Inasikitisha Spika Tulia kujifanya hajui kinachoendelea Kariakoo

Inasikitisha Spika Tulia kujifanya hajui kinachoendelea Kariakoo

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Salaam Ndugu zanu,

Bunge linaendela muda huu, mgomo wa kariakoo unaendela muda huu lakini Spika analetewa hoja hii mezani anajifanya kama hajui kinachoendelea.

Kwamba Spika anashindwa kutazama hata vyombo vya habari kujua nini kinaendelea? Eti anadai anataka ajiridhishe kama ni kweli au la?

Kuna kitu anakijua kuhusu huo mgomo anakificha?

Kwanini halipi jambo hili uzito kuacha lijadiliwe na utatuzi upatikane?

Hili suala linakwaza sana.

Pia Soma
- News Alert: - Mgomo mkubwa Soko la Kariakoo: Maduka yamefungwa, Mei 15, 2023
 
Hakuna waziri wala Speaker anayeweza kuelewa, wao shopping zao wanafanya Dubai na Turkey huko kariakoo ni kwa Walaumiwa/walalahoi sio kwa Waheshimiwa/walala hai
 
Salaam Ndugu zanu,

Bunge linaendela muda huu, mgomo wa kariakoo unaendela muda huu lakini Spika analetewa hoja hii mezani anajifanya kama hajui kinachoendelea.

Kwamba Spika anashindwa kutazama hata vyombo vya habari kujua nini kinaendelea?

Kuna kitu anakijua kuhusu huo mgomo anakificha?

Kwanini halipi jambo hili uzito kuacha lijadiliwe na utatuzi upatikane?

Hili suala linakwaza sana.
Sio jukumu la Spika kujua migomo inayoendelea tena mgomo wenyewe umetokea asubuhi na hadi sasa bado ni asubuhi. Muda mgomo unaanza yawezekana alikuwa anajiandaa kuingia bungeni.

Labda kama kuna hoja nyingine zaidi ya hii
 
Hakuna waziri wala Speaker anayeweza kuelewa, wao shopping zao wanafanya Dubai na Turkey huko kariakoo ni kwa Walaumiwa/walalahoi sio kwa Waheshimiwa/walala hai
Kabisa yaani, wanachukulia mambo poa sana. Hawajui ni kwa kiasi gani watu wanaathirika.

Yeye kama kiongozi wa Bunge alipaswa alipe jambo hili uzito
 
Anasubiri barua rasmi yenye nembo ya taifa na mwenye kutoa hiyo barua wamekataa kwamba hakuna mgomo.

Baada ya hapo kipindi cha "BUNGE LIVE" kimetolewa hewani na mwanzilishi wa kuondoa hiki kipindi ndo yule yule wa "Mungu kaamua ugomvi"
 
Wacha tusubiri tuone.
 
Lazima tujue aina hii ya mgomo serekali haiwezi kuushughulikia kwa haraka na kwa hofu kwa sababu hauleti maumivu ya haraka kwake na kwa wananchi, kwa hiyo wanaweza kuwaringia hata wiki nzima ''huitwa delaying technique''.

Hapo Nini kitatokea, wafanyabiashara wenyewe kwa wenyewe wanaweza kujikuta wanageukana na wengine kuanza kuendelea na biashara.
 
Wewe ni Mbunge na Mdau wa huu Mgomo...unalalamika sana...Kwani Dar ni Kariakoo tu...Gomeni mazima na mchome kabisa Maduka na sisi Zimamoto hatutakuja
 
Wewe ni Mbunge na Mdau wa huu Mgomo...unalalamika sana...Kwani Dar ni Kariakoo tu...Gomeni mazima na mchome kabisa Maduka na sisi Zimamoto hatutakuja

Hamna kitu unachokijua wewe.

Kwanza inaonekana hata dar hujawai kufika.

Kariakoo ndio kila kitu nchi nzima kwenye swala la biashara Maduka karibu yote njee ya kariakoo yanategemea kununua mali zote kariakoo.

Ngoja tugome wiki nzima uone hata izo gari za viongozi wenu mafisadi zitafanyiwa service na spare gani
Madawa yote jumla yanapatikana kariakoo
 
Kodi everywhere alafu CAG anasema hela zinaliwa sasa Kuna haja gani ya hizo kodi.
 
Nchi hii ni kubwa si rahisi ukajua kila kinachotokea nchini, wengne tunajua matukio kwa kupewa taarifa Kama ambavyo speaker wa bunge amahabarishwa na wanaojua kinachoendelea. Kwa hyo si ajabu kwa mtu kutokujua kinachoendelea
 
Back
Top Bottom