ACT kama NCCR wanataka waachiwe majimbo wayauze kwa ccm, lakini wanataka CHADEMA ikishinda wagawane ruzuku kwasababu eti iliwaachia majimbo.
Kwa msingi huo, Kila chama kipambane kivyake, ili kila mmoja avune alichopanda.
Waungane ili iweje?!
Malalamiko yao ilikuwa kwamba, wakati wa UKAWA Chadema iliwatumia, sasa unadhani hiyo dhana itawaisha?!
Waliionea wivu CHADEMA na kuanza kuihujumu kwa kupeleka uongo huko ccm ,kwasasa kila mtu aende kivyake.
Ukipigwa, ujue ulipigwa kihalali, na ukishinda tembea kifua mbele.
ACT ikishinda Zanzibar haita share madaraka na yeyote, kila mmoja aweke nguvu anapoona anakubalika. Hakuna haja ya kuungana kisha muanze kuoneana wivu na kuanza kusalitiana.
Akishinda sawa, na ukishindwa usilaumu muungano wala nini ukae mbali.
CCM hawataki kuungana na chama chochote, kwanini nyie muungane?!
Walipaswa waungane 5 yeas kabla ya uchaguzi, lakini sio wiki moja kabla ya uchaguzi, hii itawaletea shida.
Kila chama kipige push up zake. Kikapambane kivyake, wengi wanafiki.
Hasa Mbatia na Zitto ni wanafiki sana.
Mbatia anajiona bonge la mwanasiasa, na alijiona kaibeba CHADEMA alipokuwa UKAWA.
Zitto hakutaka UKAWA akiamini angeweza bila UKAWA, leo muungano wa nini?
Lipumba wote mnafahamu alivyo msaliti na kaishiwa hana cha kuchangia kwenye muungano, hivyo aachwe, hata asijadiliwe.