Inasikitisha; Kijana ajiua baada ya kukosa ajira Jeshini

Inasikitisha; Kijana ajiua baada ya kukosa ajira Jeshini

Kwani China , Japan hawajinyongi? Swala lililopo hapa ni ishu ya mtu kujitoa uhai wake. Sio ishu ya kuendelea ama kutokuendelea. Kwa taarifa yako, Mtu kujitoa uhai wake ni ishu ya kiroho.

NJOO KWA YESU UOKOLEWE.
Ametoa sababu ni ajira, sasa huko ndio ajira zinapatikana?
 
Ingawa siungi mkono kitendo cha huyu kijana uamuzi aliuufanya lakini serekali haikutumia busara kutangaza kienyeji kusitisha ajira hizo ilikurupuka, kwanini waliwapatia mafunzo kama walikuwa bado haeajajipanga?
 
  • Thanks
Reactions: 1gb
Kijana Sunday Matara(28)amejiua kwa kujinyonga baada uongozi wa Jeshi la Kujenga Taifa kusitisha mafunzo kwa vijana wa kujitolea 2020/2021..
maisha hayajawahi kuwa Rahisi hapa duniani, unapopitia mazingira magumu ndipo unapo imarika. Wewe mbona maisha yamekuchapa na hujajiua. Huyo kijana ni mjinga tu.
 
  • Thanks
Reactions: 1gb
" Vijana Mjiajiri "
Tunahitaji maridhiano kwanza,

Nchi ni tajiri toka 2016 pambio la mkulu ni hili sasa,huo utajiri unaliwa na nani.

Hua inaleta maudhi kwenye familia mzazi anakwambia mwanangu,mm mzazi wako nina pesa,na unaambiwa na mzazi mwenyewe wala sio majirani na hizo pesa huzioni unashindia vi malapa.

Unaonaje? Na hili la utajiri wa nchi lkn vijana wake wanajiua kwa kukosa ajira inafurahisha eee.



Ukimkosa Yesu katika maisha yako, shetani atakuchezea kama anavyotaka, na kisha hatimaye atakuchukua jumla.


YESU NI BWANA NA MWOKOZI.
Mkuu habari za kukosa ajira na kumkosa Yesu havina mahusiano.

Wanaokumbwa na tatzo hili ni la watu wote walio na Yesu na wasio na Yesu.

Au labda kama unazungumzia shetani wa nchi,hapo sawaa.

Anatuchezea kwelikweli.

Mm mwnyewe nna Yesu,na ninashuhudia vijana wengi kwenye jumuiya ya makanisani wanatoka makamasi kwa kulia sana kanisani,kisa hawana ajira.

Hili jambo linahitaji utatuzi serious bro. Kanisa lina maombi ya kufunga na kuomba kila mwaka kuombea uchumi wa mtu mmoja mmoja. Na hali bado ni ngumu,

Katika mwezi huwezi kosa ujumbe wa mahubiri yanayojikita katika kusaidia wachungaji,utoaji,zaka na semina za ujasiriamali.

Ivi unadhani kwenye makanisa nje ya nchi washirika wenye kipato kizuri washirika wamefanikiwa kuna mahubiri ya namna hiyo?zaidi ya mahubiri ya kuachana na madawa ya kulevya,sonona(depression) na break through!

Huko hawahubiriwi kupanda ndege,kujenga nyumba wala kumiliki magari maana tyr wanayo toka wapo kindergaten.
Kama utoaji wanatoa vizuri maana tyr wanavyo.

Tuwe serious kidogo bro.
 
maisha hayajawahi kuwa Rahisi hapa duniani, unapopitia mazingira magumu ndipo unapo imarika. Wewe mbona maisha yamekuchapa na hujajiua. Huyo kijana ni mjinga tu.
Ahhahaahahah..
Sasa tunawasaidiaje hawa vijana wajinga wasiendelee kujiua.
Tunawaachaje achaje yaani.
 
Serikali mnaona madhara ya mfumo mbovu wa Elimu?

Badilisheni mfumo wa elimu haraka kuokoa next generation.
 
Ahhahaahahah..
Sasa tunawasaidiaje hawa vijana wajinga wasiendelee kujiua.
Tunawaachaje achaje yaani.
Kwanza kijana lazima ajifunze kumtegemea Mungu aliyemleta duniani na asimtegemee mwanadamu. Mungu ndiye anayejua hatima yote ya maisha yako. Sasa ukianza kutegemea mwanadamu mwenye akili kama zako mimi sidhani kama ni sawa.

Kwasababu ndugu yangu hata wewe ukiamua unaweza kuwa kiongozi, ni uaumuzi wako tu. Yaani hata wewe unaweza kuwa waziri mkuu, unaweza kuwa Rais, sasa mwenzako alichukua uthubutu leo amekua waziri, alafu unaanza kumlalamikia mara hamtupi ajira mara maisha magumu. Huo ni ukosefu wa maarifa
 
  • Thanks
Reactions: 1gb
Nashangaa mtu katoka JKT eti anaona suruhuhisho ni kujinyonga mjinga kabisa wakati furusa zipo kibao bora yeye yuko na elimu vp kwa wale wasio na elimu wala ujuzi lkn life linasonga tatzo tunawaza kuajiriwa kuliko kujiajiri wenyewe na kuji

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Kwa mafunzo uliyoyapata bwana marehemu, ulishindwaje kukodi hata SMG nakuingia zako chattle?

Umekufa kibwege sana na mafunzo yako ya JKT.
Ameshindwa hata kukaba roba hawa walevi wanaoyumbayumba hapa mtaani kwetu ama labda mafunzo ya JKT yalimuacha na ulemavu hasa wa vile zile organ zetu WALUME
 
Serikali mnaona madhara ya mfumo mbovu wa Elimu?

Badilisheni mfumo wa elimu haraka kuokoa next generation.

Na hili ndilo tatizo kubwa!

Pumzika kwa Amani kijana, Muumba wa vyote akupe pumziko la Amani na Faraja!

Mfumo wa elimu haumuandai mwanafunzi/msomi kufikiria nje ya box ama kupambana na maisha katika mazingira ya aina yoyote yale! Magumu, mepesi ama ya kawaida (maana hata baadhi ya wanaojiriwa nao wanaishi hand to mouth tu! Salary to salary!

Ila pia jamii kwa ujumla wake nayo haiwezi kukwepa lawama hii! Jamii ambayo ni wazazi, walezi, ndugu, jamaa na marafiki nayo iwe tayari kusaidia kwa kila hali kuhakikisha vijana wanakua katika mazingira/mifumo yenye kupeleka fikra nje ya box na kukabiliana na aina yoyote ya maisha!

Tu adopt tabia ya kusaidiana kwa vyovyote vile (hali ama Mali) ili kupunguza hali mbaya za kiuchumi katika jamii zetu! Uchoyo na ubinafsi ni sumu mbaya sana, ni sawa na Asali kwenye bakuli la dhahabu katikati ya shimo la taka limezungukwa na nzi!

Lakini pia Vijana /wahitimu/ wasomi, nao wapunguze expectations kubwa kubwa na nyingi zilizokosa reality katika maisha yetu halisi! Ubunifu uwe ndio pathway ya kuyajenga maisha yetu! Tutumie vyanzo tulivyonavyo/ vinavyotuzunguka kubuni njia za kutengeneza vyanzo vya mapato na kujiendeleza na kuziendeleza jamii zetu! Tusiogope kuonekana vichaa katika ubunifu!!!

High school kuwa Life skills schools is the best option and opportunity all together! Kwenda mafunzo JKT ibaki uchaguzi na mapenzi ya mtu/wito kama ilivyo Udaktari ama Usanii! Dunia ya sasa inahitaji upambane kama vile roho yako itatoka the next second!

Poleni sana wote mliofikwa na msiba huu, Muumba awape Subra!
 
Ameikimbia vita ya maisha, Bwana alitoa na Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe
 
Serikali ya nchii hii hawajali vijana hata kidogo, kwa vile na sisi wengi wetu bado hatujajitambua,
Basi.. tuendelee kuisoma namba.
 
Huyu kwelee Mara,anakulaa bakora hamsaa nyambafuuu then ndo akazikwee
 
Back
Top Bottom