#COVID19 Inasemekana kirusi cha COVID-19 aina ya Delta kimeingia Mwanza

#COVID19 Inasemekana kirusi cha COVID-19 aina ya Delta kimeingia Mwanza

Niliandika kama mara 4 hivi kuhusu COVID-19 sasa wanaiita Delta Variant. Nikaandika kiufupi tu kuwa hatuishi kwenye dunia ya peke yetu, nikaendelea kuhusu ugonjwa huu kuingia nchini kutoka Uganda, hakuna aliyejali.

Sasa leo ITV wametangaza upungufu wa oxygen Bugando. Niliomba Serikali yetu tukufu ipige marufuku mikusanyiko yote mipirani, mikutanoni na hata kwenye mazishi, misiba, harusini, mikutano ya hadhara ya kisiasa na kidini n.k. Nikaandika hilo gonjwa la COVID-19 au Delta Variant linateketeza wenzetu Uganda, bado watu hawaamini.

Sasa hayawi hayawi yamekuwa. Nilishangaa sana na hata kupigiwa simu na marafiki zangu waliopo nje ya nchi wakishangaa sana kuona mechi ya Simba na Yanga kujaza watu wote wale elfu 55 sio maskhara. Narudia tena kutoa wito kwa wahusika kupiga marufuku mikusanyiko ya watu. Jamani jamani tunaishi dunia hiyo hiyo ya wenzetu tena waafrika wanaoathirika na kuteketea.

Tulete chanjo ya Pfizer kupitia mahospitali binafsi na ya serikali. Anayetaka achanje asiyetaka shauri lake ila tutashindwa hata kwenda sokoni na hizo jezi za Yanga na Simba zitageuka sanda.

EEH ALLAH TUNUSURU NA WANUSURU WAJA WAKO WOTE AFRIKA NA DUNIANI.SISI TUNAKIRI MBELE YAKO KUWA TUNAISHI KATIKA DUNIA HIYO HIYO WANAOISHI WENZETU ULIYOIUMBA WEWE MTUKUFU PEKEE. AMEEN.
usitishe watu bhana
 
Nawashangaa sana watu wenye akili zao timamu wanaotulazimisha kukuza kitu ambacho tumekuwa nacho toka enzi na enzi leo kisa wazungu wametangaza na wanalikuza watu wanajikita kutukaririsha kitu cha kawaida kabisa ili kionekane ety kinatisha huo ni uongo mtupu

Lazima wasomi wa Afrika na viongozi wa Afrika waishi walau kwa 10% ya maisha yao halisi vinginevyo tutajikuta tunapiga mark time tu hakuna la maana tutakalofanya

Toka enzi na enzi kunapo mabadiliko ya Hali ya hewa tumekuwa tukiface mafua na hali hii hutokea mara tatu kila mwaka

Tangu watangaze kuwa tutakuwa na vifo vya makundi umekuwa ni uongo uongo tu tunabanana kwenye daladala masokoni kila pahala lakini hakuna kilichobqdilika

kwa hiyo waache mara moja kututisha kwa madhumuni yao binafsi
 
Mkuu, gonjwa la UVIKO 19 lipo, kwa hiyo ni vyema ukazidi kuchukua taadhari zote muhimu zinazosisitizwa na wataalamu wa afya, wewe binafsi na wana Mwanza wengine pia. Kamwe usilichukulie poa gonjwa hili kwa kulifananisha na mafua ya msimu.
 
Chukua tahadhari acha umbulula kudanganya watu Covid ipo tena mvaya sana
 
Mwaego wala wasikutishe. Hawa wazungu wanakuonea donge na mali zako. We puyanga zako tu
 
Nisiwadanganye ndugu zangu Mwanza hali sio nzuri kwa watu tulioko kwenye ofisi za watu wengi tumelishuhudia hili
 
Korona ipo ila sio kwa kiwango hicho wanachotaka kukikuza, ingekuwepo kwa kiwango hicho wanacholazimisha mbona ingekuwa hatari, tunabanana kwenye daladala, masokoni, wanafunzi mashule mbona watu wangekuwa wanakufa kila saa.
 
Aliyekwambia covid imetua mwanza leo nani? tangu wiki tatu zilizopita kuna cases za watu wanaopata mafua na kupoteza uwezo wa kuhisi harufu, labda kama wewe ndo umeona jambo geni. Karibu mwezi mzima wizara imeshatoa tahadhari za watu kujikinga na covid, au unataka waje wakufunge pingu za miguu. Aliyekwambia chanjo ya mabeberu ya Pfizer ndo itakulinda na kifo ni nani........yaani ulivyokurupuka kuleta hii taarifa ni kana kwamba kuna jambo geni...
Jinga kabisa wewe.
 
Back
Top Bottom