Be calm
JF-Expert Member
- May 20, 2023
- 3,766
- 8,959
Ukimwona adui anafuraha juu ya changamoto aliyokusababishia unaumia lakini adui huyohuyo akipata matatizo unaumia moyo hupendi kumwona hana furaha
Ukimwona mwanayanga anafuraha Simba ikifungwa unaumia, wanayanga wakifungwa ukiona wanaumia nawe unaumia moyo kwanini hawana furaha, kwanini wamefingwa.
Mapungufu ya Rais Samia katika utawala wake nawe yanakuumiza, lakini anamazuri yake kalifanyia taifa. Ukiona wananchi wanamtukana mtandaoni unaumia, unamhurumia huyu mwanamke, ila watu wakipotea au kuuawa na wasiojulikana moyo ndiyo unaumia kabisaaa, wapinzani wakibanwa kisiasa ndiyo moyo unaumia sana.
Ukiona mtu yeyote anaangaika na maisha kiuchumi unaumia, tena umwone mwanaume umri umeenda afu anauza karanga za miamia barabarani ndiyo nalia kabisa.
Yaani ni kama sitaki mtu apate shida au huzuni ya moyo au nafsi yake iteseke.
Msibani ndiyo nalia kama ng'ombe hata kama aliyekufa si ndugu yangu. Mwenyezi Mungu atusaidie sana, hii dunia Ina maumivu mengi kuliko furaha.
Nafurahi sana nikisikia mtu anacheka sehemu haswa mwanaume maana ni Kama wanaume furaha yao ni ya muda mfupi sana, wanakufa na vitu moyoni.
NB: Usikikumbatie kitu chochote kinachokunyima furaha, maisha haya tunaishi muda mfupi sana.
Mbarikiwe watu wa Mungu🙏