Inashangaza: Watu wanamuomba ruhusa Rais Magufuli, badala ya kupewa wanatumbuliwa

Inashangaza: Watu wanamuomba ruhusa Rais Magufuli, badala ya kupewa wanatumbuliwa

Sasa wakati wewe umeomba ruhusa huku nyuma kazi zako afanye nani? Serikali hii umeshaambiwa kauli mbiu yake ni HAPA KAZI TU, sasa unadhani wananchi kero Zao zitatatuliwa na nani wakati wewe haupo?

Usifananishe sijui na mwaka 1985 au sijui serikali zilizopita, kila Rais ana mikakati yake ya kuendesha serikali, ukiomba ruhusa tunakupa mkono wa kwaheri, wengine waje waendeleze gurudumu, sasa we unataka kipindi uko kwenye kampeni nani afanye kazi zako?
 
Miaka ya 2000 mwanzoni ilitoka sera sijui sheria, ukiwa mwajiriwa ukaamua kuonesha nia kazi unaondolewa.

Namkumbuka dada roz pale mbeya aliingia kugombea kupitia cuf kazi ikaishia na ubunge kakosa.

Labda wamepunguza makali
Ukiwa CCM hata ukiacha kuingia kazini hakuna shida
 
Kwa hasira za yule bwana, hao waliomba ruhusa, wamekosa mwana na maji ya moto. Hata Ubunge majina yao hayarudi.
 
Jiwe anajulikana kwa double standards.

1. Wale wavunjie nyumba wamejenga barabarani, wale waache wamenipa kura

2. Wale wafukuzwe kazi wanavyeti feki lakini zoezi hilo halifanyiki majeshini wala kwa wateule wake

3. Hakuna kufanya siasa mpaka 2020 huku yeye chama chake kikifanya siasa

4. Vifisadi vidogovidogo anakomaa navyo na kuvitoza hela wakati mafisadi yaliyomo ndani ya CCM ameyachunia tu
 
Kuacha majukumu yako kama Dc au DED na kuanza kampeni huku wanachi wanakosa watu wa kutatua kero zao huko ni kuomba ruhusa!
Haya mambo CCM wenyewe ndio walioyaharibu. Utaona Waziri anakwenda kwenye kampeni zake binafsi anatumia gari ya Waziri ambayo huduma zake zinalipiwa na wananchi walipa kodi. Wateuzi wa rais wanakwenda kwenye mikutano ya siasa CCM haina uhusiano wowote nanutendaji wao lakini bado wanatumia fursa walizopewa na serikali ambazo hulipiwa na walipa kodi.

Sheria ziko wazi lakini wavunjaji sheria ni wao wenyewe. Ifike wakati tuheshimu sheria tulizojiwekea wenyewe. Kutoheshimu sheria ndiko kunakopelekea kuzidi vitendo vya rushwa na ubadhirifu wa mali za umma. Kwa maana hiyo ni kuikosesha serikali mapato na kudumiza wananchi kwenye janga la umasikini!!
 
Sasa wakati wewe umeomba ruhusa huku nyuma kazi zako afanye nani? Serikali hii umeshaambiwa kauli mbiu yake ni HAPA KAZI TU, sasa unadhani wananchi kero Zao zitatatuliwa na nani wakati wewe haupo? Usifananishe sijui na mwaka 1985 au sijui serikali zilizopita, kila Rais ana mikakati yake ya kuendesha serikali, ukiomba ruhusa tunakupa mkono wa kwaheri, wengine waje waendeleze gurudumu, sasa we unataka kipindi uko kwenye kampeni nani afanye kazi zako?
Si kuna wasaidizi watakaimu, ruhusa wanaomba ni kama kipindi cha zile wiki mbili au tatu za kura ya maoni. Hawaombi likizo ya ma miezi kadhaa.
 
Haya mambo CCM wenyewe ndio walioyaharibu. Utaona Waziri anakwenda kwenye kampeni zake binafsi anatumia gari ya Waziri ambayo huduma zake zinalipiwa na wananchi walipa kodi. Wateuzi wa rais wanakwenda kwenye mikutano ya siasa CCM haina uhusiano wowote nanutendaji wao lakini bado wanatumia fursa walizopewa na serikali ambazo hulipiwa na walipa kodi.

Sheria ziko wazi lakini wavunjaji sheria ni wao wenyewe. Ifike wakati tuheshimu sheria tulizojiwekea wenyewe. Kutoheshimu sheria ndiko kunakopelekea kuzidi vitendo vya rushwa na ubadhirifu wa mali za umma. Kwa maana hiyo ni kuikosesha serikali mapato na kudumiza wananchi kwenye janga la umasikini!!
Ni double standards sasa, kumbe kuna wakubwa na kampeni wameanza ?Au wao ni vile hawajaomba ruksa ndo maana wanatesa tu?
 
Someni alama za nyakati. Sio lazima tufuate ya enzi hizo eti kwa sababu fulani alifanya. Hii nzuri, na itasaidia kuwa na msimamo na kujiamini.

Tulia sehemu moja na kuna vitu vingi vya kufanya sio lazima ukagombee... fuga hata kuku na utakuwa mfugaji bora wa kimataifa huku ukiendelea na ajira yako, sio kufukuzia vyeo vya majukwani. Kama baridi ni baridi na kama joto ni joto USIWE vuguvugu.

Mtu una kitu mkononi bado unawinda na kingine, wasio nacho wafanyeje? Tayari wewe ni Mkurugenzi wa mahali fulani, unataka Ubunge ili upate Uwaziri ... sio mbaya acha ukurugenzi kapambane jimboni, ukikosa huko utatia akili... 😕 🙁

Mapovu ruksaaaaaaa......
 
Acheni tamaa wengine hawana ajira bado mnawazongazonga mtaka yote hukosa yote. Hii inaonyesha wazi kwamba mnafanya kazi ambazo.

Sio profession zenu. Wewe ni mwalimu alafu unataka siasa basi ualimu sio profession yako unaganga njaa tu alafu unalaumu.
Kwani MHESHIMIWA Rais anatokea katika shughuli ipi mkuu?
 
Makonda Yupo Kigamboni Anaangaika Tu Halafu, Uwa Namwangalia Mtumbuaji Namuona Kama Hajielewi Hivi.
Itakuwa yeye bado hajaomba ruksa. Akiandika barua ya kuomba ruksa basi ndo itakuwa imekula kwake.
 
Back
Top Bottom