Victoire
JF-Expert Member
- Jul 4, 2008
- 24,386
- 57,588
Nimejiuliza, Rais wetu mpendwa alipokuwa Mwalimu pale Sengerema Secondary School, alipoomba Ruhusa ya kwenda kugombea Ubunge kule Biharamulo. Je, aliachishwa kazi? Watu wanaomba ruhusa ili wakajaribu bahati zao, badala ya kupewa ruhusa wanatumbuliwa. Hii mnaionaje raia?
Binafsi naona sio sawa jamani au kwa vile ni nafasi za kuteuliwa? Najiuliza wale wa kwenye Sector zisizo za kuteuliwa i.e Watumishi wengine mfano walimu n.k wakiomba ruhusa nao wataachishwa kazi badala ya kupewa ruhusa. It means ukishindwa imekula kwako.
Hii ndo Tanzania ya Magufuli.