Uchaguzi 2020 Inauma sana, nasikiliza matokeo hapa nahisi kama roho inataka kutoka

Uchaguzi 2020 Inauma sana, nasikiliza matokeo hapa nahisi kama roho inataka kutoka

Hakuna mahali au wakati wowote nimetoa hoja ya UCHAPA KAZI wa Magufuli bali wewe unakiri hivyo. Basi kweli ni mchapa kazi.

Wagombea walienguliwa kwa sababu hawakukidhi vigezo vya kuteuliwa ikizingatiwa wakiteuliwa na kuchaguliwa ni wawakilishi wa watu. Tumeshuhudia baadhi ya waliochaguliwa kuhama vyama. Na hata kama wangeruhusiwa kushiriki, kwa matokeo ya uchaguzi uliomalizika, yasingebadilika

Mawakala ambao hawakuwa na barua za utambulisho waliruhusiwa kuendelea na usimamizi wakisubiri barua za utambulisho. Lakini barua zilipoletwa zilikuwa za watu tofauti kabisa, ikabidi watimuliwe. Kumbe Mawakala halisi walisusa kwa kuahidiwa malipo baada ya uchaguzi.

Hata kama pasingekuwepo na mawakala bado mchakato wa kupiga na kuhesabu kura ulikuwa wa wazi kabisa. Kama ulishiriki kupiga kura utakuwa shahidi. Isitoshe siyo wote wa Tume, walioshiriki katika mchakato wana mapenzi na CCM. Ungekuwa mchambuzi makini ungewauliza baadhi wa wasimamizi au wasaidizi wa baadhi ya vituo kupata ukweli.

TUJIFUNZE KUTAFUTA UKWELI ILI KUONDOKANA na HISIA OVU
Umeandika ujinga sana
tuulize sisi tuliokuwa ndani ya vyumba vya kura
hakukuwa na uchaguzi kweli
ulikuwa uhuni tuu
ww bwabwaja kwakuwa huna ulijualo
 
CCM wameamua kukomba kila kitu.
Mliambiwa mkakataa! Kwamba ifikapo 2020, vyama vya upinzani kalasi - kufia mbali! Mkadanganywa na wahuni waliokuwa wanamfatilia Lissu kwenye mikutano yake wakipiga kelele! Na sisi tulihudhuria mikutano hiyo yote, tukisikiliza matusi tu (hatukusikia sera yoyote). Tarehe 28/10/20 tukaamua.
 
Hili siyo la upinzani ni la watanzania wote sababu faida ya demokrasia ni kwa watanzania wote sasa inatoweka na watanzania wenzetu wanatumika kuondoa mfumo wa vyama vingi na kuingiza mfumo wa chama kimoja kibabe
Aliekuambia kuwa ni wote tunaona hakuna demokrasia ni nani?

Wale wanaoona hakuna ndio waingie barabarani wala sio wote

Sent using Jamii Forums mobile app by My phone

[/url] Eti nabakia Africa. [/url]
 
Umeandika ujinga sana
tuulize sisi tuliokuwa ndani ya vyumba vya kura
hakukuwa na uchaguzi kweli
ulikuwa uhuni tuu
ww bwabwaja kwakuwa huna ulijualo
Kama ulikuwa ndani ya chumba cha kura na ukashuhudia kura zinaibiwa usichukue hatua yoyote, hukufaa kuwepo hapo. Na kama ulilipwa kwa kazi hiyo nenda katubu na kurudisha malipo hayo.
 
Kama ulikuwa ndani ya chumba cha kura na ukashuhudia kura zinaibiwa usichukue hatua yoyote, hukufaa kuwepo hapo. Na kama ulilipwa kwa kazi hiyo nenda katubu na kurudisha malipo hayo.
Ingekuwa hatua zinachukulika kirahisi hivyo wizi usingetokea
 
Yaani nasikiliza matokeo hapa nahisi kama roho inataka kutoka.

Chama chochote cha upinzani kupata hata kiti kimoja bungeni ni ndoto labda iwe kwa kuridhisha tu wanananchi kuwa kuna demokrasia😡😡😡

Tuendelee tu kukamilisha ratiba.
mkuu una roho ngumu kweli, hadi unasikiliza kabisa. sijui unatafuta nini
 
Yaani nasikiliza matokeo hapa nahisi kama roho inataka kutoka.

Chama chochote cha upinzani kupata hata kiti kimoja bungeni ni ndoto labda iwe kwa kuridhisha tu wanananchi kuwa kuna demokrasia😡😡😡

Tuendelee tu kukamilisha ratiba.
Iambie roho isitoke. Itulie tuliiiiii..... Maisha yanaendelea hata baada ya uchaguzi
 
Yaani nasikiliza matokeo hapa nahisi kama roho inataka kutoka.

Chama chochote cha upinzani kupata hata kiti kimoja bungeni ni ndoto labda iwe kwa kuridhisha tu wanananchi kuwa kuna demokrasia😡😡😡

Tuendelee tu kukamilisha ratiba.
Watanzania tumeamua kuwa hatutaki tena upinzani. Wewe umeona wapi mwakilishi wako anakwenda bungeni kulumbana tu na kuleta vimbwenga ila maendeleo hapeleki jimboni kwake? Yaani mtu anaona ujiko kukamatwa na kufungwa huku akichekelea kuandikwa mitandaoni, si uhuni huu? Wapinzani waliopita walikuwa very useless, hakuna hata mmoja aliyestahili kuwa kiongozi.
 
Umeandika ujinga sana
tuulize sisi tuliokuwa ndani ya vyumba vya kura
hakukuwa na uchaguzi kweli
ulikuwa uhuni tuu
ww bwabwaja kwakuwa huna ulijualo
Wapi u;likuwa, wewe unatudanganya tu hapa
 
Back
Top Bottom