Inatisha: Tatizo la kulala na kushindwa kuamka japokuwa macho yamefumbua na akili ipo sawa sawa!!

Inatisha: Tatizo la kulala na kushindwa kuamka japokuwa macho yamefumbua na akili ipo sawa sawa!!

Kiukweli mimi nikilalari mgongo, huwa naota ndoto hatari sana, mara naota nimekufa, mara naota nimepigiliwa msalaba mgongoni, mara nipo mlimani kileleni nimeachiliwa kutoka huko kileleni na shuka chini, hapa kwenye kuamka sasa huwa nachukua hata zaidi ya dakika kumi huku nahangaika kuamka.

Yani nikilala kutazama juu, ndoto zangu ni kuzimu tuhhh,sijawahi ota la maaana hata siku moja
 
Hii hali inanipata sana mimi. Mwanzo nilikuwa nahisi sasa malaika mtoa roho Anafanya kazi yake[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]naogopa balaa

Ila kwa sasa huwa natulia tuli huku naomba dua tu basi baada ya muda narudi kwenye hali ya kawaida
Leo usiku tu imenikuta yaan imekua sehem ya maisha yangu na silali kimgongo mgongo.
 
Hiyo ni stage tuu ya mwenda astral wala mleta mada asiwatishe cjui umepalalize ww tulia pale ondoa hofu jua ipo kiroho alaf jaribu kuamka kiroho utaona mwili unabak pale kitandan na ww unaenda kutalii sehem mbali mbali za dunia

note kwa mara ya kwanza utasikia maumivu flan ya ganz lakin ukishazoea yataisha
 
Hali hiyo ipo ila mtoa mada amepotosha mengi, tatizo hili limewahi kuelezwa hapa miaka kama 4 iliyopita pekueni nyuzi za nyuma mtakuta likielezwa kitaalamu na namna ya ku overcome.
 
Kwa kipindi kirefu sana tangu nipo shule ya secondary nilishawahi kukumbwa na tatizo kama hili maranyingi sana najua na wewe unaesoma huu Uzi nadhani umeshawahi kupatwa na tatizo kama hili yaani unapo amka asubuhi ama usiku unashindwa kabisa Kunyanyuka na sio kwamba ni ndoto Bali unaji elewa kabisa na unaona kila shughuli zinavyo fanyika kwa wakati huo
Huu sio ugonjwa Bali ni hali inayo itwa kitaalamu "sleeping paralysis "
Hii hali ikikupata maranyingi utapata hofu kubwa sana na utahisi kama jinamizi hivi litakutokea baada ya mfupi lakini sio mambo ya kichawi wala kiroho
Na hii hali huondoka baada ya kama dakika 2-3

Hii hali husababishwa na nini?
Ina sababishwa na unapo lala katika style ya kimgongomgongo gani kulalia mgongo wako na USO wako kutazama juu wakati ume lala ni hatari sana hii kitu.
Ndio maana tuna shauriwa tulalie ubavu wetu Wa kulia.(kama waislamu wanavyo lala)

Je unapokumbwa na tatizo kama hili unatakiwa ufanye nini ilikuliondoa
Kukaa dakika 2-3 bila kunyanyuka wala kuongea na
Ukijaribu kuongea ulimi unakua mzito balaa
Yaani kama unasema baba utaishia kusema aahh
Tena sauti ya chini kabisa na kadri unavyo zidi kuongea ndivo unavyo zidi kuongea vitu visivyo eleweka ndugu wasomaji hii sio ndoto Bali ni real life situation natamani sana kupata MTU hata mmoja ambaye amewahi kukumbwa na tatizo kama hili ili awape mrejesho jinsi inavyo tisha.

==>ili kuondoa tatizo kama hili kwanza fuata hatua zifuatazo

(1) jaribu Ku kunjua mguu wako na mikono yako najua ni kazi ngumu sana ila jitahidi na mwisho wa Siku Lita ondoka kabisa.

(2)kunja USO wako kama MTU alie lamba ndimu
Hii itasaidia pia

(3)usipige kelele kwani utadhidisha uwoga zaidi kwani kelele utakayo ipiga hata MTU akiweka sikio lake mdomoni kwako hatasikia kitu.

Pia omba kwa mungu ili akuondolee tatizo hili hatari

Jinsi ya kuepuka kupatwa na tatizo kama hili
Acha kulalia mgingo wako
Asanteni wakuu
nmekutana nayo mara nyingi hasa nikilala hvyo cha ajabu kuna siku nikawa naomba niachiwe ndio ikabana zaidi yaan
 
Hii kitu hunikumba mara nyingi yan af kila nikirudi kwenye ufahamu kweli najikuta nimelalia mgongo

Ni hali ya kuogovya sana maana ata upigeje kelele usikiki mara nyingi inabid kuomba kwa imani sana uwapo kwenye hyo hali
 
Dawa ya hali hii ni kusali kabla na baada ya kuamka.kwa wale wakristo safi wanajua wakiwa ktk hali hiyo roho mtakatifu huwapa nguvu ya kukemea bila hata wao kujishughulisha sana ghafla hali hiyo inatoweka.
 
Mimi ni kilalia mgongo huwa sipati usingizi kabisa yaani naweza kesha sijui kwanini
 
Hili wala sio tatizo ni hali ya kawaida na sio lazima ulale kimgongo ndo ikutokee
Ikikutokea wala usipanic tulia tu ndani ya sekunde 10-15 unakua poa tu..
Binafsi ishanitokea sana

Cc mshana jr
Cc rakims
 
Hii imenitokea juzi tuu, nilikuwa nnasali nnahisi my rib ananisikia, ninakumbuka kumuita kabisa na kuongea nae cha ajabu ninakuja kumuuliza asubuhi
 
Unajua MUNGU alivyotuumba alijua tu itafika kipindi tutamkana(hatutatambua uwepo wake) hivyo ilibidi atuwekee vitu/matukio ambayo ni lazima utatambua uwepo wake...(lazima utatambua kuwa Mungu yupo)
 
au unatoka, unaona mwili wako umelala pale, unaona watu wanapita ukitaka kurudi kwenye mwili wako ndipo mtihani unapoanza...ipo hii ya kujiona una uwezo wa kupaa hii hunikuta sana, naweza ingia ktk mishe nikafanikisha michongo flani, nikiwa napaa, afu ukijastuka uko kwa sofa tena mchana labda ama usiku, ila sasa nikifuatilia kama itatokea nikakumbuka kilichotokea wakati niko katika ile hali basi mambo huwa supa...mimi pia nimehangaika kuhusu hili lakini bado sijapata jibu la kuridhisha
hiyo ya kupaa hata mimi hunitokea sana,
yaani badala ya kutembea,unapaa at will,huku ukiwa upright
 
au unatoka, unaona mwili wako umelala pale, unaona watu wanapita ukitaka kurudi kwenye mwili wako ndipo mtihani unapoanza...ipo hii ya kujiona una uwezo wa kupaa hii hunikuta sana, naweza ingia ktk mishe nikafanikisha michongo flani, nikiwa napaa, afu ukijastuka uko kwa sofa tena mchana labda ama usiku, ila sasa nikifuatilia kama itatokea nikakumbuka kilichotokea wakati niko katika ile hali basi mambo huwa supa...mimi pia nimehangaika kuhusu hili lakini bado sijapata jibu la kuridhisha
hiyo ya kupaa hata mimi hunitokea sana,
yaani badala ya kutembea,unapaa at will,huku ukiwa upright
 
Back
Top Bottom