Inasikitisha sana kuona baadhi ya hospitali binafsi ambazo ni PENDWA zinagomea kutoa huduma

Nilitegemea Serikali kutoa tamko la maana kumbe wakatoa tamko la kitoto kabisa. Serikali iache kuzikandamiza Hospitali kwa kigezo cha huduma, wanatakiwa kutafuta ufumbuzi wa suala hilo maana NHIF imepigwa na wao wenyewe halafu leo wanataka kubebesha mzigo Hospitali.
 
Ungezitaja tu mkuu..
 
Shida kubwa ya taifa hili ni kufanya mambo ili kupata sifa za kipumbavu za kisiasa,watu walisha onya mara nyingi kwamba serikali isifanye kila jambo kuwa la kisiasa Kuna mambo ni sensitive sana hasa afya.

Waziri amekaa kama public relations officer, badala ya mtatunzi wa matatizo ya afya.Matamko anaona kama ndo uwajibikaji.

Bure kabisa.
 
Tatizo lako ndugu muuguzi(Nursing officer) ni uchawa
 
Hospitali ilibebwa?

 
Siku hizi AFYA sio Huduma tena ni BIASHARA, wife anafanya kazi hospitali na hapo kituoni kwao wagonjwa wanaitwa wateja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…