Jembemtaji
JF-Expert Member
- Aug 21, 2014
- 1,193
- 926
Huyu jamaa aliuwawa alipomfika Mwanza alimkuta mchumba ake yupo na sakali polisi... Baada ya kuona hayo wanaume hao wawili wakaanza kupigana, na ndipo mwanamke akaamua kukimbia na kuacha ngumi zikiendelea... Polisi akazidiwa akaamua kuita polisi wenzie wawili na ndipo wakampiga hadi kumuua...Mapenzi yaondoa uhai wa Francis Ngolle aliyezaliwa mwaka 1990.
Huyu kijana namfahamu sana na tumewahi kukutana nae mara tatu mara ya kwanza nilikutana nae nyumbani kwao na mara mbili nikutana nae mtaani.
Juzi nilipata habari kuwa kijana mmoja kutoka maeneo ya mtaani kwetu ameuawa huko Mwanza alipoenda kumtebelea mchumba wake huko Mwanza akitokea Dar Es Salaam lakni kwa bahati mbaya alimkuta mchumba akiwa na mwanaume mwingine chumbani, Inasemekana huyo mwanaume aliyemkuta chumbani akiwa na mchumba wake ni askari kwahiyo mapambano yalianza ambapo mwanamke alikimbia na kuacha wanaume wakipigana.
Mwanamke aliporudi alikuta Francis Ngolle tayari amepoteza maisha ,Sasa haijulikani alipewa kipigo cha aina gani mpaka kusababisha kupoteza uhai .
Lakini cha kusikitisha sana mchumba wa Francis Ngolle mimi binafsi mfahamu sana na mara nyingi tumewahi kukutana kwenye kikundi chetu cha dini cha {VIWAWA] enzi hizo kabla ya huyu dada ajaenda kikazi mwanza lakini sikujua kabisa kama wana uchumba na FRANCIS NGOLLE.
Lakini cha kusikitisha zaidi Francis Ngolle na huyu mchumba wake hapa dar Es Salaam wanaishi karibu sana siyo mbali sana kwa lugha nyingine wanaishi karibu na mimi pia .
Francis Ngolle alikuwa tayari amejitamburisha kwa wazazi wa mchumba wake kwahiyo wazazi wa pande zote mbilli walikuwa wanatambua pia.
Kinachotia simanzi zaidi wazazi Francis Ngolle na Mchumba wake hapa Dar es Salaam wanaishi karibu,wanasali kanisa moja.
Francis Ngolle bila kujua kama anaenda kupoteza maisha anafunga safari kwenda kwa mchumba wake huko mwanza lakini anakuta mchumba wake ana bwana mwingine chumbani ,Mapambano yanaanza na mwisho wa siku anapoteza maisha.
Muda huu nimetoka msibani hakika ni majonzi makubwa sana nimejaribu kuangalia maiti yake wakati nikitoa heshima za mwisho inaonekana alipigwa sana,Utafikiri ni mtu aliyepata ajali mbaya.
R.I.P Francis Ngolle
-mikononyuma-
Funzo kwa walio hai. Tangulia FrancisKwanza mwanamke ambaye mmekutana naye ukubwani unaendeje kwake bila kumtaharifu!
Hiyo kitu siwez fanya hata siku moja!
Poleni kwa msiba.
Hili nilishaliapia miaka mingi iliyopita.....Sorry, lakini lazima niseme tu ukweli... kupigana kisa k.. ni ushamba.
Sent from my SM-T355 using JamiiForums mobile app
Nina muda mrefu sana sijaona jogoo wakipigania kuku jikeUnapigania mwanamke upo karne gani ,.. Aseeh, baada ya wanawake wakupiganie wewe daah anyway R. I. P Francis Ngolle
afu kingne alipigwa na askari wa aina gani je? Kuna hatua zozote za kisheria zimechukuliwa ningependa kujua hayo ndugu.R.I.P Shemeji yangu
Kiukweli inauma sana
Huyu nishemeji yangu kabisa mm nimeoa Dada yake
Sent from my TECNO-C9 using JamiiForums mobile app
[emoji13] [emoji13] [emoji13]Yani mimi mwanamke akinizingua saivi ndio nafurahia, Babu kuna visu vikali hatari...! Unaeza ukaona demu ukasema hivi huyu kashushwa au vipi??! Akizingua dem unatafuta kisu kingne mbona wapo wengi sana
Sent from My GooglePixel using JamiiForums mobile app
Nakumbuka hata mimi mwalimu wangu wa uchumi aliwahi kuniambia "women are like matatuu, if you miss this one hold on you will get another" yaani alimaanisha kuwa wanawake ni kama daladala ukiikosa hii usiangaike kuwa mvumilivu tu utapata nyingine na hatimae utaisahau iliyokupita mwanzo!Nina muda mrefu sana sijaona jogoo wakipigania kuku jike
Hata jogoo walishaacha kupigania mapenzi baada ya kugundua kuku majike ni weeeengi
Daladala ikikupita kituoni usiikimbilie
Subiri nyingine na ukiona daladala zinakuzingua panda bajaji,mwendokasi,bodaboda,tax,uber,treni...
Usafiri mwiiiiiiiingi
Pressure ya nini?
Sent from my SM-N910H using JamiiForums mobile app
Kama kuna mtoto anapewa koti au mzgo autangulize homwazee zamani wakati wanarudi nyumbani wakiwa mbali walikuwa wanakohoa kohoa ili kama kuna mwizi akimbie
Post sent using JamiiForums mobile app