Inasikitisha sana, Wajerumani waliipanga Tanga ikapangika 1891. Waswahili zaidi ya miaka 100 mipango miji changamoto

Sijui watu wanavuruga wapi ,kuna hawa wauza viwanja wao mwengi hawajielewi kabisa.
 
Wamekalia ushirikina na nguvu za Giza!
Bure kabisa...
 
Shida si tu maeneo ambayo tumeshaharibu, shida kubwa zaidi hadi sasa watu wanaendelea kujenga kiholela kwenye miji mipya itakayoleta slums za siku za baadae

Hapo ndiyo tatizo la viongozi wetu hawafikirii mbele ,miji mipya wangeweza kucontrol kwa kupima kabla wananchi hawajayafanya slums....Yaani wanasafiri nje lakini hawaoni kabisa wenzao walivyoyapanga majiji yao.
 
Kuna mji wa kale sanaa unaitwa Pompeii miaka takriban 2000 ilopita mara nyingi naangalia documentary zake asee wazungu wana uwezo mkubwa sanaa WA akili ule mji miaka 2000 ilopita ni mzuri sanaa umepangika kuliko miji mingi mikubwa iliyopo Tanzania
 
Narudia

Matatizo yote ya Tanzania yamesababishwa na Nyerere, yule alikuwa Dikteta, hakujali maendeleo bali kuwepo madarakani
Katika miaka 62 ya uhuru, Nyerere katawala kwa miaka 24 tu. Miaka 38 tumekuwa na Marais wengine. Nini kimewazuia kurekebisha makosa ya Nyerere?

Please HIMARS tumia kichwa chako vizuri isijekuwa ni bustani ya nywele tu
 
Wapangamiji WOTE wizara ya Ardhi wana mentality ya vijijini kwao.
Kwanza hiyo mentality ipigwe msaada.
Pili achia Tanga ya 1890s, wajerumani baada ya uhuru, 1963 hadi '67, walisaidia sana kuondoa slums jijini DSM na kuanzisha National Housing.
Katika Slums eradicating sehemu za Keko, Temeke, Kinondoni na Magomeni zilipangwa upya kwa barabara panda na nyumba wenye nafasi.
Viwanja vidogo ilikuwa around 30x30m.
Lakini wameumia wataalam wa mipangomiji wa Chuo cha Ardhi, ambao bado wana mentality ya vijijini, sasa tunaona misongamano ya Sinza na Mwenge.
Hata Mbezi yenyewe haijapangwa na kwa mshangao mkubwa wanaweza na Industrial Area(COTEX) sehemu ya kuishi watu, tena prime area kama Mbezi Beach.

Tatizo kubwa la hawa wapangaji miji yetu ni kwamba wanajenga viploti vingi vidogo vidogo ile waviuze kibinadamu.
Kijijini mentality.
 
Aisee!!
 
Kupanga miji kuna faida sana sema serikali sijui kwanini aitilii maananani!

Miji ya marekani ingekuwa haijapangwa biashara km amazon ingepata tabu sana kukua na kufikia hapo ilipo.
 
Kupanga miji kuna faida sana sema serikali sijui kwanini aitilii maananani!

Miji ya marekani ingekuwa haijapangwa biashara km amazon ingepata tabu sana kukua na kufikia hapo ilipo.

Very true, hata hawa wanaofanya delivery waliopo moja ya changamoto zao ni hawezi kufika sehemu husika bila kupiga simu kadhaa za kupata maelekezo..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…