Inasikitisha sana, Wajerumani waliipanga Tanga ikapangika 1891. Waswahili zaidi ya miaka 100 mipango miji changamoto

Inasikitisha sana, Wajerumani waliipanga Tanga ikapangika 1891. Waswahili zaidi ya miaka 100 mipango miji changamoto

Sijui watu wanavuruga wapi ,kuna hawa wauza viwanja wao mwengi hawajielewi kabisa.
 
Mji wa Tanga ulijengeka kwa haraka baada ya kutua mjerumani na moja ya kitu alichoacha alama kwenye mji wa Tanga ni kupanga mji kwa barabara 21. Miaka kadhaa nyuma nilifanikiwa kuishi kwenye mji huu kwa siku chache wakati huo google maps ndio inaanza kuwa maarufu nchini.

Pamoja kwamba wenyeji wa Tanga walikuwa wakarimu sana kumuelekeza mtu sehemu anayokwenda, nilipenda sana kutumia ramani ya kwenye simu, kama kitu kipo kwenye ramani hakika utafika vizuri bila kuzunguka zunguka

Miaka zaidi ya 100 sasa, pamoja na kuwa tunacho chuo cha Ardhi na kila mwaka kinatoa graduates, wengine wako nyumbani bila shughuli za kufanya wakati miji mingi mipya inaota kama uyoga nchini tena kiholela mpaka kukosekana njia za kufika.

Maeneo yanakinai kuyaona machoni hata ikitokea dharura kufika baadhi ya sehemu ni changamoto.

Yaani tunashindwa kufanya kitu wenzetu walichoweza miaka 100 iliyopita pamoja na maendeleo makubwa ya teknolojia kwenye namna na vifaa vya kufanya kazi hiyo ya kupanga mji.

Nini kimetushinda sisi waswahili kupanga miji yetu?

View attachment 2733112
Mji wa Tanga​
Wamekalia ushirikina na nguvu za Giza!
Bure kabisa...
 
Shida si tu maeneo ambayo tumeshaharibu, shida kubwa zaidi hadi sasa watu wanaendelea kujenga kiholela kwenye miji mipya itakayoleta slums za siku za baadae

Hapo ndiyo tatizo la viongozi wetu hawafikirii mbele ,miji mipya wangeweza kucontrol kwa kupima kabla wananchi hawajayafanya slums....Yaani wanasafiri nje lakini hawaoni kabisa wenzao walivyoyapanga majiji yao.
 
Kuna mji wa kale sanaa unaitwa Pompeii miaka takriban 2000 ilopita mara nyingi naangalia documentary zake asee wazungu wana uwezo mkubwa sanaa WA akili ule mji miaka 2000 ilopita ni mzuri sanaa umepangika kuliko miji mingi mikubwa iliyopo Tanzania
 
Narudia

Matatizo yote ya Tanzania yamesababishwa na Nyerere, yule alikuwa Dikteta, hakujali maendeleo bali kuwepo madarakani
Katika miaka 62 ya uhuru, Nyerere katawala kwa miaka 24 tu. Miaka 38 tumekuwa na Marais wengine. Nini kimewazuia kurekebisha makosa ya Nyerere?

Please HIMARS tumia kichwa chako vizuri isijekuwa ni bustani ya nywele tu
 
Mji wa Tanga ulijengeka kwa haraka baada ya kutua mjerumani na moja ya kitu alichoacha alama kwenye mji wa Tanga ni kupanga mji kwa barabara 21. Miaka kadhaa nyuma nilifanikiwa kuishi kwenye mji huu kwa siku chache wakati huo google maps ndio inaanza kuwa maarufu nchini.

Pamoja kwamba wenyeji wa Tanga walikuwa wakarimu sana kumuelekeza mtu sehemu anayokwenda, nilipenda sana kutumia ramani ya kwenye simu, kama kitu kipo kwenye ramani hakika utafika vizuri bila kuzunguka zunguka

Miaka zaidi ya 100 sasa, pamoja na kuwa tunacho chuo cha Ardhi na kila mwaka kinatoa graduates, wengine wako nyumbani bila shughuli za kufanya wakati miji mingi mipya inaota kama uyoga nchini tena kiholela mpaka kukosekana njia za kufika.

Maeneo yanakinai kuyaona machoni hata ikitokea dharura kufika baadhi ya sehemu ni changamoto.

Yaani tunashindwa kufanya kitu wenzetu walichoweza miaka 100 iliyopita pamoja na maendeleo makubwa ya teknolojia kwenye namna na vifaa vya kufanya kazi hiyo ya kupanga mji.

Nini kimetushinda sisi waswahili kupanga miji yetu?

View attachment 2733112
Mji wa Tanga​
Wapangamiji WOTE wizara ya Ardhi wana mentality ya vijijini kwao.
Kwanza hiyo mentality ipigwe msaada.
Pili achia Tanga ya 1890s, wajerumani baada ya uhuru, 1963 hadi '67, walisaidia sana kuondoa slums jijini DSM na kuanzisha National Housing.
Katika Slums eradicating sehemu za Keko, Temeke, Kinondoni na Magomeni zilipangwa upya kwa barabara panda na nyumba wenye nafasi.
Viwanja vidogo ilikuwa around 30x30m.
Lakini wameumia wataalam wa mipangomiji wa Chuo cha Ardhi, ambao bado wana mentality ya vijijini, sasa tunaona misongamano ya Sinza na Mwenge.
Hata Mbezi yenyewe haijapangwa na kwa mshangao mkubwa wanaweza na Industrial Area(COTEX) sehemu ya kuishi watu, tena prime area kama Mbezi Beach.

Tatizo kubwa la hawa wapangaji miji yetu ni kwamba wanajenga viploti vingi vidogo vidogo ile waviuze kibinadamu.
Kijijini mentality.
 
Nakazia tena!! Mwafrika hana uwezo wa kujiletea maendeleo ya kiuchumi, kisiasa, kijamiii nk!! Hana mark my words!! Mwafrika anapaswa kusimamia tena Kwa viboko kama walivyofanya wajerumani!!

Fikiria Leo Karne ya 21 mwafrika kufanya uchaguzi huru tuu hawezi!! Sasa unategemea ataweza nini!! Yaani Kwa kifupi sisi ni hovyo.
Aisee!!
 
TZ ni ubinafsi ilitakiwa Majiji yote makubwa waondoe Slums, wawalipe watu watanue barabara, wawalipe watu then majiji yote 100% ardhi iwe imepimwa....Wakifanya hivyo watawatendea haki vitukuu na vilembwe wetu.

Vijiji vyote viwe tayari vimepimwa kwa 100% kusiwe na slums tena in the future, waweke fungu waache ubinafsi.
Kupanga miji kuna faida sana sema serikali sijui kwanini aitilii maananani!

Miji ya marekani ingekuwa haijapangwa biashara km amazon ingepata tabu sana kukua na kufikia hapo ilipo.
 
Kupanga miji kuna faida sana sema serikali sijui kwanini aitilii maananani!

Miji ya marekani ingekuwa haijapangwa biashara km amazon ingepata tabu sana kukua na kufikia hapo ilipo.

Very true, hata hawa wanaofanya delivery waliopo moja ya changamoto zao ni hawezi kufika sehemu husika bila kupiga simu kadhaa za kupata maelekezo..
 
Back
Top Bottom