#COVID19 Inasemekana kirusi cha COVID-19 aina ya Delta kimeingia Mwanza

#COVID19 Inasemekana kirusi cha COVID-19 aina ya Delta kimeingia Mwanza

Tukichanjwa ndio hatutakufa? Nonsense
 
NIKO JIJI LA MWANZA
najihusisha na uendeshaji wa bodaboda

nimeshindwa kuunganisha dot kama ni korona au ni ugonjwa wakawaida.J Mos ilopita nili endesha boda bila kujifunga kizuia baridi shingoni.hivyo j pili nikaamka na dalili za kikoozi.j3 kikawa kifua kikohoz na mafua ywliombatana na kuumwa pua.yani ukivuta hewa inakua kama hewa unayo ivuta baada ya kupigwa ngumi ya puaa.

Juz hali ikawa mbaya zaidi nikaamua kuchukua baisikel nikaendesha roote nyegez malimbe kwenda kurudi.lakini bado hali ikawa vilevile.

ikabidi ni dhani tena.nikadhani kua kwakua nimeacha mazoez ya gym kwa miez 2 labda ndo homa ya gym. juzi jioni niingie gym nikapiga tizi kwa masaa3 na maji lita 2 nikawa nishatumia.lakini usiku kifua kikapamba moto.ikabidi niokoke nisalii
mungu si asthuman nikapata haueni

nimeingia gym tena asubuh ya leo kilichobaki ni kikohozi kifua kwa mbali mafua kidogo ila bado pua inaumaa kinoma kama nimepigwa ngumi ya pua..

kAMA NA WW UME EXPIRIENCE KITU KAMA HICHO UNAWEZA KUSHARE
 
Ndugu yangu tumezika watu wawili ndani ya siku tisa tu (Bukoba). Mwanza, Bugando ukifika hali ni mbaya sana katika hili janga kama ambavyo Mama alijionea hali pale Mwananyamala hospitali.
 
Ije hata delta force. Kila mtu atakufa it’s a matter of time na kila mtu afanye kimpasacho kama ni chanjo it’s okay kwa yeyote atakaye

Mimi binafsi naamini siku ikifika imefika ila iwe kwa Mpango wa Mungu so iwe Corona kama ipo! It’s okay au gonjwa lolote sawa tu infact I never fear death kwa sababu ndio njia ya kunifikisha mbinguni
 
Naam.....

Baadhi wanakataa chanjo ilihali ndugu zao wanasafiri na wengine kwenda kufanya ibada za Hija Makka na Bethlehem.....

Yaani MADAKTARI na manesi wetu wanaotupambania afya zetu WASICHOMWE CHANJO ili wamalizike ?!!

Mijitu inasahau kuwa hao MADAKTARI na manesi wanawatibu wagonjwa wa UVIKO na jioni wanarejea kwenye familia zao ,na pia kujumuika nasi MABAA na VIJIWE VYA KAHAWA ...

Sasa wanataka waeneze UVIKO na kutufanya tupukutike sote wao na sisi raia?!!!

WANAOPINGA CHANJO ni wajinga KUPITILIZA.......

#KaziIendelee
Kumbe safari za Hijja bado zipo maana nakumbuka walisema lazima uwe umechanjwa na mwishowe wakahaghairisha kabisa hakuna safari za Hijja.
 
Niko Mwanza na ninazunguka maeneo mengi kwa wiki, Shughuli zinaendelea kama kawaida.

Kwetu ni Igogo na nisehemu yenye population kubwa, sijasikia habari za watu kuugua korona.

Ninao marafiki kibao Kirumba, Malimbe, Igoma n.k, Na nisehemu zenye mikusanyiko mikubwa lakini hakuna habari ya korona huko pia.

Mahari napoishi pia sijasikia habari za ugonjwa wala vifo vilivyosababishwa na korona.

Pengine walipaswa watoe ufafanuzi vizuri kwa sababu si kwamba oxygen nikwajili ya wagonjwa wa korona pekeake.

Kwa uhaba huo wa oxygen na ugonjwa huu unavyoenea kwa kasi tayari majibu yangekuwa yameshaonekana mitaani (vifo kama ilivyo uko uganda)
Tatizo hutakiwi kuhoji utaishia kuambiwa unakataa uwepo corona, we unatakiwa ukubali tu kinachoelezwa bila kuhoji.
 
Niliandika kama mara 4 hivi kuhusu COVID-19 sasa wanaiita Delta Variant. Nikaandika kiufupi tu kuwa hatuishi kwenye dunia ya peke yetu, nikaendelea kuhusu ugonjwa huu kuingia nchini kutoka Uganda, hakuna aliyejali.

Sasa leo ITV wametangaza upungufu wa oxygen Bugando. Niliomba Serikali yetu tukufu ipige marufuku mikusanyiko yote mipirani, mikutanoni na hata kwenye mazishi, misiba, harusini, mikutano ya hadhara ya kisiasa na kidini n.k. Nikaandika hilo gonjwa la COVID-19 au Delta Variant linateketeza wenzetu Uganda, bado watu hawaamini.

Sasa hayawi hayawi yamekuwa. Nilishangaa sana na hata kupigiwa simu na marafiki zangu waliopo nje ya nchi wakishangaa sana kuona mechi ya Simba na Yanga kujaza watu wote wale elfu 55 sio maskhara. Narudia tena kutoa wito kwa wahusika kupiga marufuku mikusanyiko ya watu. Jamani jamani tunaishi dunia hiyo hiyo ya wenzetu tena waafrika wanaoathirika na kuteketea.

Tulete chanjo ya Pfizer kupitia mahospitali binafsi na ya serikali. Anayetaka achanje asiyetaka shauri lake ila tutashindwa hata kwenda sokoni na hizo jezi za Yanga na Simba zitageuka sanda.

EEH ALLAH TUNUSURU NA WANUSURU WAJA WAKO WOTE AFRIKA NA DUNIANI.SISI TUNAKIRI MBELE YAKO KUWA TUNAISHI KATIKA DUNIA HIYO HIYO WANAOISHI WENZETU ULIYOIUMBA WEWE MTUKUFU PEKEE. AMEEN.
Acha wife. We will all die
 
Mkuu bora wewe umetuonea huruma .

Embu fikiria Mtu unatumia masaa mengiii, ndani ya wodi la UVIKO, na nikila siku

Alafu mpuuzi mmoja anakuambia, Hatutaki chanjoo

Maninaaaa !! Watu wabinafsi kinyama.
Hali ya corona kwa Tanzania huko hospitali ikoje? maana kuna hoja ya kwamba Tanzania tumejiachia kwa muda kutokuchukua tahadhari sasa mbona hatujaona hospitali kuzidiwa wagonjwa mpaka sasa kama athari za kutokuchukua tahadhari?
 
Korona ipo ila sio kwa kiwango hicho wanachotaka kukikuza, ingekuwepo kwa kiwango hicho wanacholazimisha mbona ingekuwa hatari, tunabanana kwenye daladala, masokoni, wanafunzi mashule mbona watu wangekuwa wanakufa kila saa.
Haya majamaa maongo kweli watu wanadunda tu mitaani wala hamna shida kabisa
 
Niliandika kama mara 4 hivi kuhusu COVID-19 sasa wanaiita Delta Variant. Nikaandika kiufupi tu kuwa hatuishi kwenye dunia ya peke yetu, nikaendelea kuhusu ugonjwa huu kuingia nchini kutoka Uganda, hakuna aliyejali.

Sasa leo ITV wametangaza upungufu wa oxygen Bugando. Niliomba Serikali yetu tukufu ipige marufuku mikusanyiko yote mipirani, mikutanoni na hata kwenye mazishi, misiba, harusini, mikutano ya hadhara ya kisiasa na kidini n.k. Nikaandika hilo gonjwa la COVID-19 au Delta Variant linateketeza wenzetu Uganda, bado watu hawaamini.

Sasa hayawi hayawi yamekuwa. Nilishangaa sana na hata kupigiwa simu na marafiki zangu waliopo nje ya nchi wakishangaa sana kuona mechi ya Simba na Yanga kujaza watu wote wale elfu 55 sio maskhara. Narudia tena kutoa wito kwa wahusika kupiga marufuku mikusanyiko ya watu. Jamani jamani tunaishi dunia hiyo hiyo ya wenzetu tena waafrika wanaoathirika na kuteketea.

Tulete chanjo ya Pfizer kupitia mahospitali binafsi na ya serikali. Anayetaka achanje asiyetaka shauri lake ila tutashindwa hata kwenda sokoni na hizo jezi za Yanga na Simba zitageuka sanda.

EEH ALLAH TUNUSURU NA WANUSURU WAJA WAKO WOTE AFRIKA NA DUNIANI.SISI TUNAKIRI MBELE YAKO KUWA TUNAISHI KATIKA DUNIA HIYO HIYO WANAOISHI WENZETU ULIYOIUMBA WEWE MTUKUFU PEKEE. AMEEN.
Kusema wana upungufu wa mitungi ya gesi haimaanishi wanawagonjwa wengi. Taarifa iliyotolewa inaelezea upungufu wa vifaa hivyo katika kukabiliana na tatizo endapo litatokea kwa ukubwa

Kifupi hayo yamesemwa katika hali ya kuweka tanadhari
 
Mwanza Kigoma Kagera
Mguu Sawa
Mambo Siyo Shwari
😣😏🙄😶😑😐😐
Tumtangulize Mungu!!!
 
Zile sala ambazo Magufuli pamoja na baadhi ya viongozi wa dini walituaminisha kwamba zilisaidia kuondoa covid 19 kipindi kile mbona sasa haziongelewi tena..!!

Hii nchi imejaa sana usanii. 🤣 🤣
Waliyotuambia hizo sala zimesaidia na wanaotuambia hali ya corona ni mbaya sana, hao wawili wanatofauti gani?
 
Kuongezeka kwa cases huko kunaweza kuhusishwa na janga la Uganda, ni kuzingatia tu njia za kujikinga zinazoshauriwa......mafua ya msimu hayajawahi kuleta crisis hadi ya kusababisha wagonjwa wengi wapate usaidizi wa kupumua kwa mashine ya oxygen.
 
Back
Top Bottom