Inauma sana; Mapenzi yaondoa uhai wa Francis Ngolle aliyezaliwa mwaka 1990

Inauma sana; Mapenzi yaondoa uhai wa Francis Ngolle aliyezaliwa mwaka 1990

Inahudhunisha kwa kweli,pole sana wafiwa

Sent from my TECNO-N8 using JamiiForums mobile app
 
Poleni sana wafiwa

Tuliobaki tunajifunza nini kwenye ili: Inabidi kama unaenda sehemu uwe unatoa taarifa kabla maana inaonyesha jamaa kama alienda kwa surprise bila kumtaarifu mchumba wake na mwisho wake amekutana na alichokikuta.

Wazee wetu zamani walikuwa wakirudi nyumbani toka safari (Enzi hizo simu hamna) walikuwa wanawapa vijana mizigo wapeleke nyumbani huku wao wakinyuti vijiwe vya kahawa kupoteza muda ili kuepusha mafumanizi kama haya.
 
rip roommate wangu ,niliacha shughuli zangu zote tangu siku ya kwanza ulipofariki nikafunga safari hadi mbagala kisimani kwa daud, juzi usiku nilikwenda airport kuupokea mwili wako toka mwanza jana nimekudress mwili wako pale temeke hospitali ,nashindwa hata kuendelea...... ila jaman kwanini sababu ya kifochake inapotoshwa potoshwa sana jamani roho inaniuma sana
 

Attachments

  • IMG_20170712_152229.jpg
    IMG_20170712_152229.jpg
    196.3 KB · Views: 72
daah wanawake wametofautiana kuna wawerevu na mashetani huyo dada atakuwa shetani na nafsi ya marehemu itamtesa kwakuwa amekufa na dukuduku


sure ! hatakaa salama tena maishan mwake damu itamlilia had anaingia kaburini! kuna watu jaman wana roho kavuu!
 
Anaandika Respicius Francis
________________________________________

Mapenzi yaondoa uhai wa Francis Ngolle aliyezaliwa mwaka 1990.

[HASHTAG]#Huyu[/HASHTAG] kijana namfahamu sana na tumewahi kukutana nae mara tatu mara ya kwanza nilikutana nae nyumbani kwao na mara mbili nikutana nae mtaani.

[HASHTAG]#Juzi[/HASHTAG] nilipata habari kuwa kijana mmoja kutoka maeneo ya mtaani kwetu ameuawa huko Mwanza alipoenda kumtembelea mchumba wake huko Mwanza akitokea Dar Es Salaam lakni kwa bahati mbaya alimkuta mchumba akiwa na mwanaume mwingine chumbani, Inasemekana huyo mwanaume aliyemkuta chumbani akiwa na mchumba wake ni askari kwahiyo mapambano yalianza ambapo mwanamke alikimbia na kuacha wanaume wakipigana.

[HASHTAG]#Mwanamke[/HASHTAG] aliporudi alikuta Francis Ngolle tayari amepoteza maisha ,Sasa haijulikani alipewa kipigo cha aina gani mpaka kusababisha kupoteza uhai.

[HASHTAG]#Lakini[/HASHTAG] cha kusikitisha sana mchumba wa Francis Ngolle mimi binafsi mfahamu sana na mara nyingi tumewahi kukutana kwenye kikundi chetu cha dini cha {VIWAWA] enzi hizo kabla ya huyu dada ajaenda kikazi mwanza lakini sikujua kabisa kama wana uchumba na FRANCIS NGOLLE

[HASHTAG]#Lakini[/HASHTAG] cha kusikitisha zaidi Francis Ngolle na huyu mchumba wake hapa dar Es Salaam wanaishi karibu sana siyo mbali sana kwa lugha nyingine wanaishi karibu na mimi pia.

[HASHTAG]#Francis[/HASHTAG] Ngolle alikuwa tayari amejitamburisha kwa wazazi wa mchumba wake kwahiyo wazazi wa pande zote mbilli walikuwa wanatambua pia.

[HASHTAG]#Kinachotia[/HASHTAG] simanzi zaidi wazazi Francis Ngolle na Mchumba wake hapa Dar es Salaam wanasali kanisa moja##

[HASHTAG]#Francis[/HASHTAG] Ngolle bila kujua kama anaenda kupoteza maisha anafunga safari kwenda kwa mchumba wake huko mwanza lakini anakuta mchumba wake ana bwana mwingine chumbani ,Mapambano yanaanza na mwisho wa siku anapoteza maisha.

[HASHTAG]#Muda[/HASHTAG] huu nimetoka msibani hakika ni majonzi makubwa sana nimejaribu kuangalia maiti yake wakati nikitoa heshima za mwisho inaonekana alipigwa sana ,Utafikiri ni mtu aliyepata ajali mbaya.

R.I.P Francis NgolleView attachment 540970
Ana kaka yake anaitwa Tom ngolle yuko madini dom au ni majina tu yamefanana naomba kujuzwa

Sent from my TECNO-J8 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom