Inasikitisha sana hakuna mshambuliaji wa simba mwenye magoli 6 mpaka sasa

Inasikitisha sana hakuna mshambuliaji wa simba mwenye magoli 6 mpaka sasa

Kuna makosa yalifanyika wakati wa usajili kwa viongozi wa Simba kuacha kusajili washambuliaji wa kati. Huu ndio ukweli mchungu ambao baadhi ya mashabiki wa Simba hawataki kuukubali. Lakini wanashindwa tu kujiuliza maswali yafuatayo:-
1. Hivi kwa mikrosi ile ya Sakho, Banda, Mohamed Hussein na Kapombe iwapo Simba ingekuwa na mshambuliaji mahiri ingekuwa na magoli
mangapi na Ingekuwa nafasi ya ngapi kwenye ligi sasa hivi?
2. Vipi kwa zile "one two" za Chama na Morison iwapo Simba ingekuwa na mshambuliaji mwenye "kontroo" nzuri mguuni? Kagere hata kutuliza
mpira tu kawaida anapata shida anapoteza kwa adui au anatoa nje.
3. Je vipi iwapo Simba ingekuwa na mshambuliaji mwenye matumizi mazuri ya mipira ya juu mwenye uwezo wa kupiga vichwa mipira ikaingia
golini.
4. Je vipi iwapo Simba wangekuwa na mshambuliaji mwenye kasi na uwezo wa kuwapangu angalau tu hata mabeki wawili kwa pamoja?

Kwa ufupi tu Simba ilijisahau baada ya mafanikio ya takribani miaka minne mfululizo. Ikaimarisha ukuta wake zaidi kwa kumuleta Inonga (ambaye ni mtu na nusu) lakini walijisahau kuifanyia tathmini safu yao ya ushambuliaji. Kitendo cha msimu uliopita baadhi ya magoli kufungwa na viungo Chama na Luis na walitoa "assist " nyingi na ndio walikuwa wanaondoka basi viongozi wa Simba walitakiwa watafute mshambuliaji anayejiweza mwenyewe sio hao walionao wa kusubira tu wawekewa kwenye njia wafunge.
Umeandika pumba kabsa mkuu,Simba bado ni imara Sana,mshambuliaji sio lazma awe anafunga Kila sku!!!! Nafkir unaongozwa na pressure kuropoka haya unayoropoka
 
Umeandika pumba kabsa mkuu,Simba bado ni imara Sana,mshambuliaji sio lazma awe anafunga Kila sku!!!! Nafkir unaongozwa na pressure kuropoka haya unayoropoka
Mbona kama wewe ndio unaropoka..!
 
Back
Top Bottom