Inatubidi tuende na Dunia inavyotaka. Hivi Mungu yupo kweli?

Inatubidi tuende na Dunia inavyotaka. Hivi Mungu yupo kweli?

Lazima ujinga unao uandika tuukemeee!
Tatizo lako hujui kuandika.

Kizibo mwenyewe Bwege nini.
Mdau kila mada mtambuko humu JF wewe unaita ujinga.Unajua maana ya neno ujinga na matumizi ya neno hilo????????Au ubongo wako hauwezi kuhimili mada mtambuko?????.Na kingine kutumia maneno yasiyo na staha kama "Bwege au Kizibo""ni mambo ya watoto wa chuo,watu wazima mnakua na staha kwa kujibu hoja kwa hoja sio kujibu hoja kwa matusi na lugha za kejeli.
 
Mdau kila mada mtambuko humu JF wewe unaita ujinga.Unajua maana ya neno ujinga na matumizi ya neno hilo????????Au ubongo wako hauwezi kuhimili mada mtambuko?????.Na kingine kutumia maneno yasiyo na staha kama "Bwege au Kizibo""ni msmbo ya watoto wa chuo,watu wazima mnakua na staha kwa kujibu hoja kwa hoja sio kujibu hoja kwa matusi na lugha za kejeli.
Sawa Nashukuru Nimekuelewa
 
Wabongo tunapenda sana mambo ya umbea umbea kwa mfano kuna jukwaa la Historia mimi naliita la Mohamed Said mzee wa watu anapost vitu ambavyo hata mtaani hujawahi kuviskia lakini watu hata kuperuzi tu hola.
Mzee Said anaposti anayotaka yeye ila ukimuomba maelezo ya uhakika anakataa,yeye kila kitu ananasibisha na uislamu mpaka Uhuru wa Tanganyika🤣🤣🤣😂😂😂😊.Ndio maana baadhi ya watu hawaperuzi mada zake sababu kuna udini uliokithiri ndani ya mada zake
 
Wakati mwingie naperuzi tu hata miezi na sicomment chochote naona hata wale miamba waliokuwa wanatoa nondo watakuwa nao wana Id's nyingine kwa ajali ya kuchangia mada za kiwaki ili kutunza heshima zao.
Hakuna mada za""Kiwaki""mkuu.Bali kuna mada pendwa mfano""Kula tunda kimasihara""na mada fikirishi ambazo hazipendwi sana mkuu.Mada ni mada ila mapokeo ndio yanatofautiana mkuu.
 
Unajua haya mambo yanaanzia ngazi ya familia. Malezi yanachangia sana mwenendo huu wa sasa wa vijana na mabinti kuvutiwa na story za upumbavu na ujinga kuliko mambo ya msingi.

Watu wanatoka kwenye familia hazina upendo. Wanatoka familia ambazo hazina maadili, wanatoka familia ambazo baba sio kiongozi ila mama, wanatoka familia ambazo hawana utaratibu wa ibada ama kufanya sala ile kifamilia, wanatoka familia ambazo kila mtoto anakuwa kwa mfumo wa autopilot unategemea nini kwenye upande wa jamii?

So hayo unayoyashuhudia ni matokeo ya structure ya malezi ya sasa yameharibu ustawi wa jamii.

Sasa hivi unapanda daladala unakutana na mwanafunzi wa miaka 15 anamuona mzee anaingia kwenye daladala anakausha kwenye siti sababu amelipia na nani kamfunza hiyo jeuri ni mama yake alipomwambia kuwa na yeye pia ni mwanadamu so akipanda daladala alipie nauli ya mtu mzima na asipishe mtu wa aina yoyot, kizazi cha akina mama type ya akina 'giggy money' hao wanavyolea watoto wao.

Kuna siku narejea zangu nyumbani kuna sehemu napita nikakutana vibinti nadhani ni darasa la tano kama sio la nne. Vimebebelea mabegi yamejazwa madaftari lundo. Sasa nikawasalimia na kuwauliza nyie "watoto humo kwenye mabegi m'mebebelea nini mbona vinaonekana vizito sana hamchoki na kuumia migongo", wale watoto hawakunijibu wakawa kimya kama viziwi. Nikawauliza tena hamjaniskia au nyie watoto mbona mpo kimya. Hawakujibu kitu naniliwauliza zaidi ya mara tatu hadi m'moja akanijibu "tumekatazwa kuongea na watu wazima wanabaka watoto" halafu wenzake wakacheka.

Dah nikaishiwa pozi pale pale nikaendelea na safari yangu sikujibu kitu. Nikasema hii jamii itakuja kutafuta watu wanaojielewa kwa tochi sana miaka ijayo na hawatawapata kama ndio tunawalea watoto namna hii.
 
Back
Top Bottom