani nyie kama mnanufaika na corona hamieni huko ilipo mkapige pesa.

1. Wimbi la kwanza China
2 . Wimbi la Pili South Africa
3 . Wimbi la tatu India
4. Wimbi la nne.........

TUACHENI JAMANI DAH !!
La nne Mwanza
 
Niliandika kama mara 4 hivi kuhusu COVID-19 sasa wanaiita Delta Variant. Nikaandika kiufupi tu kuwa hatuishi kwenye dunia ya peke yetu, nikaendelea kuhusu ugonjwa huu kuingia nchini kutoka Uganda, hakuna aliyejali.

Sasa leo ITV wametangaza upungufu wa oxygen Bugando. Niliomba Serikali yetu tukufu ipige marufuku mikusanyiko yote mipirani, mikutanoni na hata kwenye mazishi, misiba, harusini, mikutano ya hadhara ya kisiasa na kidini n.k. Nikaandika hilo gonjwa la COVID-19 au Delta Variant linateketeza wenzetu Uganda, bado watu hawaamini.

Sasa hayawi hayawi yamekuwa. Nilishangaa sana na hata kupigiwa simu na marafiki zangu waliopo nje ya nchi wakishangaa sana kuona mechi ya Simba na Yanga kujaza watu wote wale elfu 55 sio maskhara. Narudia tena kutoa wito kwa wahusika kupiga marufuku mikusanyiko ya watu. Jamani jamani tunaishi dunia hiyo hiyo ya wenzetu tena waafrika wanaoathirika na kuteketea.

Tulete chanjo ya Pfizer kupitia mahospitali binafsi na ya serikali. Anayetaka achanje asiyetaka shauri lake ila tutashindwa hata kwenda sokoni na hizo jezi za Yanga na Simba zitageuka sanda.

EEH ALLAH TUNUSURU NA WANUSURU WAJA WAKO WOTE AFRIKA NA DUNIANI.SISI TUNAKIRI MBELE YAKO KUWA TUNAISHI KATIKA DUNIA HIYO HIYO WANAOISHI WENZETU ULIYOIUMBA WEWE MTUKUFU PEKEE. AMEEN.
We bwege kweli. Nenda kajifungie peke yako.
 
Vipi baada ya kurecover kichwa kilikaa sawa
Maana baadhi ya walioupata nilikuwa nikiwasikia wanalalamika kichwa hakija kaa sawa kuna muda wanahisi kama kizunguzungu na kuona maruweruwe lakin baada ya kupita miezi 3 ile hali ikaisha
Mie kifua ndio kilinizingua ila kichwa freshi
 
Ndio maana nikauliza hilo swali ili nijue kwamba huo upungufu ni sasa tu au toka zamani ila ilikuwa haitangazwi? maana humu mitandaoni tulikuwa tunaambiana kuwa hali ya corona ni mbaya na madaktari wanaujua ukweli ila hatukusikia kuhusu upungufu wa mitungi ya oksijeni kwa kipindi chote.
Ndugu zangu hivi 'kwa mfano wewe mwenye hospitali ungeanzia wapi kusema tuna upungufu wa mitungi wakati ule, maana ingemaanisha kuna wagonjwa wa corona, na hapo ndo shida ingekuangukia, manake serikali haikutaka kusikia story hizo za corona maana hata Rais alishatangaza ugonjwa huo haupo/ umetokomezwa ..... yaani ilikuwa kazi kweli ,na ndipo kwa kuficha wakaja na jina la ' tatizo la ugonjwa wa upumuaji' .......... hahahahaaaa
 
Back
Top Bottom