Inatisha: Tatizo la kulala na kushindwa kuamka japokuwa macho yamefumbua na akili ipo sawa sawa!!

Inatisha: Tatizo la kulala na kushindwa kuamka japokuwa macho yamefumbua na akili ipo sawa sawa!!

Ibrahim augustine

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2017
Posts
428
Reaction score
576
Kwa kipindi kirefu sana tangu nipo shule ya secondary nilishawahi kukumbwa na tatizo kama hili maranyingi sana najua na wewe unaesoma huu Uzi nadhani umeshawahi kupatwa na tatizo kama hili yaani unapo amka asubuhi ama usiku unashindwa kabisa Kunyanyuka na sio kwamba ni ndoto Bali unaji elewa kabisa na unaona kila shughuli zinavyo fanyika kwa wakati huo
Huu sio ugonjwa Bali ni hali inayo itwa kitaalamu "sleeping paralysis "
Hii hali ikikupata maranyingi utapata hofu kubwa sana na utahisi kama jinamizi hivi litakutokea baada ya mfupi lakini sio mambo ya kichawi wala kiroho
Na hii hali huondoka baada ya kama dakika 2-3

Hii hali husababishwa na nini?
Ina sababishwa na unapo lala katika style ya kimgongomgongo gani kulalia mgongo wako na USO wako kutazama juu wakati ume lala ni hatari sana hii kitu.
Ndio maana tuna shauriwa tulalie ubavu wetu Wa kulia.(kama waislamu wanavyo lala)

Je unapokumbwa na tatizo kama hili unatakiwa ufanye nini ilikuliondoa
Kukaa dakika 2-3 bila kunyanyuka wala kuongea na
Ukijaribu kuongea ulimi unakua mzito balaa
Yaani kama unasema baba utaishia kusema aahh
Tena sauti ya chini kabisa na kadri unavyo zidi kuongea ndivo unavyo zidi kuongea vitu visivyo eleweka ndugu wasomaji hii sio ndoto Bali ni real life situation natamani sana kupata MTU hata mmoja ambaye amewahi kukumbwa na tatizo kama hili ili awape mrejesho jinsi inavyo tisha.

==>ili kuondoa tatizo kama hili kwanza fuata hatua zifuatazo

(1) jaribu Ku kunjua mguu wako na mikono yako najua ni kazi ngumu sana ila jitahidi na mwisho wa Siku Lita ondoka kabisa.

(2)kunja USO wako kama MTU alie lamba ndimu
Hii itasaidia pia

(3)usipige kelele kwani utadhidisha uwoga zaidi kwani kelele utakayo ipiga hata MTU akiweka sikio lake mdomoni kwako hatasikia kitu.

Pia omba kwa mungu ili akuondolee tatizo hili hatari

Jinsi ya kuepuka kupatwa na tatizo kama hili
Acha kulalia mgingo wako
Asanteni wakuu
 
Hiyo kitu ipo,imenitokeaga kama mara nne hivi na most of the time nakuwa sijasali,mara nyingi ninaepukagaga kwa kusali tu ila ni kitu kinachotisha na kuogopesha sana.mwili unakua km umepigwa shoti
Mkuu yaani inatisha sana hii hali unakua kama ume
paralyse kwa muda
 
au unatoka, unaona mwili wako umelala pale, unaona watu wanapita ukitaka kurudi kwenye mwili wako ndipo mtihani unapoanza...ipo hii ya kujiona una uwezo wa kupaa hii hunikuta sana, naweza ingia ktk mishe nikafanikisha michongo flani, nikiwa napaa, afu ukijastuka uko kwa sofa tena mchana labda ama usiku, ila sasa nikifuatilia kama itatokea nikakumbuka kilichotokea wakati niko katika ile hali basi mambo huwa supa...mimi pia nimehangaika kuhusu hili lakini bado sijapata jibu la kuridhisha
 
Hii kitu ilinikutaga nikiwa A level aisee nilikuwa nachanganyikiea nahisi ndo nimekufa nikiwa hai daah hatari sana usiombe ikukute jamani isikieni tu na ishanitokea zaid ya mara 5.. Na ni kweli kipindi hichi nilikuwa nalalia mgongo
 
Hii kitu ilinikutaga nikiwa A level aisee nilikuwa nachanganyikiea nahisi ndo nimekufa nikiwa hai daah hatari sana usiombe ikukute jamani isikieni tu na ishanitokea zaid ya mara 5.. Na ni kweli kipindi hichi nilikuwa nalalia mgongo
Pole sana
 
Hilo huwa ni jinamizi au pale wachawi wanapokuwekea dawa zao lakini ulikuwa hujalala kabisa.

Ni kama vile umepewa dawa ya nusu kaputi lakini bado hujazimika.

Wasomi wengi wanapenda kujipa moyo kwa kigezo cha sayansi.

Fanya hili zoezi: Amua kabisa kuacha dhambi na umkabidhi Mungu maisha yako uone kama utapata hiyo shida. Baada ya hapo nenda ukazini uone usiku wake itakavyokuwa.
 
Hilo sio tatizo bali ni stage ya kutoka out kiroho huku ukiwa unajitambua
Kwa lugha nyepesi ni stage muhimu sana kuelekea kutoka nje ya mwili(astral projection)
Ni nzuri sana ukiweza kuicontral
Jiongeze uweze kutalii mahali popote duniani na hata ulimwenguni
 
Ilisha nitokea nikaambiwa nimekabwa na jinamizi.
Niliambiwa nyumba niliyoishi ilikuwa na mazindiko ya kishirikina,eti majini yao yamenikalia
 
Hii hali inanipata sana mimi. Mwanzo nilikuwa nahisi sasa malaika mtoa roho Anafanya kazi yake[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]naogopa balaa

Ila kwa sasa huwa natulia tuli huku naomba dua tu basi baada ya muda narudi kwenye hali ya kawaida
 
Hii hali inanipata sana mimi. Mwanzo nilikuwa nahisi sasa malaika mtoa roho Anafanya kazi yake[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]naogopa balaa

Ila kwa sasa huwa natulia tuli huku naomba dua tu basi baada ya muda narudi kwenye hali ya kawaida
Hahaha umenichekesha sana mkuu
Ina onekana una lalia mgongo wako
 
Hii huwa inampata ndugu yangu, Unaweza kuta yupo macho na anakuona lakn hawezi fanya kitu mara nyingi lazma umshtue ndo anaamka
 
Ukiwa usingizini kisha ukapata hofu au kuota ndoto mbaya kuna fluid inayo deploy kutoka katika ubongo.ili usijidhuru au kudhurika!sio tatizo infact lakini ni defence mechanism ikiwa kazini kwake
 
Back
Top Bottom