Inashangaza: Watu wanamuomba ruhusa Rais Magufuli, badala ya kupewa wanatumbuliwa

I knw!
Lakini kwa hali ilivyo ss,namuonea huruma! Aombe Mungu tu amsaidie!
Polepole alisema waache tamaa!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwenye maisha usipokuwa na tamaa utaendelea kweli ?Wote tusingekuwa na tamaa basi tungeishia la kwanza. Binadamu ili usonge mbele lazima utoke kwenye comfort zone.

Lazima kila hatua unayofika utamani kwenda mbele zaidi mpaka hapo kifo au ugonjwa utakaokuzuia kusonga mbele vikupate.
 
Lazima kila hatua unayofika utamani kwenda mbele zaidi mpaka hapo kifo au ugonjwa utakaokuzuia kusonga mbele vikupate.

Nimejikuta nawaza kwanini unaipambania sana hii hoja japokua kuna uwezekano mkubwa haijakugusa moja kwa moja.

Nadhani kuna umuhimu wa hili suala kukemewa, maana kwa jinsi wateule walivyo wepesi wa kutafsiri na kutekeleza maagizo yasiyokuwepo kwenye sheria, ipo siku tutajikuta wakurugenzi huko halmashauri wanatukatalia hata kwenda kusoma kwa kigezo kwamba uliajiriwa kwa nafasi hiyo unatakiwa utumikie hiyohiyo.
 
Mahali pa kumpinga unamsifia penye kumsifia unampinga, anyways ndio demokrasia yenyewe hiyo.
 
Inanishangaza maana wakati mwingine naona kama vile Watanzania tunataka tuongozwe na malaika.
Mzee Baba ktk awamu yake hii inayoisha kafanya mengi na hawezi yeyote akafananisha awamu hii na awamu zilizopia.Msema kweli ni mpenzi wa Mungu
Ameyafanya mengi yapi, mbona mie siyaoni? Hivi hujaona akina Kikwete walivyosambaza barabara nchi nzima?
Miaka mitano umeona barabara gani ya maana imejengwa
 
Miaka ya 2000 mwanzoni ilitoka sera sijui sheria, ukiwa mwajiriwa ukaamua kuonesha nia kazi unaondolewa.

Namkumbuka dada roz pale mbeya aliingia kugombea kupitia cuf kazi ikaishia na ubunge kakosa.

Labda wamepunguza makali
Huyu alikwenda chama pinzani ,hakujitambua mapema ,angekeenda ccm mpka sasa angekuwa kazini
 
Miaka ya 2000 mwanzoni ilitoka sera sijui sheria, ukiwa mwajiriwa ukaamua kuonesha nia kazi unaondolewa.

Namkumbuka dada roz pale mbeya aliingia kugombea kupitia cuf kazi ikaishia na ubunge kakosa.

Labda wamepunguza makali
dada rose aligombea kwa tiket ta cuf ndo maana. ukigombea kwa ccm hakuna tabu mambo murua kabisa wapo hata wa NEC ni watumishi wa umma lakini hakuna wakuwagusa.
 
Dada,usifananishe miaka hiyo na miaka hii, kila Rais ana kipaumbele chake, mbona umekazania sana mfano huo wa Sengerema? Kila nabii anakuja na kitabu chake, hebu fikiria, RC, RAS, DC, DAS, WAKURUGENZI WOTE WA MKOA NA WILAYA wote wa mkoa mmoja waombe ruhusa ya wiki Mbili hali itakuaje hapo mkoani?
 
Mahali pa kumpinga unamsifia penye kumsifia unampinga, anyways ndio demokrasia yenyewe hiyo.
Mimi nampinga kuwabania wenzake,wakati yeye hakubaniwa. Ila baniani mbaya kiatu chake dawa. Ipo siku akili itamkaa vizuri. Umesikia Rais wa Brasil ana Covid 19?
 
Mimi nampinga kuwabania wenzake,wakati yeye hakubaniwa. Ila baniani mbaya kiatu chake dawa. Ipo siku akili itamkaa vizuri. Umesikia Rais wa Brasil ana Covid 19?
Nimefika, na bado, wabishi wote lazima wanyamaze
 
Mkuu izo nafasi tayari wanazo wazifanyie kazi tu ili walete maendeleo kwa wananchi na taifa kwa ujumla.ubunge waache na wengine ambao hawana nafasi wakatumikie wananchi. me nakuelewa Sana mh. Rais kwenye hili
 
Mkuu usikengeuke...Yeye aligombea ubunge mara mbili na akashindwa,vipi aliacha kazi ya ualimu?
Utaratibu nikua mtu anaomba ruhusa ya likizo bila malipo
Mkuu izi nafasi za kuteuliwa aliyekuteua anaweza kukutengua kulingana na kasi anayoihitaji kwenye serikali yake . Ualimu ni ajira ya kudumu ya utumishi wa umma kwa utaratibu ukiomba ruhusa bila malipo kwa mwajiri wako atakupa utaratibu wa kufuata.
 
Ni kweli kila mtu anahitaji zaidi lakini kwa wakati sahihi tukiliacha ili swala litakuja kutuletea matatizo makubwa Kama taifa kila mtu atakua mwanasiasa kwa sababu ndo Kuna maslahi mazuri alafu kazi ndogo kwaio tutakosa wataalamu kwenye taaluma mbalimbali . Lakini pia Mimi binafsi nachukia wanaotafuta uongozi kwa lengo la kujiongezea kipato Hawa watu hawatakua njia ya kutatua changamoto za watanzania mtu ni RC,DC, mkurugenzi izi nafasi zinawatosha kuwahudumia watanzania Kama Wana Nia ya dhati
 
Kila raia wa Tanzania mwenye sifa stahiki ana haki ya kugombea nafasi yoyote ya kisiasa sijui kwa hawa wateule wa Rais wanapoteuliwa wanapoteza haki kugombea wakiwa kwenye vyeo hivyo walivyoteuliwa?au ndiyo wamenyimwa haki yao?.Kwenye utumishi wa Umma kuna sheria, Kanuni na Taratibu za utumishi ni vyema ikawekwa wazi kuwa katika vyeo fulani vya kuteuliwa na Rais hairuhusiwi kugombea nafasi za kisiasa ukiwa kwenye nafasi hizo za kuteuliwa. Kabla ya utaratibu huu, zamani mtumishi wa umma aliyetangaza nia ya kugombea ubunge alikuwa anaomba ruhusa kwa mwajiri wake kipindi cha kura za maoni kwenye vyama vya siasa na pindi anapopitishwa na chama chake kupeperusha bendera alitakiwa kujiuzuru utumishi wa umma na iwapo atashindwa kura za maoni alirejea kazini
 
Mkuu unajua ukikaa chini na kujiuliza unagundua kuwa haiwezekani...wewe ukiamua kuondoka Basi na nafasi yako inaenda na wengine. MKUU HEBU KAA CHINI UFIKIRIE utaona kabisa that's unfair.
Mkuu hii ni fair kabisa Kama unatamani nafasi nyingine ya juu hii ya chini unawaachia wengine nao
 
Mkuu kazi ya ualimu hakua ameteuliwa na mtu
 
Mkuu kongole kwa kuweka kumbukimbu vizuri
 
Huyu ni dikteta, Watanzania wana haki ya kuomba ruhusa kwa waajiriwa wao ili wakagombee nafasi yoyote ile ya uongozi na kama watashindwa wanaruhusiwa kurudi kwenye ajira zao bila matatizo lakini kwa kuwa kuna dikteta magogoni basi ndiyo hivyo tena.

 
Noted ni kweli katiba inatoa Uhuru kwa raia kugombea nafasi mbalimbali za uongozi na mh. Rais hajamkataza mtu kugombea anawapa ruksa kwa sababu anajua ni HAKI zao za kikatiba lakini katiba hio hio inampa mamlaka mh. Rais kufanya mabadiliko kwenye teuzi zake ili aendane na kasi anayoitaka kwenye serikali yake
 
Hio ruksa kwiooo..mbna km Mh anawatega na hiiiiiiihiii😅
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…