Tetesi: Inasemekana Nape Nnauye kavuliwa Uanachama wa Chama cha Mapinduzi..

Status
Not open for further replies.
Habari ambazo hazijathibitishwa zinasema Nape Moses Nnauye amevuliwa uanachama wa Chama cha Mapinduzi kufuatia kikao kilichoongozwa na Mwenyekiti jijini Dar es salaam leo...

Habari hizi ni za kunyapia nyapia zinasema hata Lazaro nae yuko matatani.

Nape Nnauye alikuwa ni waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo katika Serikali ya Awamu ya Tano kabla uteuzi wake kutenguliwa. Aliteuliwa katika baraza la mwanzo la mawaziri la Rais John Pombe Magufuli. Yeye pia ni mbunge wa jimbo la Mtama lililoko mkoani Lindi.

Hivi sasa Nape ana miaka 40 alizaliwa mkoani Mwanza Novemba 7, 1977 ambako mama yake mzazi alikuwa mfanyakazi katika sekta ya elimu. Mama mzazi wa Nape anaitwa Keziah, ni mwalimu ambaye amefanya utumishi wake hadi alipostaafu mwaka 2015 akiwa katika ngazi ya Ofisa Elimu wa wilaya anayeshughulikia takwimu. Asili ya mama mzazi wa Nape ni mkoa wa Singida, yeye ni Mnyiramba.

Baba mzazi wa Nape ni Moses Nnauye (marehemu) ambaye alistaafu utumishi wa umma akiwa Brigedia Jenerali wa Jeshi. Asili ya baba yake Nape ni mkoa wa Lindi, yeye ni Mmakonde wa Chiuta, Nyangamara.

Uzoefu mkubwa wa Nape katika masuala ya Uongozi umejikita katika masuala ya siasa zaidi kuliko “utaalamu”. Amekuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa tangu mwaka 2002 hadi 2012. Amekuwa mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho Taifa kuanzia mwaka 2002 hadi leo.

Mwaka 2010 hadi 2011 aliteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Masasi, mahali alikotumikia kwa mwaka mmoja kabla ya kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa mwaka 2011 na kisha mwaka huohuo akateuliwa kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa nafasi aliyoishikilia hadi mwishoni mwa mwaka 2015.

Nape alianza harakati za kusaka ubunge mwaka 2010, alishiriki katika kinyang’anyiro cha kura ya maoni ndani ya CCM katika jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam bila mafanikio (aliyeshinda kura za maoni ni Hawa Ng’umbi aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii wakati huo). Mwaka 2015 Nape alihamishia majeshi nyumbani kwao, jimbo la Mtama. Bahati kubwa aliyokuwa nayo ni kwamba mwanasiasa nguli ndani ya CCM, Bernard Membe alikuwa ameshatangaza kuliacha jimbo hilo ili agombee urais.

Nape akapambana na kushinda kura ya maoni ndani ya chama chake kwa kupata kura 9,344 dhidi ya mpinzani wake Selemani Mathew (mchezaji wa zamani wa Yanga) aliyepata kura 4,766 (baada ya kushindwa Selemani alihamia Chadema na kugombea kwa tiketi ya chama hicho). Kura za jumla zilizopigwa Oktoba 25 zilimtangazia Nape ushindi wa jumla wa kura 28,110, Mathew wa Chadema akatokea wa pili kwa kupata kura 13,918 huku mgombea wa CUF akishikilia nafasi ya tatu.

Nguvu

Mambo mawili makubwa yanajenga nguvu na uwezo wa Nape katika siasa za sasa. Kwanza, huyu ni mmoja wa wanasiasa vijana wenye nguvu na ushawishi mkubwa wa maamuzi ndani ya CCM. Mchango wake kwenye siasa za jumla za kuiimarisha CCM katika miaka ya hivi karibuni hauwezi kupimika. Yeye ndiye mwanasiasa kijana wa CCM aliyefanikiwa kuzunguka sehemu kubwa ya nchi akiinadi CCM kwa kutumia staili ya “kushambulia chama chake” akishirikiana na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana. Staili ile kwa kiasi fulani iliisaidia CCM kujadiliwa tena na wananchi, wengi wakianza kuona kuwa kumbe hata viongozi sasa wanasema hadharani kuwa chama kina matatizo ya maadili na mengine mengi.

Kukaa ndani ya CCM muda mrefu na kusimamia mambo mengi ya mabadiliko ya kimfumo ndani ya chama hicho kunamfanya Nape awe mmoja wa vijana wa sasa ndani ya CCM wanaokifahamu chama hicho kwa undani. Uzoefu wa namna hiyo ni jambo kubwa na umemjengea uwezo wa kutosha na uzoefu wa kujua wapi kuna matatizo gani yanayohitaji ufumbuzi wa aina gani. Hili ni jambo kubwa sana kwake japokuwa tutaendelea kupima utendaji wake.
Hawa Ng'humbi hajawahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii
 
Yes alikuwa anatafuta sababu ya kutumuliwa,ni dhahiri ana mipango yake
Hapo kwa mwenyekiti anaeona mbali asingemtimua angempa cheo chochote juu kucheza na beat lake, ila kumfukuza naona ndio wamechemka
Kwani kishafukuzwa?
 
Nape alikuwa mwanzilishi wa CCJ hivyo siyo mgeni katika uasi. Katika hili, tangu mwanzo alijua na alizungumzia hadharani yatakayompata pale alipokataa hadharani 'ubashite' kwenye tasnia anayosimamia. Kwa msimamo aliwavutia raia wengi. I am sure he will not regret his expulsion from ccm. Pengine hata atafurahia kufukuzwa kwani atakuwa huru zaidi 'to take the bull by the horns'.
 
unafikiri JK angepanick ule mchakato pale Dodoma ungeisha salama??..
Watu waliimba lakini siuliona alivyoovercome ile pressure kwa kughairisha kikao..
Mbona ilikuwa disaster tupu,unafiki ulimgharimu.
Yeye alikuwa na mdogo wake Membe ili watengeneze ufalme kama Korea Kaskazini.
Kwa ujinga au kwa kiburi fake akajikuta amekwaa kisiki,Team Lowassa wakapiga kura za chuki,ndio mnamuona Magu.Na kuna siku Magu atawatolea uvivu.
 
Kama ni kweli muda si mrefu utasikia cdm wanaanza kumsafisha kwa madodoki kuwa hakuhusika kwa lolote kufanikisha bunge live kutokomea kusikojulikana
Ni kwel ausiki mana ye anapokea oda kwa boss wake na kusimamia itekelezwe kama dereva wa gari ya mbowe ruksa inatoka ikulu kwa mnene
 
Mbona ilikuwa disaster tupu,unafiki ulimgharimu.
Yeye alikuwa na mdogo wake Membe ili watengeneze ufalme kama Korea Kaskazini.
Kwa ujinga au kwa kiburi fake akajikuta amekwaa kisiki,Team Lowassa wakapiga kura za chuki,ndio mnamuona Magu.Na kuna siku Magu atawatolea uvivu.

kama unakaa unasubiri hilo litokee utapoteza muda ndugu yangu, sasa aliyepoteza nani hapo.. Jk amekuwa Rais kwa 10 yrs na amemaliza muda wake amejiondokea. Huwezi kumlazimisha Jk amepende upande unaopenda wewe, kama binadamu naye ana choice yake na labda kama unavyosema ni kweli basi choice yake ilikuwa Membe na si huyo uliyempenda wewe..
 
Nape siwezi msamehe kwa alivyochangia kutufikisha Hapa

1.Mfungaji wa goli la mkono

2.Kashiriki kuzuia bunge live

3.Sheria kandamizi ya vyombo vya habari

4.Kashiriki kikamilifu kuchonga kinyago cha mpapure na kukiweka sebuleni
Ngoja kwanza wengi atutamsamehe tupate uakika anaweza pewa warning [emoji615] tu c unajua wale wanamapepe kweny maamuzi
 
Usiri umetawala....nawaona mnatapatapa na story zenu za kutunga kama kawaida yenu.
 
kama unakaa unasubiri hilo litokee utapoteza muda ndugu yangu, sasa aliyepoteza nani hapo.. Jk amekuwa Rais kwa 10 yrs na amemaliza muda wake amejiondokea. Huwezi kumlazimisha Jk amepende upande unaopenda wewe, kama binadamu naye ana choice yake na labda kama unavyosema ni kweli basi choice yake ilikuwa Membe na si huyo uliyempenda wewe..
Kuna watu wanahitimu na kuna wale wanasindikiza wahitimu ila wao hawahitimu,ni bora ukatumia mantiki na kupunguza muda wa hasara.
 
Hicho ni chama cha wanaokubaliana kwa kila kitu (Yesmen Political Party). Ukipenda uhuru wa maoni ni lazima ukimbie huko, la watakufurusha.
 
Habari ambazo hazijathibitishwa zinasema Nape Moses Nnauye amevuliwa uanachama wa Chama cha Mapinduzi kufuatia kikao kilichoongozwa na Mwenyekiti jijini Dar es salaam leo...

Habari hizi ni za kunyapia nyapia zinasema hata Lazaro nae yuko matatani.

Nape Nnauye alikuwa ni waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo katika Serikali ya Awamu ya Tano kabla uteuzi wake kutenguliwa. Aliteuliwa katika baraza la mwanzo la mawaziri la Rais John Pombe Magufuli. Yeye pia ni mbunge wa jimbo la Mtama lililoko mkoani Lindi.

Hivi sasa Nape ana miaka 40 alizaliwa mkoani Mwanza Novemba 7, 1977 ambako mama yake mzazi alikuwa mfanyakazi katika sekta ya elimu. Mama mzazi wa Nape anaitwa Keziah, ni mwalimu ambaye amefanya utumishi wake hadi alipostaafu mwaka 2015 akiwa katika ngazi ya Ofisa Elimu wa wilaya anayeshughulikia takwimu. Asili ya mama mzazi wa Nape ni mkoa wa Singida, yeye ni Mnyiramba.

Baba mzazi wa Nape ni Moses Nnauye (marehemu) ambaye alistaafu utumishi wa umma akiwa Brigedia Jenerali wa Jeshi. Asili ya baba yake Nape ni mkoa wa Lindi, yeye ni Mmakonde wa Chiuta, Nyangamara.

Uzoefu mkubwa wa Nape katika masuala ya Uongozi umejikita katika masuala ya siasa zaidi kuliko “utaalamu”. Amekuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa tangu mwaka 2002 hadi 2012. Amekuwa mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho Taifa kuanzia mwaka 2002 hadi leo.

Mwaka 2010 hadi 2011 aliteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Masasi, mahali alikotumikia kwa mwaka mmoja kabla ya kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa mwaka 2011 na kisha mwaka huohuo akateuliwa kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa nafasi aliyoishikilia hadi mwishoni mwa mwaka 2015.

Nape alianza harakati za kusaka ubunge mwaka 2010, alishiriki katika kinyang’anyiro cha kura ya maoni ndani ya CCM katika jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam bila mafanikio (aliyeshinda kura za maoni ni Hawa Ng’umbi aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii wakati huo). Mwaka 2015 Nape alihamishia majeshi nyumbani kwao, jimbo la Mtama. Bahati kubwa aliyokuwa nayo ni kwamba mwanasiasa nguli ndani ya CCM, Bernard Membe alikuwa ameshatangaza kuliacha jimbo hilo ili agombee urais.

Nape akapambana na kushinda kura ya maoni ndani ya chama chake kwa kupata kura 9,344 dhidi ya mpinzani wake Selemani Mathew (mchezaji wa zamani wa Yanga) aliyepata kura 4,766 (baada ya kushindwa Selemani alihamia Chadema na kugombea kwa tiketi ya chama hicho). Kura za jumla zilizopigwa Oktoba 25 zilimtangazia Nape ushindi wa jumla wa kura 28,110, Mathew wa Chadema akatokea wa pili kwa kupata kura 13,918 huku mgombea wa CUF akishikilia nafasi ya tatu.

Nguvu

Mambo mawili makubwa yanajenga nguvu na uwezo wa Nape katika siasa za sasa. Kwanza, huyu ni mmoja wa wanasiasa vijana wenye nguvu na ushawishi mkubwa wa maamuzi ndani ya CCM. Mchango wake kwenye siasa za jumla za kuiimarisha CCM katika miaka ya hivi karibuni hauwezi kupimika. Yeye ndiye mwanasiasa kijana wa CCM aliyefanikiwa kuzunguka sehemu kubwa ya nchi akiinadi CCM kwa kutumia staili ya “kushambulia chama chake” akishirikiana na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana. Staili ile kwa kiasi fulani iliisaidia CCM kujadiliwa tena na wananchi, wengi wakianza kuona kuwa kumbe hata viongozi sasa wanasema hadharani kuwa chama kina matatizo ya maadili na mengine mengi.

Kukaa ndani ya CCM muda mrefu na kusimamia mambo mengi ya mabadiliko ya kimfumo ndani ya chama hicho kunamfanya Nape awe mmoja wa vijana wa sasa ndani ya CCM wanaokifahamu chama hicho kwa undani. Uzoefu wa namna hiyo ni jambo kubwa na umemjengea uwezo wa kutosha na uzoefu wa kujua wapi kuna matatizo gani yanayohitaji ufumbuzi wa aina gani. Hili ni jambo kubwa sana kwake japokuwa tutaendelea kupima utendaji wake.
Ni vigumu ku-join pieces na kupata jibu hasa ilikuwaje Nape akawa so famous CCM.Mambo mengine ni kitendawili tega.Alibebwa?God knows.
 
Hivi ni kweli wana kaya hii KUNA AMBAYE HAJUI KOSA LA NAPE NA KWA SASA NYARANDU .BASI HUYO YUKO NCHI NYINGINE .
 
Nape akifukuzwa CCM Ndo ameisha kisiasa kabisa. Hata huyo Lazaro ni mwepesi sana kisiasa. Ni muumini wa kununua kura kuliko siasa za ushawishi.
 
Hivi ni kweli wana kaya hii KUNA AMBAYE HAJUI KOSA LA NAPE NA KWA SASA NYARANDU .BASI HUYO YUKO NCHI NYINGINE .
Kwani ana kosa gani mkuu na sisi tufahamu, ama kutoa maoni yako ni kosa siku hizi?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom