MwananchiOG
JF-Expert Member
- Apr 4, 2023
- 1,970
- 4,037
Baada ya Makosa makubwa na uvunjifu mkubwa wa kikanuni uliofanywa na Bodi ya Ligi, Inashangaza kuona mpaka sasa ni Mjumbe mmoja tu ambaye ni Mjumbe wa kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa ligi kuu Tanzania bara Ndugu Filimon Ntahilaja ambaye amejiuzulu nafasi yake na kutoka nje ya kikao baada ya maamuzi ya kutolewa ambapo yeye anaamini hayakuwa maamuzi sahihi.
Bodi ya Ligi imejidhihirisha kuwa ni taasisi isiyoheshimu miongozo na kanuni inayojiwekea. Maamuzi ambayo yameigharimu sana sekta ya michezo nchini, maamuzi yaliyowaathiri maelfu ya mashabiki na wapenzi wa mpira barani Afrika. Bodi ya Ligi imefanya maamuzi ya kukurupuka na kuathiri mashabiki, wadau na wawekezaji ambao wameathirika kwa kiasi kikubwa.
WITO : Ni wakati sasa Bodi ya Ligi, kama jinsi wanavyoadhibu vilabu vingine kwa faini. Nayo inapaswa ijiwajibishe kwa makosa haya makubwa. Pia kama kuna baadhi ya viongozi wa TFF ambao wamehusika kufanya maamuzi haya mabovu ambayo hayapo kikanuni nao wachukuliwe hatua kali.