mikononyuma
JF-Expert Member
- Jul 8, 2015
- 641
- 600
Mapenzi yaondoa uhai wa Francis Ngolle aliyezaliwa mwaka 1990.
Huyu kijana namfahamu sana na tumewahi kukutana nae mara tatu mara ya kwanza nilikutana nae nyumbani kwao na mara mbili nikutana nae mtaani.
Juzi nilipata habari kuwa kijana mmoja kutoka maeneo ya mtaani kwetu ameuawa huko Mwanza alipoenda kumtebelea mchumba wake huko Mwanza akitokea Dar Es Salaam lakni kwa bahati mbaya alimkuta mchumba akiwa na mwanaume mwingine chumbani, Inasemekana huyo mwanaume aliyemkuta chumbani akiwa na mchumba wake ni askari kwahiyo mapambano yalianza ambapo mwanamke alikimbia na kuacha wanaume wakipigana.
Mwanamke aliporudi alikuta Francis Ngolle tayari amepoteza maisha ,Sasa haijulikani alipewa kipigo cha aina gani mpaka kusababisha kupoteza uhai .
Lakini cha kusikitisha sana mchumba wa Francis Ngolle mimi binafsi mfahamu sana na mara nyingi tumewahi kukutana kwenye kikundi chetu cha dini cha {VIWAWA] enzi hizo kabla ya huyu dada ajaenda kikazi mwanza lakini sikujua kabisa kama wana uchumba na FRANCIS NGOLLE.
Lakini cha kusikitisha zaidi Francis Ngolle na huyu mchumba wake hapa dar Es Salaam wanaishi karibu sana siyo mbali sana kwa lugha nyingine wanaishi karibu na mimi pia .
Francis Ngolle alikuwa tayari amejitamburisha kwa wazazi wa mchumba wake kwahiyo wazazi wa pande zote mbilli walikuwa wanatambua pia.
Kinachotia simanzi zaidi wazazi Francis Ngolle na Mchumba wake hapa Dar es Salaam wanaishi karibu,wanasali kanisa moja.
Francis Ngolle bila kujua kama anaenda kupoteza maisha anafunga safari kwenda kwa mchumba wake huko mwanza lakini anakuta mchumba wake ana bwana mwingine chumbani ,Mapambano yanaanza na mwisho wa siku anapoteza maisha.
Muda huu nimetoka msibani hakika ni majonzi makubwa sana nimejaribu kuangalia maiti yake wakati nikitoa heshima za mwisho inaonekana alipigwa sana,Utafikiri ni mtu aliyepata ajali mbaya.
R.I.P Francis Ngolle
-mikononyuma-